Tuesday, June 30, 2009

Dawa zimemuua Michael Jackson?








KUNA taarifa kwamba, Michael Jackson alikuwa anatumia Paundi 30,000 kwa mwezi kwa ajili ya kununua dawa.

Kwa ujumla, katika siku za mwisho za uhai wake, Mfalme wa POP alikuwa akitumia dawa nyingi kwa mara moja na zenye nguvu sana hivyo huenda zimechangia kusababisha kifo chake.

Inadaiwa kwamba mwanamuziki huyo alikuwa anachanganya dawa hata ambazo kidaktari hairuhusiwi.


Soma hapo chini

DESPERATE Michael Jackson was spending £30,000 a month on prescription drugs, it was reported yesterday.

The ailing Thriller star was said to have consumed “mountains of medication” as he battled numerous disorders in the year leading up to his death.

Many prescriptions were bought under the fictitious name Omar Adams.
As well as the narcotic pain reliever Vicodin, 50-year-old Jacko gorged on other drugs like muscle relaxant Soma and sedative Xanax.




Soma na hii

Michael Jackson was taking a devastating cocktail of drugs that should never have been combined with each other in the weeks before his sudden death, it has emerged.



The singer was said taking three powerful painkillers all at the same time, when more than one is potentially fatal, and was also consuming vast quantities of other pills every day.



It is claimed Jackson, 50, was injected with the powerful painkiller Demerol - a synthetic drug similar to morphine - moments before he collapsed and died from a massive heart attack.



Sources cited by The Sun claim the star was having three of these injections every day but was also taking two other painkillers Dilaudid and Vicodin. None should ever be combined with other drugs.



On top of this deadly combination, Jackson was also taking a host of other medications as he battled to get fit and healthy ahead of his comeback concerts in Britain next month.



They included the muscle relaxant Soma, sedative Xanax, anti-depressent Zoloft, Paxil for anxiety and the heartburn pill Prilosec, it is claimed.



Such a huge amount of drugs would have been dangerous for anyone but even more so for Jackson, who at 5ft11 weighed only nine stone and whose health had long been a concern.

Saturday, June 27, 2009

Viatu vya Michael Jackson vinamtosha nani?





Michael Jackson enzi hizo





Michael baada ya 'kujifanyia ukarabati' wa pua

Michael Jackson akiwa na baba yake mzazi Joe Jackson mwaka 2005

Michael alipotunukiwa shahada ya heshima

AMEAGA dunia akiitwa Mfalme wa muziki wa POP duniani, hakuna kama yeye, na huenda hatatokea kama yeye.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 50, nyota yake katika muziki ilianza kung'ara akiwa na umri wa miaka 11 katika kundi la Jackson five.
Kwa kuzingatia historia hiyo, alitumia takribani miaka 40 kati ya 50 katika muziki na ameaga dunia wakati wapenzi wake wanasubiri maonyesho yaliyolenga kumrudisha tena kwenye ramani ya muziki kama ilivyokuwa katika miaka ya 80's alipotoa albamu ya Thriller.
Nani atavaa viatu vyake? Kuna mwanae yeyote atatimiza ule usemi 'like father like Son?'
Michael Jackson ameacha watoto watatu, Michael Joseph Jackson Jr, Paris Michael Katherine Jackson, na Prince Michael Jackson.

Friday, June 19, 2009

Rubani alivyomaliza ubishi kwenye ndege

An illiterate woman boarded a plane from Enugu to Abuja in Nigeria .
She was booked for an economy class seat. Just after the plane took-off, the woman stood up and went to sit in the first class cabin.
The flight attendant went to ask her to go back and sit in economy class because that's where the ticket allowed her to sit but she refused.
She had paid and wanted the best seat. Then the attendant informed the Jnr. pilot.
The Jnr. pilot went and spoke with the lady and she still refused.
Then the Jnr. pilot went to inform the chief pilot. The chief pilot said, I am married to an illiterate I'll go and talk to her.
The chief went and whispered some words to the woman and she peacefully stood-up and went to her economy class seat..
The attendant and Jnr. pilot surprisingly asked, sir what did you tell her?
The chief pilot said: "Easy guys, I just told her that first class is not going to Abuja , only economy class is"!!!

Wednesday, June 10, 2009

SMS zamuumbua mume mkware

MWANAMUME mmoja mkware nchini Uturuki aliumbuka vibaya baada ya kugundua kuwa mwanamke aliyemfungia safari kwenda kukutana naye baada ya kutongozana kwa kutumia ujumbe wa simu kwa muda mrefu alikuwa ni mkewe aliyekuwa akimchunguza kama ana kimada nje.

Mke wa mwanaume huyo mkazi wa mji wa Trabzon, nchini Uturuki alikuwa akimshuku mumewe kuwa na kimada nje kutokana na mabadiliko ya tabia zake aliyoyaona.

Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina moja la Hulya alisuka mpango wa kupima uaminifu wa mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Murat.

Hulya mwenye umri wa miaka 22 ili kujua kama mumewe ana kimada nje aliamua kuchukua simu ya ndugu yake na kuanza kumtumia mumewe meseji za kimapenzi akijifanya kuwa yeye ni mwanamke aliyevutiwa naye na anataka wawe na uhusiano wa kimapenzi.

Mumewe imani ilimshinda na alinasa kwenye mtego huo na kuanza kujibu meseji hizo kwa meseji kibao za mapenzi mpaka kufikia kupanga siku na sehemu ya kukutana ili waanze kujivinjari.

Mume huyo bila kujua kuwa mwanamke aliyekuwa akitumiana naye meseji alikuwa ni mkewe, alimuaga mkewe kuwa anatoka kidogo usiku kuonana na rafiki yake na atachelewa kurudi.

Huku akiwa na shauku kubwa ya kumuona mwanamke aliyekuwa akitongozana naye kwa simu, mume huyo mkware alipigwa na butwaa baada ya kuona mwanamke aliyejitokeza alikuwa ni mkewe tofauti na hesabu zake alizokuwa akipiga.

Kwa hasira mume huyo alimshushia kipigo mkewe hapo hapo na kusababisha polisi waliokuwa wakipita karibu na eneo la tukio kuingilia kati na kumkamata mume huyo.

Hulya hakuwa na nia ya kumfungulia mashtaka mumewe pamoja na kwamba alimjeruhi lakini polisi waliomkamata mumewe waliamua kumfungulia mashtaka.

Watanzania waisubiri hotuba ya JK

KUANZIA saa kumi jioni leo Rais Jakaya Kikwete atalihutubia taifa akiwa mjini Dodoma.
Rais atazungumza na wabunge na wazee wa mkoa wa Dodoma.
Bila shaka watanzania wanasubiri kwa hamu atakayosema JK kwa kuwa huenda atatoa tathimini ya mambo mengi yanayoligusa taifa wakati huu wa mtikisiko wa uchumi duniani.
Utamu wa hotuba ya JK pia unatokana na ukweli kwamba, anazungumza na wabunge siku moja kabla ya Waziri wa Fedha na uchumi kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010.

Tuesday, June 9, 2009

Rais Bongo kafariki dunia

Rais Omar Bongo na mkewe, Edith
HATIMAYE Serikali ya Gabon imetangaza kuwa Rais Omar Bongo kaaga dunia.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo amelitangazia taifa hilo msiba huo, ulinzi umeimarishwa, mipaka ya nchi hiyo ya anga, ardhi na bahari imefungwa.
Rais huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 42.
Rais huyo amefariki dunia wakati akipata tiba ya saratani jijini Barcelona nchini Hispania.
Ameaga dunia takribani miezi mitatu tangu mkewe, Edith Lucie Bongo Ondimba (45) kufariki dunia Machi 14 mwaka huu wakati akipata tiba Rabat nchini Morocco.
Edith ni binti mkubwa wa Rais wa Congo, Denis Sassou Nguessou.
Bongo na Edith walifunga ndoa mwaka 1990.
Edith aliuguzwa kwa miezi kadhaa nchini Morocco, na umma haukutangaziwa sababu za kifo chake.
Mwanaharakati huyo wa mapambano dhidi ya ukimwi alikuwa mke wa pili kwa Bongo, mke wa kwanza wa Rais huyo alikuwa , Josephine Nkama.

Choki kang'oka T- Respect?

KUNA taarifa zinazodai kuwa mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi nchini Ali Choki, a.ka Mzee wa Farasi, a.k.a Mzee wa Kijiko kabwaga manyanga katika bendi ya T-Respect.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Choki yupo kwenye mchakato wa kuifufua bendi yake ileeee
Kama kuna mwenye nyuuz zaidi weka mambo hadharani.

wake wa 'wakubwa'

Mke wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Sarah Brown(wa kwanza kushoto), mke wa Rais wa Ufaransa, Carla Bruni(katikati) na mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama wakiwa katika shughuli ya kumbukumbu iliyoitwa D-day nchini Ufaransa Juni 6.
Hivi kunapokuwa na mkusanyiko wa aina hiyo ni lazima mikono iwekwe hivyo?
Au ni kwa sababu tu nature ya binadamu kwamba wasingeweza kuiweka tofauti na walivyoiweka?

Monday, June 8, 2009

Rais Bongo yupo hai


SERIKALI ya Gabon imekanusha taarifa kwamba Rais wa nchi hiyo, Omar Bongo(73) amefariki dunia.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo ametangaza kuwa Rais Bongo yupo hai hospitalini, na ameonana naye leo asubuhi.
Bongo ni Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kuliko marais wote Afrika.
Alianza kuiongoza nchi hiyo mwaka 1967 hivyo amekuwa madarakani kwa miaka 42.
Rais Bongo yupo Barcelona nchini Hispania anapata tiba ya saratani ya utumbo.

Soma hapo chini
Gabon's President Omar Bongo, Africa's longest-serving ruler, is not dead, the country's prime minister said Monday, contradicting reports from Gabonese and French media.

Omar Bongo is Africa's longest-serving ruler.

Prime Minister Jean Eyeghe Ndong "deplored" French media reports that Bongo had died, saying he had met the president Monday morning.


He vowed to lodge a protest with the French authorities about "repeated leaks in the French press."


Bongo, 73, has been receiving treatment for intestinal cancer at the Quiron clinic in Barcelona, Spain, according to the Gabonews agency, which also reported Bongo's death earlier.


Spain's Foreign Ministry confirmed to CNN that Bongo is alive.


He is in Quiron hospital in Barcelona, Spain for a "comprehensive health check," the prime minister said in a statement.


"This morning I visited the President, accompanied by the President of the National Assembly, the Foreign Minister, the head of the President's cabinet and senior members of the presidential family and after a meeting with the medical team we can confirm that the President is alive," the statement said.

Sababu za MKE kumsaliti MUME

KUNA mdau kanitumia hii, sijafanya utafiti kufahamu kama ni kweli au hapana

Women, just as men, have affairs. Although statistically men have affairs more often than women do, wives still cheat.

In fact, the number of wives cheating on husbands has risen dramatically over the past few years.

Currently, new studies now show that between 35% and 40% of all wives cheat on husbands while the statistics for men are between 40% and 50%.
If you suspect your wife is having an affair, it could be for any number of reasons, five we listed below for your information.

1. Lack of Attention

Women typically love attention. Therefore, when they feel they are being ignored, they might look somewhere else.

For instance, if a husband comes home each night expecting dinner to be on the table, the house cleaned, and the kids finished with homework, he walks in but passes the wife without a hug, kiss, or acknowledgement for a job well done, she is going to feel isolated and ignored.

Now, when that same woman visits the grocery store and a man shopping in the same section smiles at her or perhaps picks up something she dropped, she immediately feels important.
2. Quality Time

Even if a husband were spending time at home or with the wife, if he is constantly working, reading, doing chores outside, and so on, it means his wife is not getting any quality time.

Most women want and need special time such as a date night. With this, she is pampered and given the husband’s full attention.
3. Lack of Confidence

Over time, couples can become so comfortable with one another that they forget the importance of dating and affection.

Eventually, a wife may begin to feel a lack of self-confidence. When a woman gets into this kind of rut, she no longer feels beautiful and sexy, as she once did.

If another man is paying attention to her, adoring her, offering her compliments, or inviting her to lunch or dinner, she suddenly gains confidence, feeling again like a woman.

4. Lack of Intimacy

An old belief is that men are more sexual than women are.

The truth is that many women are just as sexual than the husband is, if not more so.

Therefore, if the marriage has become stale and stagnant, otherwise boring in the bedroom, some women will look for physical satisfaction outside the home in the form of an affair.

5. Finances

Depending on the situation, some couples are overwhelmed with bills.

In addition to the mortgage, there is the cost of the children, school, groceries, sports, you name it, and the money is gone.

This means the wife seldom has extra to buy a new dress, go out with friends, or simply splurge on herself.

Although this challenge can be hard to fix, but not impossible, if another man were offering her bling, taking her places, and showering her with gifts, she may feel inclined to cheat.

Maiti, mabaki ya ndege vyaokotwa baharini

Mabaki ya ndege ya Air France iliyoanguka baharini usiku wa kumkia Jumatatu iliyopita

Askari wa kikosi cha wanamaji cha Brazil wakiokota mizigo ya abiria waliokufa katiak ajali ya ndege Air France iliyoanguka ikiwa na watu 228

Kiti cha ndege(kushoto chini) na mizigo ya abiria waliokufa kwenye ajali ya ndege iliyokuwa ikitoka Brazil kwenda Ufaransa usiku Jumapili iliyopita.

Airbus 330-200 ya Shirika la Ndege la Ufaransa
NI ajali kubwa zaidi ya ndege ya abiria tangu mwaka 2001, imeua watu 228.
Hadi leo asubuhi miili 15 imeoktwa ikielea katika bahari ya Atlantic.
Ndege hiyo Airbus 330-200 ilianguka baada ya kutokea hitilafu katika mfumo wa umeme.

Kabla ya kuanguka ilituma message 24 kueleza kuhusu tatizo hilo kwenye mfumo wa uendeshaji wa ndege hiyo inayosemekana kuwa ni salama zaidi kati ya ndege zinazotumika sasa.
Soma zaidi hapo chini

Fourteen of those messages were sent within the space of one minute, from 3.10am BST to 3.11am BST, a briefing in Paris was told today.

The messages showed 'inconsistencies' between measured velocities and indications of systems failures including the autothrust and autopilot, the investigators said.

All 228 people on board, including 12 crew, a baby and seven children, are thought to have perished in the world's worst aviation.

Saturday, June 6, 2009

Papa amtimua Askofu wa Same

TAARIFA kuwa Makao Makuu ya Kanisa katoliki Vatican yamemuondoa madarakani Askofu wa Jimbo la Same zimenisikitisha.
Ni muendelezo wa habari mbaya kuhusu kanisa hilo, hivi karibuni, polisi mkoani Dodoma walimkamata paroko wa ... anayetuhumiwa kumbaka na kumjaza mimba msichana aliyekuwa akiuza katika duka la kanisa.
Kwa kuzingatia taarifa ya Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Joseph Chennoth, Askofu Koda hatarudishwa kwenye madaraka hayo, atateuliwa askofu mwingine.
Koda aliteuliwa mwaka 1999 kuongoza jimbo la Same mkoani Kilimanjaro.
Vatican imemtaka aache kazi za kitume, afanye shughuli zake binafsi za mafunzo.
Alizaliwa Desemba 9, 1957, alipata daraja la upadre Juni 25, 1987 na alisimikwa kuwa askofu wa Same May 30, 1999.

Kumekucha wazazi CCM

MCHAKATO wa kumpata Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi unaendelea katika ukumbi wa Kilimani uliopo Uzunguni mjini Dodoma.
Wagombea watatu wanachuana kuwania wadhifa huo akiwamo Esther Nyawazwa, Athumani Mhina, na Abdallah Bulembo.
Saa chache zilizopita, Mwenyekiti wa CMM, Rais Jakaya Kikwete alifungua mkutano na kuwataka wagombea wazingatie maadili ya chama hicho tawala.

Mabomu 11 yalipuliwa Mbagala

WAHANDISI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wamemaliza kazi ya kulipua mabomu 11 katika kambi ya jeshi hilo iliyopo Mbagala Kuu, katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
kazi hiyo ilianza saa nne asubuhu, iliisha saa 5.30, wakazi wengi wa Mbagala wameyahama kwa muda makazi yao
Watu 17 wamelazwa katika hospitali ya Temeke kwa sababu ya mshituko.

Friday, June 5, 2009

Maji kukatika Dar es Salaam kesho

WAKAZI wengi wa Dar es Salaam na Bagamoyo kesho watakosa huduma ya maji ya bomba kwa saa 12.
Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO) kesho itazima mtambo wa Ruvu Chini kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Kwa mujibu wa Dawasco, huduma ya maji itakuwa kama kawaida kuanzia Jumapili asubuhi.

Mwizi akikukaba kwenye mashine ya ATM

MDAU kanitumia ujumbe akidai ni ushauri endapo mwizi atakukaba wakati unachukua hela kwenye mashine ya ATM. Mdau huyo anasema ukitekeleza ushauri huo mwizi atajuuta kukufahamu.
Soma hapo chini.
WHEN A THIEF FORCES YOU TO TAKE MONEY FROM THE ATM, DO NOT ARGUE OR RESIST, YOU MIGHT NOT KNOW WHAT HE OR SHE MIGHT DO TO YOU.

WHAT YOU SHOULD DO IS TO PUNCH YOUR PIN IN THE REVERSE, I.E. IF YOUR PIN IS 1254, YOU POUNCH 4521.

THE MOMENT YOU PUNCH IN THE REVERSE, THE MONEY WILL COME OUT BUT WILL BE STUCK INTO THE MACHINE HALF WAY OUT AND IT WILL ALERT POLICE WITHOUT THE NOTICE OF THE THIEF.

EVERY ATM HAS IT, IT IS SPECIALLY MADE TO SIGNIFY DANGER AND HELP.
NOT EVERYONE IS AWARE OF THIS. FORWARD THIS TO ALL YOUR FRIENDS AND THOSE YOU CARE FOR!

Wajawazito msivute sigara

Sigara na uvutaji wake huwathiri watumiaji wake popote walipo.
Mjamzito pamoja na kujidhuru yeye mwenyewe, humdhuru pia mtoto aliye tumboni.

Wajawazito walio wavutaji huweza kuzaa mtoto mwenye uzito wa chini "kabichi" au"njiti', mtoto pia anaweza kupata matatizo ya mapafu "pneumonia" na kudhoofu afya kwa ujumla.

Vile vile hata kama mjamzito havuti sigara, wana familia wengine wanaweza kumdhuru iwapo watakuwa wanavuta.

Wanawake na watoto wengi hudhururiwa na moshi wa sigara ndani ya majumba yao.

Hasa pale baba anapomaliza nusu paketi akiwa ndani ya nyumba yao! Kina baba msiyachafue mazingira ya nyumbani iwapo hamuwezi kabisa kuacha uvutaji.

Pombe ni sumu ya viungo vinavyokuwa. Inaponywewa na mjamzito huingia katika mishipa ya damu ya mtoto kupitia "placenta".
Pombe hudhuru viungo dhaifu vya mtoto vinavyokuwa.

Watoto wanaozaliwa na wanawake walevi huwa na tatizo la ukuaji dhaifu wa ubongo hivyo kuwafanya wasiwe na akili "nzuri".
Uzito mdogo wakati wa kuzaliwa, matatizo ya moyo,figo na macho, matatizo ya mifupa pia huweza kuwapata watoto hawa.

Hata kiasi kidogo cha pombe kinatosha kabisa kuwa na madhara kwa mtoto aliye tumboni.
Ni vizuri kuacha kabisa vinywaji hivi iwapo unampenda atakayekuwa mwanao siku zijazo.

Kwa wajawazito achana na marafiki walevi na kuwa mkali kwa mume au jamaa atakayekuletea zawadi ya pombe.
Usitembelee kabisa sehemu zinazouzwa pombe, wala usikodolee macho matangazo ya pombe.

Wednesday, June 3, 2009

Nukuu ya leo

"You don't marry someone you can live with, you marry the person YOU CANNOT live WITHOUT.

Rais Obama atimiza ahadi kwa mkewe

Rais Barack Obama na mkewe, Michelle wakijiandaa kuondoka kwenye ngome ya kijeshi ya Andrews kwenda kupanda ndege waende 'OUT' New York Jumamosi iliyopita.

Rais Obama na mkewe 'wakikwea pipa' kwenda kujivinjari New York Jumamosi iliyopita

Mapumziko yamekwisha, wamerudi nyumbani White House, Washington DC
RAIS Barack Obama ametimiza ahadi aliyoitoa kwa mkewe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Marekani.
Obama alimuahidi Michelle kwamba, mikiki mikiki ikiisha atampeleka OUT ya usiku mmoja, ndivyo alivyofanya.
Walikwenda Manahattan jijini New York Jumamosi iliyopita, wakalala huko, wakarudi White House Jumapili.
Msafara wa Rais Obama ulikuwa na ndege mbili, moja alipanda yeye na mkewe.
Nyingine walipanda wasaidizi wake na waandishi wa habari. Kulikuwa pia na helikopta kwa ajili ya ulinzi.

Chanzo cha ajali ya ndege huenda hakitajulikana

Mume wa mama huyu alikuwa miongoni mwa abiria kwenye ndege iliyoanguka baharini

Huzuni, majonzi
MAOFISA wa Serikali ya Ufaransa wamesema, kisanduku cha kumbukumbu kwenye ndege iliyoanguka baharini nchini Brazil huenda hakitapatikana.
Kwa mujibu wa maofisa hao, ndege hiyo Airbus 330-200 mali ya Shirika la Ndege la Ufaransa ilianguka sehemu mbaya hivyo ni vigumu kukipata.
Wakati inaanguka, ndege hiyo ilikuwa na watu 228, wote wamekufa.
Ilianguka saa nne baada ya kuruka nchini Brazil, chanzo cha ajali hiyo bado ni utata.

Haki za raia anapokamatwa

Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
Mwulize jina lake
Mwulize namba yake ya uaskari
Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.

Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.

Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.

Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.

Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.

Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.

Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.

Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Tuesday, June 2, 2009

Breaking News

Sehemu ya ndani ya Airbus 330-200
MABAKI ya ndege yameokotwa baharini katika eneo linalohisiwa kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa ilianguka wakati ikitoka Brazil kwenda Ufaransa Jumapili usiku.


Ndege hiyo ilipotea kwenye vyombo vya kuongozea ndege saa nne baada ya kuondoka Brazil na haitathibitika kama mabaki yaliyookotwa ni ya ndege hiyo.


Soma kwa kirefu hapo chini.


BRAZILIAN air force aircraft searching the Atlantic Ocean on Tuesday for a missing Air France flight that had been carrying 228 people have found debris from a plane, an air force spokesman
said.


The 'small remains' were located 650 kilometres northeast of Brazil's Fernando do Noronha island.


The plane went missing on Monday on route from Rio de Janeiro to Paris with 228 people on board.


Reports from Brazil say that planes continue to search the Atlantic Ocean, with French and Brazilian military aircraft and ships involved in the search.


It could not immediately be confirmed that the debris were from Air France flight AF 447, spokesman Jorge Amaral told reporters.


Among the pieces of wreckage located was an aircraft seat, he said.


'The search is continuing because it's very little material in relation to the size' of the Air France Airbus A330, he said.


Mr Amaral added that officials needed 'a piece that might have a serial number, some sort of identification' to be sure that it came from the missing airliner.


The Fernando do Noronha archipelago lies 370 kilometres off Brazil's north-east coast.


Brazilian media outlets had earlier reported that debris from the missing Air France passenger jet had been sighted floating on the Atlantic Ocean by the crew of a French freighter.


The Douce France is reported to be in the same area off the coast of Senegal where a Brazil TAM airline pilot was also reported to have seen a burning piece of wreckage, reported news.com.au.

'Hakuna uwezekano kuwapata wakiwa hai'

Ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa Airbus 330-200
NI maafa sekta ya anga, na msiba uliogusa takribani mabara yote.
Mabaki ya ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa inayoaminika kuwa imeanguka katika bahari ya Atlantiki bado hayajapatika.
Serikali ya ufaransa imesema, uwezekano wa kuwapata watu 228 waliokuwamo kwenye ndege hiyo ni MDOGO SANA.
Ndege hiyo, Airbus 330-200 ilianguka jumapili usiku saa nne baada ya kuondoka Reo de Janeiro, Brazil kwenda Paris Ufaransa.
Wakati inaanguka ilikuwa futi 35,000 kutoka usawa wa bahari ikiwa na raia wa nchi 32.
Kazi ya kutafuta mabaki baharini inaendelea.

Monday, June 1, 2009

Padre ahama kanisa aendelee na mahaba

Picha zilizochapishwa kwenye jarida zikimuonyesha Padre Alberto Cutie akijinafasi na mpenzi wake ufukweni
Padre na mpenzi wake wakijinafsi ufukweni
Padre wa Kanisa Katoliki, Alberto Cutie

Padre Cutir akiongoza misa ya mazishi

Padre Cutie akiwa na mpenzi wake, Ruhama Canellis wakati wa hafla ya kumkaribisha padre huyo kwenye kanisa la Anglikana nchini Marekani, Alhamisi iliyopita.


PADRE wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Miami nchini Marekani amehamia kanisa la Anglikana ili aendelee na mahaba na amuoe mpenzi wake.


Padre Alberto Cutie(40) amekiri kuwa na mpenzi,Ruhama Canellis(38), alikuwa naye wakati akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi iliyopita mjini Miami.


Mume mtarajiwa wa mwanamke huyo aliyeachana na mumewe,amesema, ataendelea na kazi ya kuchunga kondoo wa bwana katika kanisa la Anglikana.


Mwanzoni mwa mwezi huu alisema, yeye ni mpenzi wa mwanamke huyo kwa miaka miwili na kwamba, kabla ya hapo walikuwa marafiki kwa muda mrefu.


"Ninaamini nimezama kwenye penzi, ninaamini kwamba nimejitahidi kukabiliana na hili, kati ya mapenzi yangu kwa Mungu, mapenzi yangu kwa kanisa na mapenzi yangu kwa ajili ya utumishi"amesema.


Kanisa Katoliki Miami Beach lilimfukuza mtumishi huyo wa Mungu baada ya jarida linaloandikwa kwa lugha ya kihispania,TVnotas, kuchapisha picha zilizopigwana mapaparazi kwa zaidi ya siku tatu.


Picha hizo zilizomuonyesha Padre huyo akiwa katika mahaba ikiwa ni pamoja na kumkumbatia,kumbusu mpenzi wake na kuwa katika mazingira ya kingono katika ufukwe wa bahari kwenye pwani ya Florida.

Ronaldo akijinafasi Italia



NYOTA wa Barcelona, Messi 'alimfunika' mshambuliaji tegemeo wa Man United, Ronaldo kwenye mpambano wa fainali Ligi la Mabingwa Barani Ulaya.
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kupunguza maumivu hayo, Ronaldo amekwenda kupumzika nchini Italia.
Picha hizo juu zinamuonyesha CR7 akijinafasi kwa kuogelea kwenye ufukwe wa Porto Cervo, Sardinia nchini humo.
Kuna tetesi kwamba mchezaji huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya Paundi milioni 70 anajiandaa kuihama Man U.