Saturday, June 27, 2009

Viatu vya Michael Jackson vinamtosha nani?





Michael Jackson enzi hizo





Michael baada ya 'kujifanyia ukarabati' wa pua

Michael Jackson akiwa na baba yake mzazi Joe Jackson mwaka 2005

Michael alipotunukiwa shahada ya heshima

AMEAGA dunia akiitwa Mfalme wa muziki wa POP duniani, hakuna kama yeye, na huenda hatatokea kama yeye.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 50, nyota yake katika muziki ilianza kung'ara akiwa na umri wa miaka 11 katika kundi la Jackson five.
Kwa kuzingatia historia hiyo, alitumia takribani miaka 40 kati ya 50 katika muziki na ameaga dunia wakati wapenzi wake wanasubiri maonyesho yaliyolenga kumrudisha tena kwenye ramani ya muziki kama ilivyokuwa katika miaka ya 80's alipotoa albamu ya Thriller.
Nani atavaa viatu vyake? Kuna mwanae yeyote atatimiza ule usemi 'like father like Son?'
Michael Jackson ameacha watoto watatu, Michael Joseph Jackson Jr, Paris Michael Katherine Jackson, na Prince Michael Jackson.

No comments:

Post a Comment