Tuesday, June 2, 2009

'Hakuna uwezekano kuwapata wakiwa hai'

Ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa Airbus 330-200
NI maafa sekta ya anga, na msiba uliogusa takribani mabara yote.
Mabaki ya ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa inayoaminika kuwa imeanguka katika bahari ya Atlantiki bado hayajapatika.
Serikali ya ufaransa imesema, uwezekano wa kuwapata watu 228 waliokuwamo kwenye ndege hiyo ni MDOGO SANA.
Ndege hiyo, Airbus 330-200 ilianguka jumapili usiku saa nne baada ya kuondoka Reo de Janeiro, Brazil kwenda Paris Ufaransa.
Wakati inaanguka ilikuwa futi 35,000 kutoka usawa wa bahari ikiwa na raia wa nchi 32.
Kazi ya kutafuta mabaki baharini inaendelea.

No comments:

Post a Comment