Monday, June 1, 2009

Padre ahama kanisa aendelee na mahaba

Picha zilizochapishwa kwenye jarida zikimuonyesha Padre Alberto Cutie akijinafasi na mpenzi wake ufukweni
Padre na mpenzi wake wakijinafsi ufukweni
Padre wa Kanisa Katoliki, Alberto Cutie

Padre Cutir akiongoza misa ya mazishi

Padre Cutie akiwa na mpenzi wake, Ruhama Canellis wakati wa hafla ya kumkaribisha padre huyo kwenye kanisa la Anglikana nchini Marekani, Alhamisi iliyopita.


PADRE wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Miami nchini Marekani amehamia kanisa la Anglikana ili aendelee na mahaba na amuoe mpenzi wake.


Padre Alberto Cutie(40) amekiri kuwa na mpenzi,Ruhama Canellis(38), alikuwa naye wakati akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi iliyopita mjini Miami.


Mume mtarajiwa wa mwanamke huyo aliyeachana na mumewe,amesema, ataendelea na kazi ya kuchunga kondoo wa bwana katika kanisa la Anglikana.


Mwanzoni mwa mwezi huu alisema, yeye ni mpenzi wa mwanamke huyo kwa miaka miwili na kwamba, kabla ya hapo walikuwa marafiki kwa muda mrefu.


"Ninaamini nimezama kwenye penzi, ninaamini kwamba nimejitahidi kukabiliana na hili, kati ya mapenzi yangu kwa Mungu, mapenzi yangu kwa kanisa na mapenzi yangu kwa ajili ya utumishi"amesema.


Kanisa Katoliki Miami Beach lilimfukuza mtumishi huyo wa Mungu baada ya jarida linaloandikwa kwa lugha ya kihispania,TVnotas, kuchapisha picha zilizopigwana mapaparazi kwa zaidi ya siku tatu.


Picha hizo zilizomuonyesha Padre huyo akiwa katika mahaba ikiwa ni pamoja na kumkumbatia,kumbusu mpenzi wake na kuwa katika mazingira ya kingono katika ufukwe wa bahari kwenye pwani ya Florida.

1 comment:

  1. Heri Padre Albeto umeamua jambo jema kuliko kumkosea Mungu kwa kufanya dhambi ukijidanganya watu hawakuoni.Mungu akutie nguvu katika utumishi wako....Amen

    ReplyDelete