Wednesday, June 3, 2009

Chanzo cha ajali ya ndege huenda hakitajulikana

Mume wa mama huyu alikuwa miongoni mwa abiria kwenye ndege iliyoanguka baharini

Huzuni, majonzi
MAOFISA wa Serikali ya Ufaransa wamesema, kisanduku cha kumbukumbu kwenye ndege iliyoanguka baharini nchini Brazil huenda hakitapatikana.
Kwa mujibu wa maofisa hao, ndege hiyo Airbus 330-200 mali ya Shirika la Ndege la Ufaransa ilianguka sehemu mbaya hivyo ni vigumu kukipata.
Wakati inaanguka, ndege hiyo ilikuwa na watu 228, wote wamekufa.
Ilianguka saa nne baada ya kuruka nchini Brazil, chanzo cha ajali hiyo bado ni utata.

No comments:

Post a Comment