Thursday, April 30, 2009

Mabomu Dar yameua watano


HADI sasa milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mbagala mkoani Dar es Salaam imeua watu watano.


Mkuu wa Mkoa huo, William Lukuvi ameitaja idadi hiyo leo asubuhi wakati akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Channel Ten cha jijini humo.


Kwa mujibu wa Lukuvi, chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika na kwamba, uchunguzi utafanywa baada ya kwisha kwa moto katika ghala la silaha kambini hapo.


Mabomu yaliyokuwa yamehifadhiwa ghalani hapo yalilipuka jana kwa nyakati tofauti na kusababisha mitikisiko, moshi, nyumba zimebomoka, zimepata nyufa, na kuna nyingine zimeungua.


Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa, watu wengi wakiwamo watoto wamepotea na pia kulikuwa na uporaji na wizi kwenye makazi ya watu.

No comments:

Post a Comment