Saturday, May 23, 2009

Jay Dee awajibu wanaouliza atazaa lini

Lady Jay Dee akiwa nyumbani kwake
Nyumbani anayoishi nyota wa muziki wa kizazi kipya, Lady Jay Dee jijini Dar es Salaam.
MUDA mfupi uliopita niliperruz kwenye blog ya Judith Wambura, a.k.a Lady Jay Dee, a.k.a Binti Machozi, a.k.a Komando, a.k.a mama Some Food nikakuta waraka huu aliouandika kwa wanaomuuliza atazaa lini.
Nimeliweka jibu hili ili uone kawajibu nini, mimi simooo.
Kwanza email zenu nimezipata nashukuruni sana kwa maswali japo najua mnaouliza hili wote ni wenye nia mbaya
sio kweli kwamba mtafurahi saaana nikizaa najua kuna wengi mna wish hata nisipate mtoto kabisa ili mfurahi na kunisema zaidi...
Jibu la hili mnalo nyie, iwapo mtanifafanulia nini maana ya MGUMBA na TASA kama mnavoniita coz hata mimi sijui nitazaa lini mkishanijibu ndio nitajua kama nitazaa ama la.
Pili, hiivi mnapenda muziki wangu au mnapenda kuona watoto wangu pengine mngekuwa na msimamo na kipi mnachokipenda toka kwangu kama kweli mnasema Jide tunakuzimia
Ila uwe na watoto usiwe nao pumzi utavuta na ikifika siku ya aliekukopesha kuichukua atakunyang'nya na watoto kama hujawaandalia msingi mzuri utaacha wanateseka vile vile, yote maisha.
Sasa nijibuni, mnataka nizae lini na kwa nini?? maana mimi sio MUNGU kwa hiyo sina jibu la hilo swali lenu mnanionea bureee kama vipi ongeeni na SIR GOD...Atawajibu eti kwanini JIDE hazai ? je ni MGUMBA au TASA?

Najua mnaonipenda mko wengi na ndio maana mimi na nyinyi tuko juu sasa basi nisaidieni kuwaelimisha hao binamu zetu wengine wasipotee.
Mpende jirani yako kama nafsi yako
Love you always

2 comments:

  1. Big-up sana Jay Dee, umejibu vema!!!!!! coz walimwengu huwa hawakosi neno!!!! mie nakukubali wewe pamoja na vyote ulivonavyo

    ReplyDelete
  2. Jamaniiii, ama kweli watu wengi lkn binaadamu wachache!!! wapotezee hao, hawana jipya dadangu, labda wanataka urithi........, wachawi tu hao.

    ReplyDelete