Rais Omar Bongo na mkewe, Edith
HATIMAYE Serikali ya Gabon imetangaza kuwa Rais Omar Bongo kaaga dunia.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo amelitangazia taifa hilo msiba huo, ulinzi umeimarishwa, mipaka ya nchi hiyo ya anga, ardhi na bahari imefungwa.
Rais huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 42.
Rais huyo amefariki dunia wakati akipata tiba ya saratani jijini Barcelona nchini Hispania.
Ameaga dunia takribani miezi mitatu tangu mkewe, Edith Lucie Bongo Ondimba (45) kufariki dunia Machi 14 mwaka huu wakati akipata tiba Rabat nchini Morocco.
Edith ni binti mkubwa wa Rais wa Congo, Denis Sassou Nguessou.
Bongo na Edith walifunga ndoa mwaka 1990.
Edith aliuguzwa kwa miezi kadhaa nchini Morocco, na umma haukutangaziwa sababu za kifo chake.
Mwanaharakati huyo wa mapambano dhidi ya ukimwi alikuwa mke wa pili kwa Bongo, mke wa kwanza wa Rais huyo alikuwa , Josephine Nkama.
No comments:
Post a Comment