Friday, April 24, 2009

Buriani Phares Kabuye


Basi la R.S Investment baada ya kupinduka leo asubuhi

ALIYEKUWA Mbunge wa Biharamulo Magharibi mkoani Kagera, Phares Kabuye (TLP) amekufa kwenye ajali ya gari leo mkoani Morogoro.

Kabuye alikuwa akisafiri kwa basi la Rs Investiment lenye namba za usajili T 934 ADA akitoka Kagera kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa TLP unaofanyika Jumapili jijini humo.

Kbuye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na alijaza fomu kutetea nafasi yake.


Basi hilo aina Scania lilipinduka baada ya dereva kushindwa kulimudu, likapoteza mwelekeo likiwa kwenye mwendo mkali.


Inadaiwa kuwa wakati ajali hiyo inatokea basi hilo lilikuwa likiendeshwa na kondakta.



Kabuye alipata ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2005, Oktoba 12 mwaka 2007 Mahakama Kuu Tanzania ilitengua matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo kwa maelezo kuwa alimkashifu mgombea wa CCM, Anatoly Choya.

Katika miaka ya 1990 Kabuye alikuwa Mbunge wa CCM, na amewahi pia kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki.

Kabuye alikuwa na mvuto wa aina yake anaposimama kuzungumza bungeni kutokana na lafudhi yake, na hoja zake.

Bunge la Tanzania limekuwa likipoteza wabunge wanaokufa katika ajali, miezi kadhaa iliyopita, Salome Mbatia na Chacha Wangwe walikufa katika ajali za magari.

No comments:

Post a Comment