Saturday, June 6, 2009

Papa amtimua Askofu wa Same

TAARIFA kuwa Makao Makuu ya Kanisa katoliki Vatican yamemuondoa madarakani Askofu wa Jimbo la Same zimenisikitisha.
Ni muendelezo wa habari mbaya kuhusu kanisa hilo, hivi karibuni, polisi mkoani Dodoma walimkamata paroko wa ... anayetuhumiwa kumbaka na kumjaza mimba msichana aliyekuwa akiuza katika duka la kanisa.
Kwa kuzingatia taarifa ya Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Joseph Chennoth, Askofu Koda hatarudishwa kwenye madaraka hayo, atateuliwa askofu mwingine.
Koda aliteuliwa mwaka 1999 kuongoza jimbo la Same mkoani Kilimanjaro.
Vatican imemtaka aache kazi za kitume, afanye shughuli zake binafsi za mafunzo.
Alizaliwa Desemba 9, 1957, alipata daraja la upadre Juni 25, 1987 na alisimikwa kuwa askofu wa Same May 30, 1999.

No comments:

Post a Comment