Thursday, April 30, 2009

Cheyo Mbunge Bunge la Afrika




Bunge la Tanzania limemchagua Mbunge wa Bariadi(UDP), John Momose Cheyo kuwa Mbunge katika Bunge la Afrika.

Cheyo kachaguliwa muda mfupi uliopita katika mkutano wa 15 wa Bunge utaomalizika muda mfupi ujao mjini Dodoma.

Wabunge 205 walipiga kura, mbili ziliharibika, Cheyo amepata kura 111, mpinzani wake, Khalifa Suleiman Khalifa amepata kura 92.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda yupo anahutubia Bunge kuhitimisha mkutano huo.

Wabunge walikutana kwa siku 10, waliuliza maswali 108, Pinda aliulizwa maswali 18 ya papo hapo.

JK kuongoza mkutano kujadili mabomu

RAIS Jakaya Kikwete mchana huu ataongoza mkutano wa viongozi wa Serikali kujadili na kutathimi milipuko ya mabomu katika ghala la kuhifadhia silaha mkoani Dar es salaam.
Mabomu hayo yalilipuka jana katika ghala hilo la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) lililopo Mbagala wilayani Temeke.
Muda mfupi uliopita Waziri mkuu, Mizengo Pinda amesema bungeni kwamba, baada ya mkutano huo Serikali itatoa tamko kuhusu milipuko hiyo iliyosabisha hasara ya mali, vilema, majeraha, na vifo.

Mabomu Dar yameua watano


HADI sasa milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mbagala mkoani Dar es Salaam imeua watu watano.


Mkuu wa Mkoa huo, William Lukuvi ameitaja idadi hiyo leo asubuhi wakati akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Channel Ten cha jijini humo.


Kwa mujibu wa Lukuvi, chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika na kwamba, uchunguzi utafanywa baada ya kwisha kwa moto katika ghala la silaha kambini hapo.


Mabomu yaliyokuwa yamehifadhiwa ghalani hapo yalilipuka jana kwa nyakati tofauti na kusababisha mitikisiko, moshi, nyumba zimebomoka, zimepata nyufa, na kuna nyingine zimeungua.


Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa, watu wengi wakiwamo watoto wamepotea na pia kulikuwa na uporaji na wizi kwenye makazi ya watu.

Wednesday, April 29, 2009

Mabomu yaua Dar es Salaam


WATU wawili wamekufa, zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa baada ya mabomu kukipuka katika kambi ya Jeshi Mbagala, wilayani Temeke.



Taarifa za habari za vyombo vya habari zimetangaza idadi hiyo ya waliokufa wakiwamo watoto.



Huenda idadi ya vifo itaongezeka kwa kuwa hali za baadhi ya majeruhi ni mbaya hivyo imebidi walazwe Katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.




Majeruhi wengi wamelazwa katika hospitali ya Temeke

Mbagala hatari

HALI ya usalama Mbagala bado si shwari, watu wengi wameumia na wengine wamezimia kwa hofu.
Taarifa kutoka kwenye kambi yalipolipuka mabomu hayo zimedai kuwa huenda itatokea milipuko mikubwa kuliko iliyotokea hadi sasa kwa kuwa kuna mabomu makubwa hayalipuka.
Hadi sasa Mbagala ni vurugu tupu, wengi wamezimia kwa mshtuko, wengi wamepotea wakiwamo watoto, na kuna nyumba zimeungua.
Kuna taarifa zinazodai kuwa watu kadhaa wamekufa, polisi hawajathibitisha.
Baadhi ya mabomu yamelipuka kwenye makazi ya watu, moshi umetanda Mbagala na kwa ujumla shughuli za kijamii zimeathirika sana.
Milipuko ilisikika hadi katikati ya jiji la Dar es Salaa, na kuna taarifa zinazodai kwamba mashine za ATM kwenye mabenki hazifanyi kazi.
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imewataka wananch wasiende Mbagala kwa kuwa eneo hilo ni hatari kwa sasa, na waliopo huko wasikae kwenye makundi.
Wananchi pia wametakiwa kuzima simu za mkononi kwa kuwa zinavutia mabomu.
Kuna taarifa kwamba, wananchi wameamriwa kutokaa kwenye maghorofa marefu hivyo huenda wafanyakazi wengi leo wamewahi kurudi makwao.

Breaking News

KAMANDA wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amewataka wananchi wasiende Mbagala kwa kuwa eneo hilo ni hatari kwa sasa.
Kamanda huyo pia kawataka wananchi walioko huko wasikuanyike, na wazime simu zao za mkononi.
Kova amesema, mabomu mengi yamelipuka katika kambi ya jeshi iliyopo Mbagala Kizuiani na hajui chanzo cha ajali hiyo.
Taarifa kutoka eneo la tukio zimebainisha kwamba, moshi umetanda eneo hilo , kuna giza, na pia nyumba kadhaa zinaungua.
Milipuko mikubwa ilisikika saa kadhaa zilizopita, na kuna majengo katikati ya jiji la Dar es Salaam yameathirika.

Milipuko Dar es Salaam

KUNA sauti kubwa za milipuko zinazodaiwa kusababishwa na kulipuka mabomu katika kambi ya jeshi iliyopo Mbagala, Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa ghala la kuhifadhia silaha katika kambi hiyo limelipuka.
Nimezungumza na mkazi wa huko amesema wananchi wamezikimbia nyumba zao, wapo barabarani hawafahamu cha kufanya na wengine wanalia.
Mwanzo kulikuwa na taarifa kwamba ni mazoezi ya jeshi lakini baadaye zilipatikana taarifa kuwa si mazoezi, ni ajali katika kambi hiyo, mabomu yanalipuka.
Inadaiwa kuwa kuna nyumba zimeanguka na huenda kutakuwa na maafa.
Vishindo vya milipuko hiyo vinasikika hadi katikati ya jiji la Dar es Saaam.

Wizara yaomba wanaume wafanyiwe tohara

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema wanaume ambao hawajatahiriwa watumie busara, wafanyiwe tohara ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Aisha Kigoda ametoa ombi hilo muda mfupi uliopita bungeni mjini Dodoma.
Matokeo ya tafiti za kisayansi yamebainisha kwamba uwezekano wa mwanaume aliyetahiriwa kuambukizwa Virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini (VVU) ni mdogo kulinganisha na ambao hawajafanyiwa tendo hilo.

"press Conference" ya First Lady




NI nadra kuona au kusikia Mke wa Rais akiandaa mkutano rasmi ajibu maswali kuhusu maisha yake Ikulu.

Hivi karibuni Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama, alifanya hivyo, alijibu maswali kumhusu yeye na hususani maisha yake White House.

Msiba Kanisa Katoliki Shinyanga

PADRE Jacob Makula wa kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga amekufa.
Padre huyo aliaga dunia juzi saa nne usiku baada ya kupata ajali ya pikipiki wakati akienda kwenye makazi yake.
Alikuwa akiiendesha, akashindwa kuimudu, akaanguka na kufa papo hapo.
Atazikwa Ijumaa katika makaburi ya Kanisa hilo jimboni humo.

Monday, April 27, 2009

Ni Arsenal na Man United Jumatano

Mashine za Arsenal. Arshavin na Fabregas



Cesc Fabregas akishangilia bao alilofunga jana, alicheka na nyavu mara mbili





Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger

KOCHA wa Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger amesema The Gunners wana uwezo wa kuifunga timu yoyote duniani.


Wenger amesema, haidharau Man United lakini anakwenda Old Trafford kushinda.


Kocha huyo Mfaransa amesema, ingawa Mashetani wekundu wana uzoefu, pasi za vijana wake si mchezo hivyo wanakwenda kutafuta goli na kushinda.

Vinara hao wa soka Uingereza watapambana Jumatano katika kipute cha nusu fainali ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Jana Arsenal waliinyuka Middlesbrough mabao 2 kwa bila, Juzi Man U iliishinda Totenham Hotspurs 5 kwa 2.
Sindano mpya ya The Gunners, Andre Arshavin haitacheza game la keshokutwa.

Mastaa wanapokutana

Oprah na Mchungaji Jesse Jackson

Oprah na Jesse Jackson

Oprah na mwanamuziki/mcheza sinema Jennifer Hudson

Oprah na mcheza sinema Denzel Washington

Oprah na Jennifer wakijiachia

Oprah na Jennifer

Oprah na Denzel Washington

Samaki 'wa magufuli' hasara


GHARAMA za kuhifadhi zaidi ya tani 290 za samaki waliokamatwa katika meli ya uvuvi, MV Tawariq1, kwenye bahari ya Hindi eneo la Tanzania zimefika zaidi ya sh bilioni moja.

Samaki hao waitwao Jodari wana thamani ya sh bilioni mbili na hadi sasa haijulikani watauzwa lini.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Jonas Melewasi amesema, kwa kuwa mahakama iliagiza samaki hao wauzwe kwa mnada, mchakato wa kuwapata watakaosimamia uuzwaji huo unaendelea.

Alikiri kuwa kuchelewa kuwauza samaki hao kunaongeza gharama za kuwahifadhi samaki hao katika kampuni ya Bahari Foods Limited ya Dar es Salaam.

Hadi sasa haifahamiki samaki hao wapo chini ya Wizara au polisi, kwa kuwa Ijumaa iliyopita , Msemaji Mkuu wa Wizara hiyo, Judith Mhina, alisema, wapo chini ya polisi na wanaisubiri mamlaka hiyo itangaze mnada ndipo wao (Wizara) watakachukua jukumu la kusimamia uuzwaji.

Mhina alisema, kwa kuwa wapo chini ya uangalizi wa polisi ni jukumu la mamlaka hiyo kusema mnada utafanyika lini na wapi, na kwamba Wizara itasimamia mnada huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Upepelezi Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo amesema si kweli kuwa samaki hao wapo chini ya Polisi, wapo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Aprili saba mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ilikubali ombi la upande wa mashitaka la kutaka samaki hao wauzwe kwa mnada na fedha zitakazopatikana ziwekwe kwenye mfuko maalumu wa serikali kama kielelezo mahakamani.

Ni huduma au biashara?

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili inatoza sh 20,000 kila siku kuhifadhi maiti katika chumba cha maiti hospitalini hapo, sh 30,000 kuweka dawa kwenye mwili wa marehemu Mtanzania, sh 200,000 kufanya uchunguzi wa mwili wa raia wa Tanzania na sh 25,000 kuosha na kuuvisha mwili.

Maiti ambao si raia wa Tanzania wanalipiwa sh 60,000 ili kuwekewa dawa, na sh 400,000 kufanyiwa uchunguzi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Muhimbili, Aminiel Algaesha amesema, viwango hivyo si vikubwa, na vinalingana na ubora wa huduma hizo katika chumba za kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

“Hizi ndiyo gharama zetu tulizoweka ili kukidhi mahitaji” alisema Algaesha na kubainisha kwamba, uongozi wa hospitali umeweka gharama hizo ili wafiwa wasiache maiti zikae muda mrefu Muhimbili.

Kwa mujibu wa Algaesha, wafiwa wanatozwa fedha hizo ili pia kufidia gharama za uendeshaji kwa kuwa chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili kina majokofu ya kisasa yanayotumia umeme mwingi.

Alisema Muhimbili haiwakomoi watu na kusema gharama za kuhifadhi maiti na huduma nyingine kwa marehemu Muhimbili ni ‘standard’ hasa ikizingatiwa kuwa ni hospitali ya rufaa.

Mtu akifariki dunia Muhimbili na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo, kuanzia siku ya tatu wafiwa watatozwa sh 20,000 kila siku utakazohifadhiwa, na endapo maiti itatoka nje ya hospitali hiyo kwenda kuhifadhiwa hapo wafiwa watatozwa kiasi hicho kuanzia siku mwili utakapofikishwa.

Saturday, April 25, 2009

Wapenzi jukwaani


Rihanna na Chriss Brown 'wakikamua'




















BILA shaka hizo picha zitakuburudisha week end hii. Ni Chriss Brown na mpenzi wake, Rihanna wakifanya mavituuz jukwaani.
Uhusiano wao umekuwa na misuko suko lakini hawaachani.

Man U kumng'oa Kaka Milan?






KUNA taarifa kwamba huenda Manchester United itamsajili kiungo mshambuliaji wa AC Milan ya Italia, Ricardo Kaka.

Ni habari njema kwa mashabiki wa Man U lakini huenda itakuwa shubiri kwao endapo klabu hiyo ya Uingereza italazimika kumuuza Christian Ronaldo Real Madrid.

Kuna taarifa pia kwamba, Si Alex Furgerson anamtaka KAKA azibe nafasi ya Ronaldo endapo dogo huyo atakwenda Madrid, lakini pia timu hiyo ya Hispania inaitaka lulu hiyo a Milan.

Soma hapo chini ujue kinachoendelea

MANCHESTER UNITED held talks with Kaka yesterday (Ijumaa) over a sensational summer move.
The Brazilian’s representatives met United to discuss personal terms which would total £35million in wages alone.

A source close to the AC Milan superstar confirmed: “It was a very positive meeting, although
nothing was agreed.


“The player wants a five-year contract and wages of £135,000 a week. He is very keen to join United and these are figures that are within United’s pay structure. It’s up to them what happens now.”


The talks did not involve any discussion about a transfer fee but Milan expect to get at least £70m for their star player.


The big question now is how United will find the cash — and whether they will sell Cristiano
Ronaldo in the summer to Real Madrid.


Kaka, 27, has already spoken of his affinity for United, saying: “They have some great players in
Giggs and Scholes and especially Wayne Rooney.


“One of my best friends, Anderson, is also there — how can anyone say no?
“They are the English and European champions and a great club to play for.”

Zuma ni raha tu

Jacob Zuma akiserebuka na wafuasi wake kufurahia ushindi

Wafuasi wa Zuma duh


Zuma akiwa na wafuasi wake wakisherekea ushindi wa ANC

Zuma akiwa katika vazi la kizulu




Zuma akipiga kura Jumatano wiki hii




Mzee Nelson Mandela baada ya kupiga kura Jumatano wiki hii.

CHAMA cha ANC kimeshinda uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini hivyo ni dhahiri kwamba, Jacob Zuma(67) ndiye Rais mtarajiwa wa nchi hiyo.

Kifo cha DECI

Najua mliipenda DECI, Serikali imeipenda zaidi, bwana alitoa, Serikali imetwaa, uamuzi wa Serikali uheshimiwe, Amen.

Friday, April 24, 2009

Buriani Phares Kabuye


Basi la R.S Investment baada ya kupinduka leo asubuhi

ALIYEKUWA Mbunge wa Biharamulo Magharibi mkoani Kagera, Phares Kabuye (TLP) amekufa kwenye ajali ya gari leo mkoani Morogoro.

Kabuye alikuwa akisafiri kwa basi la Rs Investiment lenye namba za usajili T 934 ADA akitoka Kagera kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa TLP unaofanyika Jumapili jijini humo.

Kbuye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na alijaza fomu kutetea nafasi yake.


Basi hilo aina Scania lilipinduka baada ya dereva kushindwa kulimudu, likapoteza mwelekeo likiwa kwenye mwendo mkali.


Inadaiwa kuwa wakati ajali hiyo inatokea basi hilo lilikuwa likiendeshwa na kondakta.



Kabuye alipata ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2005, Oktoba 12 mwaka 2007 Mahakama Kuu Tanzania ilitengua matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo kwa maelezo kuwa alimkashifu mgombea wa CCM, Anatoly Choya.

Katika miaka ya 1990 Kabuye alikuwa Mbunge wa CCM, na amewahi pia kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki.

Kabuye alikuwa na mvuto wa aina yake anaposimama kuzungumza bungeni kutokana na lafudhi yake, na hoja zake.

Bunge la Tanzania limekuwa likipoteza wabunge wanaokufa katika ajali, miezi kadhaa iliyopita, Salome Mbatia na Chacha Wangwe walikufa katika ajali za magari.

Mke wa Ashley Cole yupo juu

Mlinzi wa Chelsea na Timu taifa ya Uingereza, Ashley Cole






Britney Spears



Cheryl na mwenzake walipowasili Uingereza wakitoka Tanzania Machi mwaka huu




Cherly na wenzake walipofika Uingereza wakitoka Tanzania


MKE wa Mlinzi wa Matajiri wa London, Chelsea ya Uingereza, Ashely Cole, Cheryl, ametajwa kuwa ni mwanamke mwenye MVUTO zaidi wa kimapenzi mwaka 2009.

Kimwana huyo amewabwaga mastaa kibao, Britney Spears amekuwa wa nne.

Cheryl na wasanii wenzake wa kundi la muziki la Girl Aloud walikuja Tanzania machi mwaka huu kupanda Mlima Kilimanjaro.

Angalia orodha 10 bora wenye mvuto wa kimapenzi, kwenye mabano ni nafasi zao mwaka jana.
FHM's 100 Sexiest supplement, featuring 52 pages of 'the hottest women in the world', comes free
with the June edition of FHM, on sale now. Here is the FHM 100 Sexiest Women 2009 top 10

1. Cheryl Cole (7)

2. Megan Fox (1)

3. Jessica Alba (2)
4. Britney Spears (31)

5. Keeley Hazell (3)

6. Adriana Lima (21)

7. Elisha Cuthbert (4)

8. Kristin Kreuk (48)
9. Anna Friel (re-entry)

10. Freida Pinto (new entry)

Polisi inawasaka ze utamu

MAKAO makuu ya Polisi yanafanya uchunguzi ili kuwabaini na kuwachukulia hatua wanaoendesha tovuti ya zeutamu.com kwa madai kuwa umekuwa ukitumika visivyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI) Peter Kivuyo, alisema jana kuwa polisi wanazifanyia kazi taarifa kwamba tovuti hiyo imetoa picha inayomdhalilisha Rais Kikwete.

Thursday, April 23, 2009

Madiba alipompiga tafu Jacob Zuma


Mzee Mandela akipanda kwenye jukwaa huku akisaidiwa na Jacob Zuma na Winnie Mandela.

Mandela akimtazama Zuma akiselebuka

Mikakati ya mwisho mwisho

Dah, Mzee Mandela akisalimiana na mkewe wa zamani Winnie.

Ilikuwa ni Aprili 19, siku ya mwisho ya kampeni za ANC kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini.
Mamilioni ya wananchi wa huko jana walipigia kura, hadi sasa ANC kinaongoza.