Sigara na uvutaji wake huwathiri watumiaji wake popote walipo.
Mjamzito pamoja na kujidhuru yeye mwenyewe, humdhuru pia mtoto aliye tumboni.
Wajawazito walio wavutaji huweza kuzaa mtoto mwenye uzito wa chini "kabichi" au"njiti', mtoto pia anaweza kupata matatizo ya mapafu "pneumonia" na kudhoofu afya kwa ujumla.
Vile vile hata kama mjamzito havuti sigara, wana familia wengine wanaweza kumdhuru iwapo watakuwa wanavuta.
Wanawake na watoto wengi hudhururiwa na moshi wa sigara ndani ya majumba yao.
Hasa pale baba anapomaliza nusu paketi akiwa ndani ya nyumba yao! Kina baba msiyachafue mazingira ya nyumbani iwapo hamuwezi kabisa kuacha uvutaji.
Pombe ni sumu ya viungo vinavyokuwa. Inaponywewa na mjamzito huingia katika mishipa ya damu ya mtoto kupitia "placenta".
Pombe hudhuru viungo dhaifu vya mtoto vinavyokuwa.
Watoto wanaozaliwa na wanawake walevi huwa na tatizo la ukuaji dhaifu wa ubongo hivyo kuwafanya wasiwe na akili "nzuri".
Uzito mdogo wakati wa kuzaliwa, matatizo ya moyo,figo na macho, matatizo ya mifupa pia huweza kuwapata watoto hawa.
Hata kiasi kidogo cha pombe kinatosha kabisa kuwa na madhara kwa mtoto aliye tumboni.
Ni vizuri kuacha kabisa vinywaji hivi iwapo unampenda atakayekuwa mwanao siku zijazo.
Kwa wajawazito achana na marafiki walevi na kuwa mkali kwa mume au jamaa atakayekuletea zawadi ya pombe.
Usitembelee kabisa sehemu zinazouzwa pombe, wala usikodolee macho matangazo ya pombe.
No comments:
Post a Comment