Saturday, May 30, 2009

Siku ya kihistoria

MUDA mfupi uliopita Rais Jakaya Kikwete amezindua mradi mkubwa wa maji yanayotoka Ziwa Viktoria kwenda Shinyanga, Kahama, na baadhi ya vijiji vya Geita, Kwimba, na Misungwi.
Rais kasema, leo ni siku ya kihistoria kwa maeneo hayo, na kwamba ndoto zimetimia.
Mradi huo ni mkubwa kuliko yote katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara ukiacha wa Afrika Kusini.
Umejengwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania, sh bilioni 242 Tsh, na hakuna hata senti moja ya wafadhili ilyotumika.
Umejengwa kwa miaka mitano, makandarasi watano wamesambaza mabomba yenye urefu wa kilomita 600.
Rais Kikwete kampongeza Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwa moyo wake wa kuthubutu, na amesema, Mkapa ni Shujaa.
Mkapa, na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa wamehudhuria sherehe za kuuzindua mradi huo.

Michael Jackson ahofu kuaga dunia

SARATANI inayomsumbua mfalme wa muziki wa POP, Michael Jackson, imesababisha ashindwe kutembea, na anahofu kuwa itamuua.
Ingawa madaktari wamemweleza kuwa saratani hiyo inatibika, ana mashaka kuwa 'itamuondoa'.
Seli za saratani zimeonekana kwenye kifua, pua na mkono.
Kuna taarifa kwamba, hatatibiwa kwa mionzi, sehemu zilizoathirika zitakuwa zinakatwa.

Friday, May 29, 2009

Miss Universe 2009

Washiriki wa shindano la Miss Universe 2009(Picha kwa hisani ya Michuzijr.blogspot.com)
WAREMBO 20 kesho watachuana kuwania taji la Miss Universe Tanzania 2009.
Warembo hao wapo kwenye maandalizi ya mwisho kwenye hoteli ya Belinda iliyopo kando ya barabara ya kwenda Whitesands Hotel.
Mshindi wa taji hilo linalozidi kupata umaarufu nchini atapatikana katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Hivi karibuni, muandaaji wa shindano hilo, Maria Sarungi alisema, kiny'ang'anyiro cha kumpata Miss Universe Tanzania ni kigumu kuliko cha kumpata Miss Tanzania, na kwamba shindano la dunia la kumsaka Miss Universe ni gumu kuliko la Miss World.

Msiba Dar es Salaam

MUME wa Mwandishi wa habari, Margareth Chambiri, amekufa katika ajali ya gari mjini Lindi.
Kwa mujibu wa ndugu wa Margareth, Aminata Juma, Kennedy Chambiri alikufa papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi wakati akienda katika ofisi za TANROADS mjini humo.
Inadaiwa kwamba Kennedy alikywa akiendesha Pick Up, alimpa lifti mwanamke aliyekuwa na mtoto, muda mfupi baadaye gari hiyo lilipinduka yeye (Kennedy) na mtoto huyo wakafa papo hapo.
Haijafahamika kama gari alilokuwa akiendesha liligonga mti, kitu au kugongana na gari lingine.
Maiti ya Kennedy imefikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo asubuhi.
Aminata amesema, wafiwa na waombolezaji watakutana nyumbani kwa marehemu Kawe kesho kuanzia saa nne asubuhi kwa ajili ya ibada ya mazishi itakayoanza saa saba mchana katika kanisa la wasabato Kinondoni.
Baada ya ibada, mwili utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirishwa Jumapili kwenda Tarime kwa ajili ya mazishi na maziko.
Mwili wa Kennedy utazikwa Jumatatu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, amen.
Kwa wasiomfahamu, Kennedy ni baba mzazi wa yule mtoto aliyeimba wimbo Tanzania eeeh, Martina Chambiri.

Maswali ya Dk Mwakyembe kwa Polisi



Taarifa ya Kamati hiyo maalum, kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima la tarehe 26 Mei, 2009 inanitaka nisitoe kauli zisizo za kitaalamu! Nina maswali kadhaa ya kuuliza:

Kwanza, ni utaalamu gani unahitajika kuelezea kitu kilichomsibu mtu?
Mathalan, nyumba yangu imeungua moto. Kwa mantiki ya kamati hiyo maalum, siruhusiwi kuelezea kuwa chanzo cha moto kilikuwa kibatali au mshumaa, mpaka nimsubiri Kombe na timu yake ya “wataalam” waje kupiga ramli kama walivyofanya kwenye ajali yangu?

Pili, tumepata ajali nyingi nchini na abiria na madereva wamekuwa chanzo muhimu cha taarifa kwa Polisi kujua chanzo cha ajali.
Kwa nini vigezo na taratibu zigeuke kwenye ajali ya Dk. Mwakyembe peke yake (ambapo wahusika wakuu katika ajali hiyo hawatakiwi kuongea)?

Tatu, kama suala hapa ni uelewa wa sheria husika, mwenendo wa upelelezi na wa mashitaka, ni nani katika Kamati hiyo ya Kombe anayeweza akadai kuwa na uelewa mpana na wa kina kunipita?

Tumepata ajali nyingi kama Taifa zilizosababisha majeraha na vifo vya wananchi na viongozi na hata kuzua maswali mengi kuhusu vyanzo vya ajali hizo bila Polisi kuingilia uhuru wa kusema wa majeruhi wala kuunda Kamati maalum za uchunguzi.

Lakini ajali yangu ambayo kwa ulinzi na baraka za Mwenyezi Mungu haijasababisha upotevu wa maisha, inajengewa kwa makusudi mazingira ya malumbano na kuundiwa Kamati maalum ya uchunguzi yenye lengo la kuziba watu midomo.

Hamasa hii ya Jeshi la Polisi kudodosa kila ninalolisema na kulitafutia maelezo mbadala, inatokana na nini, inachochewa na nini na kwa faida ya nani?
Kwa kuwa sheria za nchi zinataka vyombo vya kiutawala vya maamuzi (quasi-judicial bodies) vizingatie kanuni za haki za asili (principles of natural justice), ni nini kiliizuia Kamati hiyo maalum kunihoji mimi na dereva wangu ili kukidhi matakwa ya kanuni za haki za asili na kupata picha iliyo kamilifu zaidi ya ajali hiyo?

Man United wanajuuta kuwafahamu Barcelona

Kocha wa Barcelona akifurahia ushindi Mei 27 dhidi ya Man United. Ni msimu wake wa kwanza kwenye timu hiyo, ametwaa makombe matatu ukiwamo ubingwa wa Hispania na Klabu Bingwa Barani Ulaya.

Eto'o na Messi wamesababisha msiba Trafford

Eto'o akifunga bao la kwanza.

Classical goal from classical player. Messi akifanya vituuz kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la mashetani wekundu.
KOCHA wa Man United Fargerson amekiri kwamba Barca 'was not reachable' hivyo Mashetani hawakuweza hata kubeep.
Cristian Ronaldo kasema, Barcelona usipime, wapo juu na walistahili kushinda.
Kipa Van Deer Sar anasema, Barca si mchezo, ndiyo timu bora Ulaya.
Ushindi wa Barcelona huenda umefungua milango zaidi kwa Ronaldo kuondoka Old Trafford.
Nyota huyo wa Man U amesema hana uhakika kama atabaki kwenye timu hiyo.
Kwenye mtandao wapenzi wa Man wanasema CR7 asiondoke kwa kuwa Mashetani wekundu hawana uwezo wa kumsajili Messi a.k.a Maradona mpya na kwamba ni nyota huyo tu anayeweza kulinganishwa naye.
Jana niliwaeleza wapenzi wa United kwamba mpambano wa Rome ulionyesha tofauti ya kiwango cha Ronaldo na Messi wakasema KWELI.
Niliwauliza, kwa kuzingatia hilo, nani ni bora zaidi, wakasema Messi.
Kwa mtazamo wangu, ANDREAS INIESTA ni mchezaji BORA duniani kwa sasa.

Mwenge kuanza kukimbizwa leo Mwanza

MUDA mfupi ujao Makamu wa Rais Dk Ally Mohamed Shein atawasha Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa jirani wapo kwenye uwanja huo kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Mwenge huo utakimbizwa katika wilaya 138 kwa kuanzia na nane za Mwanza kuanzia leo hadi Juni tano.
Juni sita hadi 13 utakimbizwa katika wilaya nane za Kagera, kuanzia Juni 14 utakimbizwa mkoani Kigoma hadi Juni 17, na utakuwa Tabora kuanzia Juni 18 hadi 23.
Mwenge huo utazimwa Oktoba 14 mwaka huu katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.

Ajifungua akiwa na miaka 66

MWANAMKE nchini Uingereza amejifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 66.
Elizabeth Adeney alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji Jumanne mchana.
Alipata ujauzito kwa njia ya kupandikizwa(IVF), hali yake na mtoto nzuri.

Tuesday, May 26, 2009

Vimwana wakionyesha vituuuz vya Remtullah








MEI 23 mbunifu wa mavazi aliye juu hivi sasa nchini, Ally Remtullah alionyesha ni kwa nini kazi zake zinaheshimika hata nje ya Tanzania.
Wasichana kadhaa walipanda jukwaani jijini Dar es Salaam kuonyesha ubunifu wa kijana huyo anayeishi jijini humo.
Onyesho hilo lililopewa jina la Delectables fashion show lilikuwa baab kubwa, hongera kaka.
Nimewahi kuzungumza na kijana huyo akasema anatamani siku moja Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma, avae nguo aliyoibuni yeye.
Watu wengi maarufu nchini wanavaa nguo alizobuni kijana huyo.

Kwa wanaovuta sigara

SOMA hayo maneno chini ya hiyo sigara halafu jiulize kama ni muhimu kuendelea kuvuta sigara.
Ni ushauri tu, samahani kama nimekukwaza.

Red Bull marufuku Ujerumani

MAMLAKA za majimbo matano nchini Ujerumani zimepiga marufuku uuzwaji aa kinywaji cha RedBull kwa kuwa kina kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya cocaine.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hizi, idadi ya watu kwenye majimbo hayo ni sawa na nusu ya idadi ya watu nchini humo.
Miaka kadhaa iliyopita nchi za Ufaransa, Norway, na Denmark zilipiga marufuku matumizi ya kinywaji hicho kwa madai kuwa kina madhara kwa wanaokitumia ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo.
Ufaransa ililazimika kuruhusu tena matumizi ya Red Bull kwa kuwa sheria za Umoja wa Ulaya(EU) zinazuia kupiga marufuku matumizi ya chakula ama kinywaji kama haijathibitika kuwa vina madhara.
HATA HIVYO, taarifa za wataalamu wa SUMU zinawashauri wanawake wajawazito wasinywe Red Bull kwa madai kuwa kinywaji hicho kinaweza kusabanisha mimba itoke
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA) mpo?
Soma sehemu ya story kuhusu agizo hilo la kuzuia uuzwaji wa RedBull nchini Ujerumani.
– Regulators in the German states of Hesse and North-Rhine Westphalia banned the sale of Red Bull after finding traces of cocaine during tests, the Telegraph reports.

Levels of the chemical were not high enough to pose a health risk, but require the drink to be reclassified as a narcotic under German law.
A nationwide ban will likely follow.

The manufacturer of Red Bull has rejected the ban as baseless, claiming that “de-cocainized (sic) extract of coca leaf is used worldwide in foods as a natural flavoring,”
and pointed out that coca leaf extract is considered safe for use as an additive within the EU and the US.
Chanzo kingine kimeandika hivi:
RED Bull Cola has been taken off the shelves in Germany after inspectors found traces of COCAINE.
Coca leaf extracts in the drink tested positive for the Class A drug in routine food safety tests.

Officials said the cocaine levels were not a health risk — but the drug was banned in food.

Shops were told to stop selling the drink in five German states, which make up half the country’s population.

A nationwide ban was being considered yesterday.

But Red Bull insisted coca leaf was a safe flavouring and the drink should go back on sale.

Saturday, May 23, 2009

Ni kweli Ronaldo anahamia Madrid?


Lulu ya Man United, Christiano Ronaldo

Carlos Tevez naye mguu ndani, mguu nje
KUNA taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba mshambuliaji nyota wa Manchester United ya Uingereza, Christiano Ronaldo AMEAMUA kuhamia Real Madrid.
Kama taarifa hizi ni za kweli, litakuwa pigo KUBWA kwa mashetani wekundu kwa kuwa huenda Carlos Tevez hatakuwa kwenye kikosi cha Sir Alex Fugerson msimu ujao.
Soma hiyo taarifa hapo chini.
CRISTIANO RONALDO plans to quit Manchester United this summer for a £70million move to Real Madrid.
And in a double whammy for United, Manchester City are ready to battle Liverpool to capture Carlos Tevez.

Ronaldo has told friends and team-mates to forget stories he is staying at Old Trafford.

After a hat-trick of titles and two Champions League finals, he feels he has achieved what he wanted.

Now he is keen to revive Real's fortunes in a record-breaking switch to the Bernabeu.

A United source said: "He looks to have made up his mind again. He is not saying it publicly with such a big game coming up next week in the Champions League final.

"But in his mind that will be his last. The fact Real trailed Barcelona in La Liga this season only
makes the challenge more exciting for him."

Ronaldo made his feelings clear to those close to him as recently as last Saturday, when the champagne was still flowing after United's title-clinching home draw with Arsenal.

SunSport understands a number of senior players have been trying to talk round the Portuguese wizard but he is having none of it.

And manager Alex Ferguson, who won the same fight last summer, will now find it very difficult to keep the World Player of the Year.

Jay Dee awajibu wanaouliza atazaa lini

Lady Jay Dee akiwa nyumbani kwake
Nyumbani anayoishi nyota wa muziki wa kizazi kipya, Lady Jay Dee jijini Dar es Salaam.
MUDA mfupi uliopita niliperruz kwenye blog ya Judith Wambura, a.k.a Lady Jay Dee, a.k.a Binti Machozi, a.k.a Komando, a.k.a mama Some Food nikakuta waraka huu aliouandika kwa wanaomuuliza atazaa lini.
Nimeliweka jibu hili ili uone kawajibu nini, mimi simooo.
Kwanza email zenu nimezipata nashukuruni sana kwa maswali japo najua mnaouliza hili wote ni wenye nia mbaya
sio kweli kwamba mtafurahi saaana nikizaa najua kuna wengi mna wish hata nisipate mtoto kabisa ili mfurahi na kunisema zaidi...
Jibu la hili mnalo nyie, iwapo mtanifafanulia nini maana ya MGUMBA na TASA kama mnavoniita coz hata mimi sijui nitazaa lini mkishanijibu ndio nitajua kama nitazaa ama la.
Pili, hiivi mnapenda muziki wangu au mnapenda kuona watoto wangu pengine mngekuwa na msimamo na kipi mnachokipenda toka kwangu kama kweli mnasema Jide tunakuzimia
Ila uwe na watoto usiwe nao pumzi utavuta na ikifika siku ya aliekukopesha kuichukua atakunyang'nya na watoto kama hujawaandalia msingi mzuri utaacha wanateseka vile vile, yote maisha.
Sasa nijibuni, mnataka nizae lini na kwa nini?? maana mimi sio MUNGU kwa hiyo sina jibu la hilo swali lenu mnanionea bureee kama vipi ongeeni na SIR GOD...Atawajibu eti kwanini JIDE hazai ? je ni MGUMBA au TASA?

Najua mnaonipenda mko wengi na ndio maana mimi na nyinyi tuko juu sasa basi nisaidieni kuwaelimisha hao binamu zetu wengine wasipotee.
Mpende jirani yako kama nafsi yako
Love you always

Aksanteni, Mungu awabariki

TAREHE na mwezi kama leo miaka ileee, Caroline Msongo alijifungua mtoto wa kiume mjini Dodoma akapewa jina Basil a.k.a Msafiri.
Leo nina furaha sana, nawashukuru wote ambao kwa namna moja au nyingine wamenipongeza na kunitakia heri, Mungu awazidishie upendo.
Kwa kuwa leo ni birthday yangu, nimeona niweke picha hiyo juu nikiwa na mwanangu, Brian a.k.a Imeda.

Friday, May 22, 2009

Drogba akitoka kujinafasi



HIVI karibuni kamera za mapaparazi zilimnasa mshambuliaji wa matajiri wa London, Chelsea ya Uingereza, Didier Drogba akitoka kujirusha Club jijini London.
Ziangalie kwa makini hizo picha hasa ya 2, 3 na 5 kutoka juu, jibu utakalopata baki nalo.

Msiba CUF

MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi, Soud Yusuf Mgeni (CUF) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC) mwakilishi huyo alikuwa akisumbiliwa na mapafu.
Marehemu Yusuf Mgeni anatarajiwa kuzikwa kesho Pemba, Zanzibar.

Breaking News

MUDA mfupi uliopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuhukumu Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Temeke,Jamila Nzota kifungo cha miaka 11 baada ya kupatikana na hatia ya kula njama, kudai na kupokea rushwa.
Amekutwa na hatia katika makosa manne, hukumu itakwenda pamoja hivyo atakaa jela miaka mitatu.
Hakimu huyo amefanya kazi kwa takribani miaka 30, katia mchanga kitumbua chake kwa kuwa kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma, amepoteza haki zake zote.
Katika kosa la kwanza, mahakama imeridhishwa na ushahidi kwamba, Agosti mwaka 2007 hakimu huyo alikula njama za kudai rushwa.
Mahakama imeridhika pia kuwa, Agosti mwaka huo huo Hakimu huyo alipokea rushwa ya sh milioni moja kati ya sh milioni tano alizokuwa akidai.
Amepatikana na hatia ya kudai rushwa ya sh milioni nne zilizosalia.
Hakimu huyo pia amekutwa na hatia ya kupokea rushwa ya sh 700,000 Desemba 4 mwaka 2007 katika hoteli ya Slip Way jijini Dar es Salaam.
Fedha hizo ni sehemu ya rushwa ya sh milioni nne alizokuwa akizidai.
Nzota aliomba huruma ya mahakama kwa maelezo kuwa ana watoto sita na wajukuu wawili wanaomtegemea.

Dk Mwakyembe kalazwa Muhimbili

Dk Harrison Mwakyembe
Gari la Dk Mwakyembe baada ya ajali
KAMA itaonekana inafaa, Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe atapelekwa nje ya nchi kutibiwa.
Katibu wa Bunge, Dk Kashillilah jana likaririwa akisema kuwa wabunge wa haki ya kutibiwa nje ya nchi.
Dk Mwakyembe amelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili(MOI) jijini Dar es Salaam akipata tiba ya maumivu aliyopata alipopinduka na gari jana asubuhi.
Gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 362 ACH lilipinduka saa moja asubuhi wakati akija Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi, gari hilo lilipinduka wakati likilipita lori, mbele kulikuwa na shimo.
Kwa mujibu wa RPC Nyombi, baada ya gari hilo kuingia kwenye shimo tairi lilichomoka, likapoteza mwelekeo, likapinduka.

Wanachuo Ustawi ombeni msamaha

WANAFUNZI wa stashahada ya juu katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii waliofukuzwa wanatakiwa kuomba msamaha.
Wanafunzi hao wanatakiwa kuandika barua za kuiomba msamaha Serikali kama mamlaka hiyo ya nchi ilivyoagiza.
Mkuu wa Taasisi hiyo iliyopo Dar es Salaam, Profesa Rwegoshora ameagiza kwamba, barua hizo zifike kwake kabla ya tarehe 28 mwezi huu.
Watakaoomba msamaha watatakiwa pia kufika katika kikao cha kamati ya nidhamu kitakachoanza saa tatu asubuhi Juni 3 mwaka huu.
Wanafunzi hao walifukuzwa chuo kwa kuwa walikaidi amri iliyowataka waondoke mabwenini Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Thursday, May 21, 2009

Dk Mwakyembe apinduka na gari


MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa, alipinduka na gari leo saa moja asubuhi.

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Oscar Gabone ameshauri aletwe Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Dk Gabone amesema, Mbunge huyo amejigonga katika upande wa kushoto wa taya lakini hali yake si mbaya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi amekaririwa akisema kuwa, gari alilokuwa akisafiria Dk Mwakyembe lilipinduka saa 1.10 asubuhi katika mteremko wa Ihemi.
Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 362 ACH lilipinduka baada ya kulipita lori.

Kuna taarifa kwamba ofisi ya Bunge imetuma ndege binafsi ikamchukue kumleta Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Dereva wake hakuumia ila anasema anasikia maumivu ya kichwa.

Breaking News

MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe (CCM) ameumia katika ajali ya gari iliyotokea Iringa leo.
Inadaiwa kwamba, Mbunge huyo maarufu amevunjika taya, gari lake limeharibika sana.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Mwakyembe anasafirishwa kwa ndege kuletwa Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Dk Mwakyembe alijipatia umaarufu alipokuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa ya ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Richmond.
Ripoti ya kamati hiyo ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Edward Lowassa ajiuzulu hivyo Baraza la Mawaziri lilivunjwa.
Taarifa zaidi baadaye.

Mwanaume mwenye uke bandia aaga dunia

MKAZI wa Dar es Salaam aliyefanyiwa operesheni kuwekewa uke wa bandia amefariki dunia.
Abdallah Aluu, anayefahamika kwa jina la Victoria aliaga dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo jijini humo.
Victoria alifikishwa Muhimbili Jumatatu mchana, akalazwa katika wodi ya wanawake, na iligundulika kwamba alikunywa sumu kwa lengo la kujiua.
Kabla ya kupelekwa Muhimbili alilazwa kwenye wodi ya wanawake katika Hospitali ya Mwananyamala kuanzia Jumapili alifajiri akiwa hajitambui.
Alikuwa akiishi mtaa wa Kipongoso, Mbezi Beach jijini humo. Habari zimebainisha kwamba, aliacha ujumbe kwamba ameamua kujiua baada ya kuzidiwa na mapenzi!
Inadaiwa kuwa miaka kadhaa iliyopita aliuza nyumba ili kufanyiwa operesheni ya kukatwa uume na kuwekewa uke wa bandia na alikuwanao hadi alipoaga dunia jana.

Michael Jackson kufanyiwa operesheni


MFALME wa muziki wa POP, Michael Jackson (50) anajiandaa kufanyiwa operesheni ya kuondoa sehemu ya ngozi yake ili kupambana na kansa ya ngozi.


Hivi karibuni madaktari walibainisha kwamba nyota huyo ana kansa ya ngozi.


Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, sehemu ya ngozi ya kifuani na puani itaondolewa na atahitaji mapumziko ya miezi kadhaa.


Mwanamuziki huyo alikuwa anajiandaa kufanya ziara ya 'kufa mtu' London Julai mwaka huu lakini imefahamika kuwa hataweza, na ataifanya Machi mwakani.

Wednesday, May 20, 2009

'Kutembea' na mume wa mtu(2)

IRRESPECTIVE of the fact that today’s women are liberated, many still continue to perceive the married man as having a certain type of security.

Cynical as it may sound, such women tend to think that married men will cater for their emotional needs better than any single man out there.

On the other hand, some women perceive having an affair with a married man as some sort of triumph over the wife.

Although this signifies a lack of self-respect and self-worth, such women get a feeling of
accomplishment and triumph over the legitimate woman.

This perception could not be further from the truth as it is obvious that the married man (trophy) is already taken.

Unfortunately, such women get a non-existent feeling that they are extra special and better than the man’s legal wife.

This again clearly shows that such women are only living in a fantasy world.

Additionally, some women go after the married man because they are dying to get what the legitimate woman has.

In most cases, women do this maliciously to try and get back at the married man’s wife for reasons better known to them.

Cannavaro kaihama Real Madrid


MLINZI king'ang'anizi, Fabio Cannavaro (35) ameihama Real Madrid ya Hispania, anarudi kwenye timu yake ya zamani, Juventus ya Turin, Italia.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Italia amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Juve.
Mwaka 2006 Cannaro aliihama Juve akaenda Madrid.

Nao walikuwepo

Wake wa Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli(kushoto) na Thobeka Mabhija wakishuhudia mume wao akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini

Rais Zuma na mkewe wa kwanza, Sizakele Khumalo

Mzee Nelson Mandela na mkewe, Graca.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na mkewe, Grace wakati wa sherehe za kuapishwa Zuma jijini Pretoria.

Rais Zuma akimshukuru mzee Mandela kwa support aliyompa.

Pacha wenye baba tofauti

Mama mzazi wa pacha wenye baba tofauti,Mia Washington akiwa mmoja wa watoto hao, Jordan

Mia akiwa na Justin

MAMA mzazi wa pacha hao, Mia Washington anajuuuta kumsaliti mchumba wake na anashangaa kwa nini 'maajabu' hayo yamemtokea yeye.
Mia ana mchumba, na aliamini kwamba ujauzito ulikuwa wa 'honey' wake lakini pia anakiri kwamba alikuwa anamsaliti kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.
Alijifungua pacha wawili, Jordan na Justin miezi 11 iliyopita, walipishana dk saba kuzaliwa, mwenzi wake aliamini wote ni wanawe.
Kadri siku zilivyokwenda watoto hao walianza kuonekana kuwa tofauti, wakapimwa DNA, duh, kumbe wana baba tofauti.
Mchumba wa mama huyo amemsamehe na anawalea watoto hao.

Monday, May 18, 2009

Mwanaume Dar ana uke wa bandia

MWANAUME jijini Dar es Salaam amelazwa hospitali akiwa na jinsia ya kike.
Amelazwa katika wodi ya wanawake katika hospitali ya Mwananyamala jijini humo.
Polisi walimfikisha hospitalini hapo jana saa 11 alfajiri.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Suleiman Mtani amekaririwa akisema kuwa, mgonjwa huyo jana alikuwa hajitambui.
Inadaiwa kuwa, mtu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30 ni shoga, aliokotwa katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Mbezi Beach akiwa hajitambui.
Kuna madai pia kuwa, anaishi Kawe, aliuza nyumba ili apate fedha za kumwezesha kuondoa uume wake na kuwekewa uke nchini Thailand.
Habari kutoka hospitalini hapo zimebainisha kwamba, mgonjwa huyo amekatwa uume, amewekewa uke uliobainika kuwa na kina kifupi kuliko wa mwanamke wa kawaida.
Mgonjwa huyo ametajwa kwa jina moja la Victoria.

'Kutembea' na mume wa mtu (1)

WAKATI naperuuz nimekutana na hii kitu, isome inaweza kukusaidia kufahamu ni kwa nini inaonekana ni kawaida kwa wanawake kupenda 'kutembea' na waume za watu, na vijana 'wanajirusha' na mijimama.

Temptation of the forbidden - Some people perceive married couples as the forbidden temptation since they are already committed and hence unavailable.

Interestingly, there’s an excitement that stems from the fact that such people are already taken, and attracting them gives the “hunter” a sense of power and accomplishment.

Furthermore, the challenge and the risk involved in conquering the prey makes the entire game even more exciting.
It is no secret that most single women have an obsession for married men owing to the human trait of wanting what one cannot have.

On the other hand, some hunters go for one’s confidence, experience in intimate matters and authority.

And even though it’s utterly unjustifiable and shameless, some people find a sense of accomplishment in bedding someone else’s man or woman.

This has a lot to do with the satisfaction that comes with breaking rules and doing things the wrong way without being caught.
In other words, some people seek their sexual highs through cheating because
of the excitement that comes with getting away with something taboo.

Tuzo za CNN waandishi Tanzania mmh

FINALISTS in the prestigious CNN MultiChoice African Journalist 2009 Competition were announced by Azubuike Ishiekwene, Chair of the independent judging panel.
The competition is now in its 14th year.

This year the competition received entries from 836 journalists from 38 countries throughout the continent, including French and Portuguese speaking Africa.

There are 25 finalists from 12 countries:

• Ayodeji Adeyemi, TELL Magazine, Nigeria•
Biaou Daniel Valérien Adje, ORTB - Parakou, Benin•
Anas Aremeyaw Anas, The Crusading Guide, Ghana•
Rajen Bablee, Samedi Plus, Mauritius•
Ernesto Bartolomeu, TPA, Angola•
Nicola De Chaud, Backyard Productions for Carte Blanche, South Africa•
Ethar El-Katatney, Business Today Egypt •
Hazel Friedman, Special Assignment, SABC, South Africa•
Halden Krog, The Times, South Africa• Anna-Maria Lombard, Health-e News Service for 3rd Degree e.tv, South Africa•
Paul McNally, Men's Health Magazine, South Africa •
James Moturi Mogaka, KTN, Kenya•
Fredrick Mugira, Freelance for Mail & Guardian online www.mg.co.za, Uganda•
Sammy Muraya, Metro FM, Kenya•
Boniface Mwangi, Expression Today, Kenya•
John Benson Mwangi, KTN, Kenya• John-Allan Namu, KTN, Kenya•
Elshadai Negash, Freelance for Fortune Newspaper, Ethiopia •
Luís Nhachote, Zambeze, Mozambique •
Tolu Ogunlesi, Contributing Editor for Glide Magazine, Nigeria•
Violet Otindo, K24 Television, Kenya •
Odette Schwegler, Backyard Productions for Carte Blanche, South Africa•
Viviane Tiendrébéogo, Radiodiffusion Télévision du Burkina Faso•
Beauregard Tromp, The Star, South Africa•
Alain Zongo, L'Observateur Paalga, Burkina Faso

Ancelotti akubali kubeba mikoba Chelsea


Carlo Ancelotti

KOCHA wa AC Milan ya Italia , Carlo Ancelotti amethibitisha kwamba yeye ni kocha mtarajiwa matajiri wa London, Chelsea.

Taarifa rasmi kuhusu kocha huyo zinatarajiwa kuwekwa bayana wikii hii.

Kocha huyo wa AC Milan ya Italia tayari amemweleza mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuhusu uamuzi wa kubeba mikoba aliyobebwa na Guus Hiddink.


Marco Van Basten huenda atamrithi Ancelotti AC Milan.


Soma habari hiyo kwa kirefu hapo chini

CARLO ANCELOTTI has confirmed he will take over at Chelsea this summer.

An official announcement will be made as soon as AC Milan decide on his successor — likely to be this week.

SunSport understands Ancelotti told Roman Abramovich of his decision yesterday morning.
It followed Milan’s 2-1 defeat by Udinese on Saturday evening that confirmed Jose Mourinho’s Inter as champions.

Ancelotti met with club directors, including vice-president Adriano Galliani, after the Udinese
defeat.

It was agreed Ancelotti’s eight-year reign at the San Siro was over and he was told he could leave for Stamford Bridge with Milan’s blessing.

Former Holland and Milan striker Marco Van Basten, who recently quit as Ajax boss, is in talks to take over from Ancelotti.

SunSport revealed on February 10 that Ancelotti, 49, was the man Blues owner Abramovich wanted to replace Phil Scolari.

We also reported that Guus Hiddink’s appointment was never anything other than in a caretaker role.

A four-year contract worth £22million was agreed a month ago and will be signed after Ancelotti
undergoes a medical.

He has already identified a major summer signing in Aston Villa star Ashley Young — as we revealed last week.

Ancelotti made up his mind to take the Blues job after Milan president Silvio Berlusconi blamed him for failing to land the title.

Saturday, May 16, 2009

Michael Jackson ana kansa ya ngozi




MFALME wa muziki wa Pop, Michael Jackson(50) ana kansa ya ngozi.
Uchunguzi wa madaktari umebainisha kuwa, sehemu za mwili wake zina tatizo hilo na pia kuna seli za saratani usoni hivyo huenda pia kutaathirika.
Kwa mujibu wa madaktari, saratani hiyo inatibika.

Soma taarifa hiyo kwa kirefu hapo chini

Pop superstar Michael Jackson has been diagnosed with skin cancer.

The King of Pop was diagnosed with the disease in recent weeks after doctors spotted signs of cancerous cells on his neck and pre-cancerous cells on his face, a British tabloid claimed.

However, the fans of the superstar can take heart in the fact that the disease is treatable.

"Michael's test showed spots of skin cancer on his body, and cell which could turn to skin cancer on his face.
He was at first very concerned, but says he has been assured by the doctors that they can treat this and he will recover," a source told ‘The Sun’.

The 'Thriller' hitmaker is determined to recover soon as he wants to make a successful comeback with his 50 date concert series at London's famed O2 Arena this July.

"Michael is really looking forward to his concerts and is determined to wow his fans at each and every gig. He said he's insisted that any treatment must fit around the concerts, and the show will go on," the source added.

The 'Heal the World' singer has been making regular visits to a dermatologist in Beverly Hills, and last month he showed up at Cedars-Sinai Medical Center in Los Angeles, which, according to the newspaper, has a specialist lab to test for skin cancer.

The singer was earlier dogged with bad health reports which claimed that Jackson suffered from a series of skin conditions and was diagnosed with vitiligo over 20 years ago.

The disease affects skin pigmentation and is responsible for the singer's pale look, the report said.

The popstar, who has been nicknamed 'Whacko-Jacko', is controversy's favourite child, be it dangling his son from a hotel balcony, numerous plastic surgeries, child molestation accusations or his multiple marriages.

DStv bei juu

MultiChoice would like to advise all DStv and analogue customers that from 1 April 2009, the monthly DStv and analogue subscription rate will increase.

The following increases apply for the various bouquets:

DStv Premium subscription from R468.99 to R499.00 (a 6% increase)

DStv Compact R199.00 to R219.99 (10 % increase)

PVR access fee R 55.00 to R60.00

DStv Indian North (stand-alone) from R227.75 to R237.00. DStv Indian North (add-on) from R 143.63 to R 152.80

DStv Portuguesa (stand-alone) from R222.75 to R237.00 (6.4% increase) DStv Portuguesa (add-on) from R143.63 to R152.80

DStv Indian South (stand-alone) from R168.91 to R179.70

DStv Indian South (add-on) from R108.61 to R115.60

Analogue from R254.06 to R269.00 (5.8%)

DStv Select increases from R139.00 to R148.00 (as of 1 May 2009)

There will be no increase to the various Decoder Care Contract (DCC) fees or to the reconnection fees.

The annual price increase is to accommodate the rise in operating costs of the company.

Pombe marufuku Mpanda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe, Tunu.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku wakazi wa Mpanda wasinywe pombe Jumatatu hadi Ijumaa.


Waziri Mkuu amewaruhusu wanywe Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.


Alitoa agizo hilo wakati akihutubia wakazi wa kata ya Kibaoni wilayani Mpanda mashariki.


Waziri Mkuu amezaliwa katika kijiji kilichopo katika kata hiyo.

Friday, May 15, 2009

ATCL wapata bosi mpya


AIR TANZANIA COMPANY LIMITED



STAFF NOTICE

STAFF NOTICE NO. 02 TO: ALL STAFF



ACTING APPOINTMENT

On 23rd February 2009, I was appointed to the NIC restructuring task force by His Excellency the President of the United Republic of Tanzania.



The Minister for Finance and Economic Affairs has also appointed me to the Board of Directors of NIC effective from 23rd April, 2009.



I have been informed that the appointment to the task force will be a full time job for six months effective from 1st May, 2009


In view of the above, the ATCL Board of Directors has appointed Mr. William Haji to act in the position of Managing Director and CEO with effect from 8th May 2009 for a period of six months or as it would be appropriate.



While at the same time Mr William Haji will remain as substantive Director of Finance


You are asked to give him the necessary cooperation to enable him accomplish his responsibilities.


I wish ATCL all the best .

David E. Mattaka


MANAGING DIRECTOR & CEO

ISSUED BY: MANAGING DIRECTORS OFFICE
DATE: 11TH MAY, 2009