MUDA mfupi uliopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuhukumu Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Temeke,Jamila Nzota kifungo cha miaka 11 baada ya kupatikana na hatia ya kula njama, kudai na kupokea rushwa.
Amekutwa na hatia katika makosa manne, hukumu itakwenda pamoja hivyo atakaa jela miaka mitatu.
Hakimu huyo amefanya kazi kwa takribani miaka 30, katia mchanga kitumbua chake kwa kuwa kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma, amepoteza haki zake zote.
Katika kosa la kwanza, mahakama imeridhishwa na ushahidi kwamba, Agosti mwaka 2007 hakimu huyo alikula njama za kudai rushwa.
Mahakama imeridhika pia kuwa, Agosti mwaka huo huo Hakimu huyo alipokea rushwa ya sh milioni moja kati ya sh milioni tano alizokuwa akidai.
Amepatikana na hatia ya kudai rushwa ya sh milioni nne zilizosalia.
Hakimu huyo pia amekutwa na hatia ya kupokea rushwa ya sh 700,000 Desemba 4 mwaka 2007 katika hoteli ya Slip Way jijini Dar es Salaam.
Fedha hizo ni sehemu ya rushwa ya sh milioni nne alizokuwa akizidai.
Nzota aliomba huruma ya mahakama kwa maelezo kuwa ana watoto sita na wajukuu wawili wanaomtegemea.
No comments:
Post a Comment