Monday, May 18, 2009

Mwanaume Dar ana uke wa bandia

MWANAUME jijini Dar es Salaam amelazwa hospitali akiwa na jinsia ya kike.
Amelazwa katika wodi ya wanawake katika hospitali ya Mwananyamala jijini humo.
Polisi walimfikisha hospitalini hapo jana saa 11 alfajiri.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Suleiman Mtani amekaririwa akisema kuwa, mgonjwa huyo jana alikuwa hajitambui.
Inadaiwa kuwa, mtu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30 ni shoga, aliokotwa katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Mbezi Beach akiwa hajitambui.
Kuna madai pia kuwa, anaishi Kawe, aliuza nyumba ili apate fedha za kumwezesha kuondoa uume wake na kuwekewa uke nchini Thailand.
Habari kutoka hospitalini hapo zimebainisha kwamba, mgonjwa huyo amekatwa uume, amewekewa uke uliobainika kuwa na kina kifupi kuliko wa mwanamke wa kawaida.
Mgonjwa huyo ametajwa kwa jina moja la Victoria.

1 comment:

  1. Angebahatika kuwa mwanamke si ajabu angetamani kuwa mwanaume.
    Ah, masumbufu ya dunia na kushindwa kumiliki tamaa za mwili kisawasawa.
    Pole kwake.

    ReplyDelete