Wednesday, June 10, 2009

Watanzania waisubiri hotuba ya JK

KUANZIA saa kumi jioni leo Rais Jakaya Kikwete atalihutubia taifa akiwa mjini Dodoma.
Rais atazungumza na wabunge na wazee wa mkoa wa Dodoma.
Bila shaka watanzania wanasubiri kwa hamu atakayosema JK kwa kuwa huenda atatoa tathimini ya mambo mengi yanayoligusa taifa wakati huu wa mtikisiko wa uchumi duniani.
Utamu wa hotuba ya JK pia unatokana na ukweli kwamba, anazungumza na wabunge siku moja kabla ya Waziri wa Fedha na uchumi kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010.

No comments:

Post a Comment