HALI ya usalama Mbagala bado si shwari, watu wengi wameumia na wengine wamezimia kwa hofu.
Taarifa kutoka kwenye kambi yalipolipuka mabomu hayo zimedai kuwa huenda itatokea milipuko mikubwa kuliko iliyotokea hadi sasa kwa kuwa kuna mabomu makubwa hayalipuka.
Hadi sasa Mbagala ni vurugu tupu, wengi wamezimia kwa mshtuko, wengi wamepotea wakiwamo watoto, na kuna nyumba zimeungua.
Kuna taarifa zinazodai kuwa watu kadhaa wamekufa, polisi hawajathibitisha.
Baadhi ya mabomu yamelipuka kwenye makazi ya watu, moshi umetanda Mbagala na kwa ujumla shughuli za kijamii zimeathirika sana.
Milipuko ilisikika hadi katikati ya jiji la Dar es Salaa, na kuna taarifa zinazodai kwamba mashine za ATM kwenye mabenki hazifanyi kazi.
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imewataka wananch wasiende Mbagala kwa kuwa eneo hilo ni hatari kwa sasa, na waliopo huko wasikae kwenye makundi.
Wananchi pia wametakiwa kuzima simu za mkononi kwa kuwa zinavutia mabomu.
Kuna taarifa kwamba, wananchi wameamriwa kutokaa kwenye maghorofa marefu hivyo huenda wafanyakazi wengi leo wamewahi kurudi makwao.
No comments:
Post a Comment