Wednesday, June 3, 2009

Rais Obama atimiza ahadi kwa mkewe

Rais Barack Obama na mkewe, Michelle wakijiandaa kuondoka kwenye ngome ya kijeshi ya Andrews kwenda kupanda ndege waende 'OUT' New York Jumamosi iliyopita.

Rais Obama na mkewe 'wakikwea pipa' kwenda kujivinjari New York Jumamosi iliyopita

Mapumziko yamekwisha, wamerudi nyumbani White House, Washington DC
RAIS Barack Obama ametimiza ahadi aliyoitoa kwa mkewe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Marekani.
Obama alimuahidi Michelle kwamba, mikiki mikiki ikiisha atampeleka OUT ya usiku mmoja, ndivyo alivyofanya.
Walikwenda Manahattan jijini New York Jumamosi iliyopita, wakalala huko, wakarudi White House Jumapili.
Msafara wa Rais Obama ulikuwa na ndege mbili, moja alipanda yeye na mkewe.
Nyingine walipanda wasaidizi wake na waandishi wa habari. Kulikuwa pia na helikopta kwa ajili ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment