Saturday, October 24, 2009

Mume amuua mke kwa kisu

POLISI mkoani Rukwa inamshikilia mkazi wa hapa, Anthony Tundu (30) kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma kisu mkewe, kisha naye kujichoma kisu kwa nia ya kujiua kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, amesema,tukio hilo lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa 6.45 usiku, baada ya wanandoa hao kurejea nyumbani wakitoka katika kilabu cha pombe.

Inadaiwa kuwa,baada ya kuingia chumbani ulizuka mzozo baina yao, Tundu alimtuhumu mkewe, Sabina Sasala (25), kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya vijana katika eneo hilo.

Inadaiwa kuwa,Tundu,alimweleza mkewe kuwa, hali hiyo inamvunjia heshima na kusababisha ndoa yao idharaulike.

Kamanda amesema,baada ya kuzozana kwa muda mrefu, wanandoa hao walipigana.

Wapangaji wenzao hawakwenda kuamua ugomvi huo kwa kwa madai kuwa,walikuwa wamechoka kuwasuluhisha, kwa sababu wanandoa hao wana na tabia ya kupigana kila wanapolewa.

Mantage amesema,baada ya kupigana kwa muda mrefu,Tundu alisikika akitoka nje huku akitukana na kuelekea jikoni.

Kamanda Mantage amesema, Tundu alichukua kisu,alikwenda nacho chumbani na kumchoma mkewe tumboni,
utumbo ukatoka nje na akavuja damu nyingi.

Kamanda amesema,mwanamke alilia kwa sauti kubwa akiomba msaada kwa majirani, walifika chumbani na kumkuta sakafuni,mumewe alikwishakimbia.

Majirani walimchukua na kumkimbiza kituo cha Polisi cha mjini hapa, wakampeleka katika Hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga akiwa amepoteza fahamu,akafariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda Mantage, majirani walimtafuta Tundu, wakamkuta kichakani akiwa na jeraha kubwa tumboni, kisu kilikuwa pembeni yake,alikitumia kujichoma, walimpeleka hospitali, amelazwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Friday, October 23, 2009

Kataa kataa kata, kataa kata kataa, kata kiuno kata












OKTOBA 21, Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama aliwaita watoto acheze nao Ikulu.

First Lady wa USA si mchezo, watoto walitolewa kijasho, mama Obama anazungusha ringi kiunoni kama nini sijui, it was nice kwa kweli, natamani siku moja itokee na hapa kwetu.

Machozi ya damu

MWANAMKE nchini India, Rashida Khatoon, amekuwa gumzo nchini humo kutokana na hali yake ya kutoa machozi ya damu kila anapolia.

Rashida amewashangaza hata madaktari kwa hali yake hiyo ya kutiririka machozi ya damu kila anapolia.

Kwa siku mwanamke huyo humwaga chozi la damu mara kadhaa.

"Sisikii maumivu yoyote, badala ya machozi ya kawaida, damu zinapotitirika ni kitu cha kushangaza" alisema mwanamke huyo.


Viongozi wa dini wa India wanadai kwamba mwanamke huyo ni miujiza toka Mungu.

Thursday, October 22, 2009

Binti Mtanzania BBA 2009


BINTI Mtanzania katika jumba la Big Brother Afrika 2009, Elizabeth Gupta.


Alivyoingia alionyesha ana MSIMAMO kuhusu yale mambo yetu, kaanza kulainika?



Mrithi wa Mwanyika atema cheche

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema(55),amesema ana msimamo na haogopi shinikizo la yeyote.

Werema amesema,Rais Jakaya Kikwete anafahamu kuwa ana msimamo na waliowahi kufanya kazi na yeye wanatambua kuwa hafanyi uamuzi kwa kushinikizwa.

“Bila shinikizo hakuna kazi,mimi ni mtu wa msimamo,aliyeniteua anajua msimamo wangu na hata waliowahi kufanya kazi nami wananijua sishinikizwi na mtu” amesema Werema muda mfupi baada ya Rais Kikwete kumuapisha Ikulu, Dar es Salaam.

Werema anafahamu kuwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu inahusishwa na rushwa katika kuingia mikataba ya Serikali lakini yeye amesema “ninaporidhika ndipo mikataba itatekelezwa sitaki kushinikizwa”.

Amesema,hana taarifa rasmi kwamba,ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inahusika kuingia katika mikataba mibovu.

“Mimi sifahamu taarifa hizo nasoma kwenye magazeti hivyo nahitaji kufanya utafiti wa kutosha na kuwasiliana na taasisi nyingine za Serikali kupata taarifa kamili ndipo nijue kama nachukua hatua”.amesema.

Werema ana taaluma ya sheria ya biashara,namna ya kujadiliana katika mikataba na namna ya kufanya biashara ya umeme katika kubinafsisha nishati hiyo.

Amesema,ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haina uhaba wa wataalamu wa mikataba na amebainisha kwamba,mikataba mingine wanalazimika kuingia bila kuwa na uwezo wa kujadili ikiwemo ya Benki ya Dunia.

Jaji Werema amewahi kuwa wakili wa Serikali kwa miaka 23 kuanzia mwaka 1984,na Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu kuanzia mwaka 2007.

Anachukua nafasi ialiyoiacha Johnson Mwanyika,yupo kwenye likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Mwanyika aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Desemba, mwaka 2005.

Wednesday, October 21, 2009

Adaiwa kuua mashemeji WANNE kwa kuwachoma moto

JESHI la polisi mkoani Tabora limemkamata Salum Katunija(35)kwa tuhuma za kuua watoto wanne kwa kuwachoma moto.

Katumija anatuhumiwa kuwaua watoto hao wa familia moja Oktoba 17 mwaka huu saa nne usiku.

Kwa mujibu wa Polisi watoto waliouawa ni wadogo wa mke wa mtuhumiwa, wametengana siku chache zilizopita.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Emson Mmari,amesema, Katunija, anatuhumiwa kuwateketeza watoto hao katika kitongoji cha Ikami,kijiji cha Nyangahe, kata ya Bukumbi wilayani Uyui,mkoani Tabora.
Wakati watoto hao wanachomwa, mama yao mzazi,Kulwa Shija,na binti yake mwingine,Rehema Joseph,walikuwa jirani wakisherekea harusi ya ndugu yao.
Mmari amesema,wakati wakiendelea kushehereka,ghafla waliona moto ukiwaka katika nyumba yao,wakakimbia kwenda huko na kukuta nyumba hiyo ikiungua.

Amesema,walipiga kelele za kuomba msaada, wananchi wakaacha kushehereka harusi wakaenda kujaribu kuuzima moto huo lakini ilishindikana.Watoto wote waliokuwa ndani ya nyumba waliteketea.

Kwa mujibu wa Kamanda Mmari, watoto waliokufa ni Malecha Juma,(11)aliyekuwa darasa la tatu,Shija Juma,(10) aliyekuwa darasa la pili,wote walikuwa wanasoma shule ya msingi Ukili katika kata ya Bukumbi.

Marehemu wengine ni Mageta Juma,(7) na Dotto Juma (4),walikuwa hawajaanza shule. Kamanda Mmari amesema,Polisi walifanya uchunguzi wakabaini kuwa, Salum Katunija alikuwa ni mume wa Rehema Joseph,walikuwa wameachana siku chache zilizopita.
Amesema, wanandoa hao walitengana kutokana na kinachodaiwa kuwa ni mke kumchoka mume kwa sababu ya ulevi na kupigwa.

Kwa mujibu wa Mmari,Katunija alikuwa akifika nyumbani kwa mkwewe,Kulwa Shija,ili amuombe mkewe msamaha warudiane, ikashindikana.
Kamanda huyo amesema,baada ya juhudi zake kushindikana,Katunija aliamua kuwachoma moto shemeji zake kwa kuwa mkewe aligoma kurudi nyumbani.
Mmari amesema, Polisi wanachunguza kubaini ukweli wa tukio hilo,mtuhumiwa yupo rumande.

Tuesday, October 20, 2009

Polee, nyamaza basii


Wanaume wakenya wafunga ndoa London


WANAUME wawili raia wa Kenya,Daniel Chege (39) na Charles Ngengi(40) wamefunga ndoa jijini London, Uingereza.

Ndoa hiyo imekuwa gumzo jijini humo hasa ikizingatiwa kuwa ni mara ya kwanza kwa shoga mkenya kuolewa nchini Uingereza.

Soma hapo chini

The wedding has been the talk of the week in London among the Kenyan communities.

The wedding of Mr. Daniel Chege Gichia, 39, who wed Charles Ngengi, 40, in London on Saturday 17th October, 2009.

It is the first Kenyan gay wedding in the UK where both partners are from Kenyans.

A team of about 20 people including the guests arrived at at Islington Council Registry Office, Islington Town Hall, North London at 11.30 am.

The bridal party consisted of two Kenyan ladies and two Kenyan men of which one had flown from Holland for the wedding. There was very strict instructions about the press.

The press people were denied entry to the registrar's office and even afterwards there was a heated argument press men where the bridal party insisted that the press men should leave but they had no power to do so as it was in a public place.

After the wedding a reception ceremony followed in North London at Safari Bar, 975 High Road, North Finchley. About 100 guests attended the reception.

There was tension at the reception as some of the security team evicted some cameramen fearing that the news and photos would land into Kenya newspapers.

Among the guests who attended the wedding was a old Kenyan lady currently visiting UK who was escorted by her three daughters to the wedding.
After witnessing what was happening the old lady had this to said: How come God allowed me to come over to the UK to see such things. Why? Is this what is causing our girls not to marry?) "the disappointed lady commented.

Monday, October 19, 2009

Mke wa Ashley Cole 'anapokamua'




MKE wa mwanasoka mahiri wa Uingereza, Ashley Cole, Cherly 'akikamua' jukwaani mwishoni mwa wiki.
Nyota huyo wa kundi la Girl Aloud aliwapagawisha mashabiki wake hasa alipoimba wimbo uitwao Fighting for this love

'Jisaidie kabla ya kupanda ndege'

SHIRIKA la ndege la Japan, All Nippon Airways (ANA) limeanzisha mbinu ya aina yake ya kubana matumizi na kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Shirika hilo linawataka abiria wake waende chooni kwanza kabla ya kupanda ndege.

Shirika hilo lilisema kwamba abiria wakipanda ndege baada ya kujisaidia watakuwa wamepunguza uzito katika ndege na hivyo lita za mafuta ya ndege yatakayotumika zitapungua.

Shirika hilo la ndege linaweka wafanyakazi wake kwenye mageti ya njia zinazokwenda sehemu za kupanda ndege.

Jukumu la wafanyakazi hao ni kuwakumbusha abiria kwenda chooni kwanza kabla ya kupanda ndege.

Shirika hilo la ndege linaamini kwamba uzito utakaopungua kwenye ndege zao utasaidia kupunguza matumizi ya mafuta ya ndege na hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kiasi cha tani tano za gesi ya Carbon Dioxide katika kipindi cha mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa televisheni ya NHK ya Japan, shirika hilo la ndege lilianza majaribio ya mwezi mmoja ya mpango huo Oktoba mosi mwaka huu.

Kama majaribio hayo yataonyesha mafanikio kwa ndege zao 42 basi mbinu hiyo ya kubana matumizi itaendelezwa kwa ndege zote za shirika hilo.

Ajali, maajabu


NIMEWAHI kushuhudia basi lenye abiria lilitumbukia mtoni wilayani Arumeru, Arusha, lakini sijawahi kuona au kusikia gari likipanda juu ya paa!
Ni ajali ya aina yake, na unaweza kukisia lilikuwa katika mwendo mkali kiasi gani hadi likafika huko juu.
Wakati gari hilo linaanguka juu ya paa, wanandoa, Peter na Kay Arnold walikuwa ndani ya nyumba hiyo, wamesurika.
Dereva ameumia sana.
Ajali hiyo imetokea jijini Sydney, Australia.

Katoa mimba 15 katika miaka 17

IRENE Vilar wa Colorado, Marekani alishika ujauzito mara 15 katika kipindi cha miaka 17 lakini alizotoa zote kabla hazijawa kubwa.
Anasema,alifanya hivyo si kwa sababu alikuwa na matatizo ya kiafya,mumewe hakutaka mtoto na hakutaka waachane kwa sababu hiyo.
Kwa sasa mwanamke huyo ana umri wa miaka 40, ameandika kitabu kilichosababisha malalamiko nchini Marekani kiasi cha kusababisha watu wengine wamtumie ujumbe wa kumtishia maisha yake.
Baadhi ya watu wanashinikiza Irene afungwe jela kwa vichanga 15 alivyovikatisha maisha yao.

Irene alianza safari yake ya 'kuzipanchi' mimba alipokuwa na umri wa miaka 16 akaimaliza alipofikisha umri wa miaka 33.

Ana watoto wawili Loretta, 5, na Lolita, 3, katika kitabu hicho ameeleza namna alivyotoa mimba hizo 15.
Kitabu hicho kinaitwa "Impossible Motherhood: Testimony of an Abortion Addict".

Irene alikubaliwa kuingia chuo kikuu cha New York University akiwa na umri mdogo wa miaka 15 na hapo ndipo alipoanza mapenzi na mwalimu wake wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 50 na baadae kuoana naye mwaka
uliofuatia.

Irene anasema, mwalimu wake huyo ambaye alikuwa ni profesa wa masuala ya lugha, alikuwa hataki kuzaa naye mtoto kwa kile alichodai kwamba uhusiano wake wa kimapenzi huwa hauzidi miaka mitano na kupata mtoto kungeharibu uhusiano wao.

Irene alikuwa akitumia vidonge vya kuzuia mimba mara chache sana na wakati alipoacha kutumia vidonge hivyo na kupata mimba, alikuwa akizitoa mimba hizo.
Irene anadai kwamba alikuwa akizitoa mimba hizo ili kuepuka asije akakimbiwa na mumewe huyo lakini baadae alitokea kupenda kutoa mimba.

Hata hivyo Irene alikataa kusema kama mumewe alikuwa na taarifa yoyote ya tabia yake ya utoaji mimba.

Sala ya kumuombea mzazi


"Dear God, please send clothes to all those poor naked ladies in Daddy's Cellphone, Amen."

Friday, October 16, 2009

Halooo, halooo, hapo ni makumbusho?

JAMAA anapiga simu ofisi ya makumbusho ya Taifa.

"Haloo hapo ni makumbusho ya taifa?

OFISI:Ndio tukusaidie nini?

JAMAA:"Ok, naomba mnikumbushe mwaka juzi saa yangu niliipoteza wapi?"

OFISI:"Pumbavu hiyo siyo kazi yetu"

JAMAA:Sasa makumbusho mnakumbusha nini?"

OFISI:Tunahifadhi mambo ya zamani.

JAMAA:"Ahaa.....kumbe saa yangu mtakuwa nayo!" Nakuja kuichukua sasa hivi.

Mtanzania (Elizabeth) katika jumba la BBA
















Thursday, October 15, 2009

Maswali kabla ya kuoa/kuolewa

KABLA ya kutamka “Hadi kifo kitakapotutenganisha”, au hata kabla ya kukubali kuvishwa pete ya engagement kuna maswali muhimu sana (hard questions) ambayo unahitaji kujiuliza.

Ukijiuliza maswali hayo unaweza kufahamu success au failure ya mahusiano ya ndoa pengine hata kabla ndoa haijafika popote.

Kujiuliza mwenyewe na kumuuliza yule unayatarajia kuoana naye itakusaidia kufahamu kama umempata mtu sahihi na pia kuweza kuondoa matatizo ya kawaida ambayo wengi hupelekea kuachana.

Chukua muda (honestly) kufanya evaluation ya namna unavyojisikia (feelings) na motivations kwa ajili ya wewe kuoa au kuolewa.

Ni vizuri kupata majibu ya maswali kabla hujaoana naye ili kuweza kushughulikia matatizo hayo kabla ya ndoa kuanza.

Kuna maeneo muhimu sana katika ndoa ambayo bila kuyafahamu na kuingia kichwa kichwa hakuna wa kumlilia isipokuwa wewe mwenyewe.

Suala la ndoa ni sensitive sana,ukishindwa acha utapata alama utakayoibeba maisha yako yote hapa duniani na pia unaweza kuathiri maisha ya wengine.

Swali la kwanza

Je, ni kweli tunapendana?
Je, ni kweli nitaendelea kumpenda hata miaka 30 ijayo?
Ni kitu gani au sifa zipi zinanifanya nimpende?
Uwe mkweli unapoyajibu haya maswali.

Unahitaji kufahamu na kujisikia ni kweli unampenda mwenzako isije kuwa ni tamaa tu.

Upendo huanza kidogokidogo na hutokea kwa kumpenda mtu mzima kama alivyo, awe ana pesa au la na pia si kumpenda kama wewe unavyotaka awe.

Kumbuka mke au mume si kipande cha udongo wa mfinyanzi kwamba utamefinyanga kwa kadri unavyotaka wewe.
Swali la pili:
Kwa nini tunaoana?
Kwa nini namhitaji kuoana naye?
Ni kwa sababu ninataka mtoto?
Ni kwa sababu ninataka hela zake au najisikia upweke upweke, au nataka sex au nataka kuondokana na kero za mama au wazazi?

Au naona nachelewa kuolewa/kuoa? au rafiki zangu wananisema sana au na mimi nionekane nimeoa au kuolewa?
Kuoa au kuolewa kwa sababu za ajabu ajabu huweza kukufikisha mahali ambapo utajikuta upo disappointed, frustrated na hatimaye kuachana.

Oa au olewa kwa sababu ni wakati wake na umwe umeamua wewe.
Swali la tatu:

Ni nini matarajio ya ndoa yangu?

Umejiandaa kuwa mume/ mke?
Umejiandaa kuwa baba/mama?
Upo tayari kuvumilia changamoto za ndoa?

Matarajio ya mtu anapoamua kuingia kwenye ndoa huweza kujenga au kuharibu ndoa.

Kuna baadhi ya imani potofu kuhusu ndoa,unatakiwa kuzifahamu hata kabla hujaingia kwenye ndoa. Kuamini kwamba ukiolewa basi mwenzako anatakiwa kukufanya happy si kweli, furaha unayo wewe kwanza.

Kufikiria kwamba eti mume/mke ataweza kusoma akili yako si kweli, unahitaji kueleza kile unachotaka na si kubaki kimya eti anajua.

Kuamini kwamba ukioa au kuolewa basi kila kitu mtafanya pamoja si kweli, kila mtu ana interest zake.

Na kutaka kuwa na ndoa unayotaka wewe badala ya wote kwa pamoja unaweza kujikuta kwenye total disappointment. "Truly loving another means letting go of all expectations.

It means full acceptance, even celebration of another's personhood."

Atengana na mkewe, anyonga watoto wao

NI taarifa ya kusikitisha, mwanaume raia wa Zimbabwe, Petros Williams (37) anadaiwa kuua wanawe wawili, Yolanda(4) na Theo (2) kwa kuwanyonga nyumbani kwake nchini Uingereza.
Inadaiwa kuwa amefanya hivyo kama kisasi baada ya kutengana na mkewe ambaye ni mama mzazi wa watoto hao.

Mama watoto hao, Morongoe Molemohi (30) ni raia wa Afrika Kusini.


Soma Zaidi hapo chini
Father is being questioned by police on suspicion of murder after his two young children were found
strangled at their home.

Yolanda Molemohi, four, and her two-year-old brother Theo were found unconscious in their bedroom by their
horrified mother.

It is understood they were found with narrow cord wrapped around their necks with their father beside them.

Yolanda Molemohi, four, and her two-year-old brother Theo were found strangled in their bedroom Although their mother, Morongoe Molemohi, 30, tried desperately to revive the youngsters, they were
pronounced dead in hospital.

It has been revealed that Mrs Molemohi and her Zimbabwean-born husband, Petros Williams, 37, had recently separated and that the children had been spending the past few days with their father.

Detectives are examining the possibility that Williams, a finance director, murdered his children in revenge for his churchgoing wife walking out on him.

It is understood that Williams, who was rambling and incoherent, collapsed at a police station and was taken to hospital. He is due to be questioned over the double killing.

Fainali ya BSS



USIKU wa Oktoba 13 ilikuwa ni fainali ya shindano la kusaka vijana wenye kipaji cha kuimba.
Kijana kutoka Mwanza, Paschal Cassian a.k.a Baba Rita(Aliyevaa shati la kijani/ Jeusi) alifanya kweli na kuwa mshindi wa BSS mwaka huu.
Paschal kajipatia zawadi ya Sh milioni 25, Sh milioni 1.5 kwa kuwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la kutunga wimbo wa ukimwi na nyinginezo.
Uwezo wa kuimba wa kijana huyo ulisababisha Jaji Mkuu wa shindano hilo, Rita Paulsen na jaji mwenzake, Master J wasimame kutoa heshima kwake.
Awali majaji hao walionyesha wazi kumkubali zaidi mshiriki mwingine, Kelvin Mbati (Aliyevaa shati la Bluu) lakini wapenzi na mashabiki wa muziki walitofautiana nao.



















Adhabu


Monday, October 12, 2009

Ni kweli?

Wanawake wanajali (caring) na wanafahamu kupenda (loving),

Wanawake hutoa machozi hata wakiwa na furaha,

Wanawake hufanya hata vitu vidogo vidogo kuonesha wanajali,

Wanawake huweza kusimama mahali popote kwa ajili ya kitu wanachokiamini ni the best kwa watoto wao.

Wanawake wanauwezo wa kutabasamu hata kama wamechoka, hawawezi kujizuia.

Wafahamu namna ya kubadili mlo wa kawaida na kuwa special kwa occasion yoyote.

Wanajua jinsi ya kumfariji rafiki au mtu ambaye anaumwa.

Wanawake huleta kicheko na furaha duniani.

Wanajua namna ya kumliwaza mtoto kwa saa nyingi.
Wanawake wengi ni wakweli na watiifu.

Wanawake wengi hujikuta wanatoa machozi wanapojikuta wanakosa haki yao.

Wanawake wanafahamu wafanye nini ili mwanaume ajisikie ni mfalme.

Wanaweza kwenda extra mile kumsaidia rafiki yao.

Wanawake wanawezesha dunia kuwa mahali bora kuishi.

Wanaume wana sifa muhimu zipi?

Friday, October 9, 2009

Zombe kaomba kustaafu

“Ifikapo Septemba 21, mwaka huu, nitakuwa natimiza umri wa miaka 55 ambapo kwa hiari yangu mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua nistaafu kwa hiari, hasa nikizingatia matatizo ambayo nimeyapata kwa kubambikiziwa kesi ya mauaji na huku taratibu za kisheria zikikiukwa wazi wazi kwa hila na kunikomoa.

“Napenda kufahamisha ofisi yako kuwa, ifikapo Septemba 21, mwaka huu, mimi naomba nistaafu kwa hiari na nilipwe mafao yangu yote kama sheria inavyoelekeza katika kifungu Na.58(4) cha “Police Force and Auxilliary Service Act, R.E 2002’, baada ya kuonekana sina hatia ya kosa hilo la mauaji na nilipoachiliwa na Mahakama Kuu Agosti 17 mwaka huu, na vifaa vya serikali ikiwemo sare za jeshi nitazirudisha pasipo shaka,” inasema sehemu ya notisi hiyo.

Kwa mujibu wa barua yake kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), aliyoiandika Septemba 22, mwaka huu, ambayo ilipokelewa na ofisi ya IGP, alimwarifu mkuu huyo kuwa anakabidhi kitambulisho cha kazi Na. 8051 kilichotolewa Machi 8, mwaka 1999 kwa cheo cha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Abdallah Zombe.

“Katika barua hii ya pili kwako IGP, napenda kurudia tena nimeamua kustaafu kwa hiari katika Jeshi la Polisi Tanzania baada ya kubambikiziwa kesi ya mauaji kwa makusudi yaliyo wazi, huku vifungu vya sheria ya nchi hii vikikiukwa wazi wazi kwa lengo la kunikomoa.

Afya ya Rais Kikwete hadharani

DAKTARI wa Rais Jakaya Kikwete amesema kiongozi huyo hana matatizo yoyote ya kiafya.

Dk. Peter Mfisi, amesema, vipimo anavyofanyiwa kila mara Rais vinaonesha hana matatizo yoyote mwilini mwake zaidi ya maumivu ya shingo na wingi wa damu mwilini.

Ameyasema hayo wakati akizungumzia mjadala uliojitokeza kupitia vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu afya ya Rais, baada ya kukatiza hotuba Jumapili iliyopita katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Wakati akizungumza uwanjani hapo,Rais Kikwete aliishiwa nguvu,na kwa mujibu wa daktari wake, tatizo ilikuwa ni uchovu wa safari.

Rais Kikwete alikwenda Kirumba kushiriki maadhimisho ya miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT).

“Wakati tukio hilo linatokea nilikuwapo, nilichukua vipimo muhimu kama daktari anavyotakiwa kufanya linapotokea tukio kama lile kwa mtu.

Vipimo vyote vilithibitisha kuwa Rais hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya ambayo yangeweza kuhusishwa kuwa chanzo cha tukio lile,” alisema Dk. Mfisi.

Daktari huyo anasaidiana na daktari bingwa wa maradhi ya moyo katika Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili,Dk. Mohamed Janabi, kumtibu Rais Kikwete Dk Mfisi alisema, ingawa maadili ya kazi yake ya udaktari hayamruhusu kutoa siri ya ugonjwa wa mtu anayemtibu,kwa kuzingatia maslahi ya taifa na umma wa Watanzania, na kwa kuwa Rais mwenyewe ameridhia taarifa hizo zitolewe, aliamua kuzungumza na waandishi wa habari.

Akifafanua kuhusu vipimo alivyomfanyia uwanjani Kirumba muda mfupi baada ya kuzidiwa na uchovu, Dk. Mfisi alisema,msukumo wa damu yake ulikuwa wa kiwango cha 130/85mmhg ambacho ni cha kawaida kwa mtu wa umri wake.
Oktoba 7, Rais Kikwete alitimia umri wa miaka 59.

“Mapigo ya moyo wake yalikuwa 76 kwa dakika ambayo pia ni ya kawaida.
Sukari kwenye damu ilikuwa 5.5mmol/l ambayo nayo ilikuwa ya kiwango cha kawaida. Joto la mwili lilikuwa digrii 37.5 za sentigredi ambalo ni la kawaida.

Rais pia hakuwa na kiungo chochote kilichoonekana kutetereka, jambo ambalo lilithibitisha kuwa hakupata kiharusi,” alisema Mfisi na kuongeza ndiyo sababu akamruhusu kuendelea na sherehe.

Alisema,baada ya kurudi Dar es Salaam, aliwasiliana na madaktari wenzake wa ndani na nje ya nchi na kuwasimulia tukio na vipimo, walithibitisha kuwa tatizo lilikuwa ni uchovu kwa sababu wanaifahamu vizuri afya ya Rais Kikwete kwa kuwa mmoja wao alimchunguza siku moja kabla ya kuondoka New York, Marekani, kurejea nchini mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Napenda kuwahakikishia wananchi wenzangu kuwa katika miaka hii minne, Rais wetu amefanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake.
Nadiriki kusema kuwa hakuna kipimo ambacho hatujapata kukifanya katika uchunguzi wa mambo muhimu ya afya yake,” alisisitiza.

Rihanna
















Mume wa shoga ajiua

MUME wa shoga amejiua nchini Uingereza baada ya mkewe (mwanaume mwenzie) kumkimbia na kuanza penzi jipya kwa mwanaume mwingine.

Mwaka 2006 mchekeshaji maarufu wa nchini Uingereza,Matt Lucas,ambaye ni shoga alifunga ndoa na mpenzi wake Kevin McGee.
Harusi yao ilikuwa ya kukata na shoka, mastaa wengi wakubwa Uingereza walihudhuria.

Ndoa hiyo ya jinsia moja ilivunjika mwaka jana, na ikawa ndoa ya kwanza ya watu wa jinsia moja kuvunjika tangu ndoa hizo ziliporuhusiwa nchini Uingereza mwaka 2005.

Inadaiwa kuwa ndoa hiyo ilivunjika kwa kuwa,Lucas alishindwa kuvumilia tabia ya mumewe ya kutumia dawa za kulevya.

Baada ya Luca kumkimbia mumewe,Kevin alizidisha matumizi ya dawa za kulevya,na alipogundua kuwa Lucas kapata bwana mwingine, alijiua.

"Kifo ni bora kuliko kuendelea kuishi" ndio ujumbe wa Kevin aliouacha kwenye ukurasa wake wa Facebook saa chache kabla ya kujiua.

Baada ya polisi kutaarifiwa kuhusu ujumbe wa Kevin kwenye Facebook, waliukuta mwili wake nyumbani kwake, mjini Edinburgh.

Sifa za ufataki zampeleka jela, kuchapwa bakora 1,000

MKAZI wa mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia,Mazen Abdul Jawad, alikamatwa baada ya kuhudhuria kipindi kinachoitwa "Red Line" kinachoandaliwa na televisheni ya LBC yenye makazi yake nchini Lebanon.

Katika kipindi hicho chenye watazamaji wengi nchini Saudia, Jawad alijisifu kwa namna alivyokuwa akifanya mapenzi na wanawake mbali mbali.
Alijisifu pia kuwa alianza kufanya mapenzi tangu alipokuwa na umri wa miaka 14.

Kipindi hicho kilirushwa hewani julai 15 mwaka huu na kusababisha hasira miongoni mwa wananchi wa Saudi Arabia.

Takribani watu 200 walifungua mashitaka ya malalamiko dhidi ya Abdul Jawad, ambaye ni mfanyakazi wa shirika la ndege la Saudia.

Serikali ya Saudia iliamua kuchukua hatua kali kwa kuzifunga ofisi mbili za LBC nchini humo na kumkamata na kumfungulia mashitaka Abdul-Jawad.

Kipindi hicho kilianza kwa kumuonyesha Abdul-Jawad, akielezea namna alivyomla uroda jirani yake wakati huo akiwa na umri wa miaka 14.

Baada ya hapo aliwaongoza watazamaji kwenye chumba chake ambacho takribani vitu vyote ni vya rangi nyekundu na aliwaonyesha pia wanasesere wake kwa ajili ya ngono.

Baada ya hapo alijiunga na wanaume wengine watatu na kuanza kujadiliana masuala ya ngono.

Mahakama ya nchini Saudia ilimuona Abdul-Jawad ana hatia na ilimhukumu kwenda jela miaka mitano pamoja na kuchapwa jumla ya bakora 1,000.

Mbali na adhabu hizo, mahakama imeamuru kuwa,Abdul-Jawad,asisafiri kwa miaka mitano baada ya kutoka jela.
Kwa mujibu wa amri hiyo,hataruhusiwa kuongea na vyombo vya habari kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kumaliza kifungo chake.

Mwanasheria wake alitangaza kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.
alidai kwamba,Abdul-Jawad alikuwa akielezea maisha ya mapenzi ya watu wengine.

Mwanasheria huyo alidai kwamba televisheni ya LBC ilikuwa ikimrekodi mazungumzo yake bila kufahamu kwamba alikuwa anarekodiwa.

Wanaume wengine watatu ambao walichangia mawazo yao katika mjadala wa mapenzi wa Abdul-Jawad walipatikana na hatia ya kujadili masuala ya mapenzi hadharani na walihukumiwa kwenda jela miaka miwili na kuchapwa bakora
300 kila mmoja.

Wednesday, October 7, 2009

Idd Simba awachokoza wabunge

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Idd Simba, amesema, lugha ya kiingereza imesababisha Tanzania iwe na sheria mbaya za madini.

Mbunge huyo wa zamani wa Ilala, Dar es Salaam amesema,anaona aibu kwa kuwa alishiriki kupitisha sheria mbaya za madini zinazotumika kuinyonya nchi.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa,chanzo cha ubaya wa sheria hizo ni lugha ya kiingereza kwa kuwa zimeandikwa kwa lugha hiyo lakini idadi kubwa ya wabunge hawaielewi kwa ufasaha.

“Zile sheria ni mbaya na mimi naona aibu kwamba zilipitishwa wakati nikiwa kwenye lile Bunge, lakini unatarajia nini wakati sheria zile zinatungwa kwa Kiingereza,na si wabunge wengi wanaoelewa lugha hiyo,” amesema.

Akijibu maswali baada ya kuwasilisha mada kuhusu nafasi ya sekta binafsi kwenye utawala na maendeleo, Simba amesema,kwa kuwa sheria nyingi zimeandikwa kwa Kiingereza,mambo mengi yanapitishwa bungeni bila wabunge kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sheria husika.

“Huu ndio ukweli halisi na haya ni maoni yangu,” amesema Simba baada ya kuulizwa swali iweje sasa baada ya kukaa pembeni anaona namna sekta binafsi inavyonufaisha wageni zaidi kuliko wazawa, hasa kwenye sekta ya madini wakati sheria zilipitishwa naye akiwa Mbunge.

AY alipokamua BBA Afrika Kusini


MSANII nyota wa nyimbo za bongo flava, Ambwene Yesaya a.k.a AY akikamua wakati wa onyesho maalum la Big Brother Afrika(BBA) Revolution 2009 Jumapili iliyopita nchini Afrika Kusini.

Hongera Brian a.k.a Imeda




Rais Kikwete leo anatimiza umri wa miaka 59, Brian jana alitimiza umri wa miezi TISA.
Nawapongeza kwa hatua waliyofikia, Mungu awalinde na kuwaepusha na mabaya ya dunia hii.

Happy birthday Rais Kikwete











RAIS Jakaya Kikwete leo ametimiza umri wa miaka 59.
Rais Kikwete alizaliwa Oktoba 07,1950 katika kijiji cha Msoga mkoani Pwani.

Monday, October 5, 2009

Marafiki wa kukodi

KAMA unahitaji watu watakaojifanya kuwa marafiki zako wa karibu sana wakati unapopiga misele kwenye mitaa ya Japan basi usitie shaka, kuna kampuni nyingi zinazotoa huduma ya kukodisha marafiki.

kampuni hizo zinatoa watu watakaojifanya marafiki au hata ndugu wa karibu kwenye misiba na hata sherehe za harusi.

Ukitaka hata mtu wa kujifanya mume wako au mke wako usiwe na hofu kwani kampuni za marafiki feki zitakutatulia tatizo hilo.

Kampuni ya kwanza ya marafiki feki ilianzishwa nchini humo miaka tisa iliyopita lakini hivi sasa kuna kampuni kubwa zaidi ya 10.

Mojawapo ya kampuni hizo inayoitwa Hagemashi Tai ikiwa na maana ya "Nataka kukufurahisha" huwatoza wateja wake sawa na Tsh. laki mbili kwa rafiki mmoja feki wa kupiga naye misele.

Kama unahitaji rafiki feki wa kujifanya rafiki wa karibu na kutoa hotuba ya kukusifia kwenye harusi yako basi kuna malipo ya ziada ambayo hutolewa.

Mfumo wa maisha ya kisasa ndio unaosemekana kuchangia watu wengi kuwa wapweke na kuwa na marafiki wachache wanaowazunguka hivyo kuhitaji marafiki zaidi feki wa kupiga nao stori au kuwa karibu nao wakati wa sherehe au kwenye misiba.

Hiroshi Mizutani, mmiliki wa kampuni ya marafiki feki ya Office Agents yenye wafanyakazi 1,000 alisema kwamba marafiki feki anaowakodisha kwa watu huwa wanavaa nadhifu na huonyesha furaha wakati wote kama vile watu wenye kazi bora duniani.

Iwapo marafiki feki watahitajika kusimamia harusi basi hujifunza historia ya wanandoa mapema kabla ya kuhudhuria harusi.

Wasanii wengi wa maigizo wamekuwa wakilichangamkia dili hilo la marafiki feki na makampuni mengi bado yanahitaji wasanii zaidi watakaoigiza kama marafiki feki katika maisha ya kweli ya kila siku.

Ndoa ya Obama miaka 17




RAIS Barack Obama(48) wa Marekani na mkewe, Michele (45)wamefanya kumbukumbu ya miaka 17 ya ndoa yao. Wana watoto wawili, Sasha na Malia.

Mwanza yatesa Miss Tanzania 2009

MISS Tanzania 2009 ni Miriam Gerald (20).

Msichana huyo kutoka Mwanza, amewashinda warembo wengine 28
Mrembo huyo ataiwakilisha Tanzania katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini.

Miriam amejipatia pia zawadi ya gari aina ya Suzuki Grand Vitara lenye thamani ya Sh milioni 53 na Sh milioni tisa.

Licha ya kushinda taji hilo, msichana huyo amechaguliwa kuwa Miss Redd's Photogenic 2009 linalotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).

Beatrice Lukindo (20) kutoka vyuo vya elimu ya juu ameibuka kuwa mshindi wa pili.

Msichana huyo atapata zawadi Sh milioni 6.2 zinazotolewa na Kampuni ya simu za mkononi,Vodacom Tanzania.


Juliet Emmanuel wa Ilala(19) amekuwa mshindi wa tatu, atajipatia zawadi ya Sh milioni nne zilizotolewa na Vodacom.

Sylvia Shally(19) ni mshindi wa nne na Sia Ndaskoi ni mshindi wa tano.
Mwakilishi wa Kanda ya Mashariki, Tory Oscar (21) ameibuka kuwa mrembo mwenye kipaji, atapata zawadi ya Sh 500,000.

Sia Ndaskoi(19) amechaguliwa kuwa Balozi wa Utalii wa Ndani.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) itampa mrembo huyo wa Temeke Sh milioni 2.1, na Laptop ya kisasa.

Friday, October 2, 2009

Swali la leo

Mnagombania ndizi mgomba wenu?

Dogo 'kapinda'

Mtoto Dong Dong wa nchini China ana umri wa miaka MINNE, kawashangaza watu wengi kwa tabia yake ya kunywa pombe na kuvuta sigara kupita kiasi.
Picha ya mtoto huyo akivuta sigara ilitolewa kwenye gazeti la Jianghuai Morning Post.
Gazeti hilo limesema, mtoto huyo alianza kuvuta sigara tangu alipokuwa na umri wa miaka miwili.
Dong Dong anaishi na bibi na babu yake kwenye kijiji cha Banqiao katika mji wa Anhui nchini China.
Bibi yake ambaye ana duka la chakula, sigara na bidhaa mbali mbali kwenye kijiji hicho, alielezea tabia ya mtoto huyo kuiba sigara kwenye duka lake.
"Wakati anapohitaji sigara huchukua toka nyumbani au huiba paketi ya sigara kwenye duka langu".
Bibi yake aliendelea kusema, mbali na tabia yake ya kuvuta sigara iliyopindukia Dong Dong pia hunywa sana pombe.
Daktari Zhang Gong, toka hospitali ya watoto ya mji huo, alielezea kushangazwa sana na jinsi mtoto huyo anavyovuta sigara na kutoa moshi kama gari moshi.

"Kwa jinsi anavyovuta sigara, anaonekana ni mzoefu sana na ana historia ndefu ya kuvuta sigara ingawa umri wake ni mdogo", alisema Dr Zhang.

Dong Dong ni mmoja kati ya watu milioni 350 wanaovuta sigara nchini China.
Idadi hiyo ya wavutaji sigara China ni kubwa kuliko nchi yoyote duniani.
Kwa mujibu wa tovuti ya TobaccoChina.net , asilimia 60 ya wanaume wa nchini China wenye umri wa kuanzia miaka 15 wanavuta sigara mara kwa mara.

Bikira za China Sh 20,000

Baada ya kutoa dawa za kuongeza ukubwa wa makalio na mapaja ya wanawake, wachina wametoa vifaa vinavyotumika kama bikira kwa wanawake.
Bikira hizo feki zimeanza kuzua mtafaruku mkubwa kwenye nchi za kiarabu.
Vifaa hivyo vina soko zaidi kwenye nchi za kiarabu kwani kwa mujibu wa tamaduni za nchi hizo mwanamke anayeolewa akiwa hana bikira huonekana ni muhuni na huitia aibu familia yake.

Katika nchi za kiarabu si jambo geni ndoa kuvunjika siku ya harusi baada bwana harusi kula tunda kwa mara ya kwanza na kukuta tunda lake likiwa limeshadokolewa.

Bikira hizo feki zina uwezo wa kutoa damu bandia wakati wa kujamiiana na hivyo kumwezesha bi harusi ambaye hana bikira ya kweli, kuzuga kama vile bikira yake ndio inavunjwa kwa mara ya kwanza.

Bikira hizo feki zimesababisha mtafaruku mkubwa nchini Misri.
Wabunge nchini humo wanataka adhabu ya kifo itolewe kwa mtu yeyote atakayeziingiza nchini humo.
Wabunge hao wamesema,kwa kuwa bikira hizo feki zinatumika kwa lengo la kuwadanganya wanaume, wametaka Serikali itoe tamko la kuzipiga marufuku kuingizwa nchini humo.

Bikira hizo feki zimepata soko kubwa kwa kuwa zinauzwa kwa bei chee hivyo hazina gharama kama zilivyo operesheni za kutengeneza bikira.
Operesheni hizo hufanyika kwa siri kwenye baadhi ya mahospitali katika nchi za kiarabu.

Nchini Syria bikira hizo feki kutoka China zinauzwa kwa dola 15 (Tsh. elfu 20) tu.

Miss Tanzania hapatoshi leo

LEO ni leo, saa kadhaa zijazo watanzania watamfahamu mwakilishi wao katika shindano la urembo la kimataifa, Miss World linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Majaji tisa leo watamchagua msichana mmoja kati ya 29 awe Miss Tanzania 2009.
Homa ya shindano hilo imepanda miongoni wa warembo hao, na kila mmoja amejigamba kwamba atashinda taji hilo kumrithi Miss Tanzania wa sasa, Nasreen Karim.
Kuanzia saa moja usiku,tovuti za www.habarileo.co. tz na www.dailynews.co.tz zitarusha 'live' taarifa za shindano hilo kutoka ukumbini,Dar es Salaam.
Miss Tanzania 2009 atapata zawadi ya gari aina ya Suzuki Grand Vitara lenye thamani ya Sh milioni 53, na fedha taslimu Sh milioni tisa.
Mshindi wa pili atapata Sh milioni 6.2, mshindi wa tatu Sh milioni nne, mshindi wa nne Sh milioni tatu, na mshindi wa tano atajipatia Sh milioni 2.4. Kwa mujibu wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, washindi wa sita hadi 10 kila mmoja atajipatia Sh milioni 1.4, na washindi wa 11 hadi 29 kila mmoja atajipatia Sh 700,000.
Watakaoshuhudia fainali ya shindano hilo katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam wanatarajia kupata burudani kutoka kwa wasanii wakiwemo wa bendi ya FM Academia 'Wana Ngwasuma', kundi la Tanzania House of Talents(THT), Ali Kiba, Malo, Dogo Mfaume, Fid Q, na Profesa J.
Mwanamuziki nyota, Koffie Olomide , pia anatarajiwa kukonga nyoyo za watakaokuwa ukumbini na wale watakaoshuhudia kwenye televisheni.

Thursday, October 1, 2009

Majaji wa Miss Tanzania 2009

Bobby Collymoi wa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, Susan Mungy wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Doris Malulu, wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) na Preshant Patel kutoka Kamati ya Miss Tanzania.

Wengine ni Devotha Mdachi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), rubani wa ndege za shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Sadik Muze,Lusekelo Mwakalukwa wa
Tanzanite One, Benard Mlunya wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,na Stella Kariuki wa kampuni ya Samsung.

Shindano la Miss Tanzania 2009 litafanyika kesho kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Nukuu ya leo

"Wananchi walikuwa na sauti katika kuongoza nchi, leo matajiri ndio wenye sauti. Viongozi wako karibu na matajiri, zamani ukiwa serikalini lazima utunze siri za serikali, leo siri zinavuja sana, watu wanaona yanayotendeka, wengine wanalipwa milioni tano na marupurupu, wengine wanaambulia laki moja, ndio maana sasa kuna migomo ya walimu, wanafunzi na wananchi," Joseph Warioba.

Ni kweli?

KUNA mdau kanitumia hii, duh!
KAMA madege yanavyotua na kuondoka ndivyo mawazo kuhusu sex huja yenyewe kwa mwanaume! Binadamu hawezi kuwa amekamilika akiwa kimwili na kiroho peke yake bila hisia (emotions).

Pia kuna tofauti kubwa sana namna mwanamke na mwanaume wanavyoweza kufanyia kazi emotions kwenye ubongo.

Bila kufahamu tofauti hizi kati ya mwanaume na mwanamke wakati mwingine husababisha suala la mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume kuwa na matatizo hasa kutokana na upande mwingine kushindwa kuelewa mwenzake anahitaji nini au kitu gani na wakati gani.

Linapokuja suala la emotions mwanamke ana uwanja mkubwa sawa na barabara yenye uwezo wa kupitisha magari 8 kwa wakati mmoja (eight lanes superhighway)
wakati mwanaume ni sawa na barabara moja ya kwenda kijijini kiasi kwamba magari hata mawili kupishana ni kasheshe.

Hii ina maana kwamba, kumkumbatia mwanamke huweza kumpa raha na msisimko wa ajabu kihisia, na ukimsikiliza akiongea humpa raha na kumpa ahuaeni kuliko kawaida.

Wakati mwanaume kuongea sana bila kutoa point kwa maneno machache anaona unampotezea muda wake.

Pia mwanamke huweza kukumbuka kutukanwa, au kupigwa na anaweza kukumbuka rangi ya chumba mlichokuwa wakati wa hilo vagi, shati mwanaume ulivaa, sura yako wakati mnapigana au kutukanana na siku, mwezi na mwaka kwa kuwa inahusishwa moja kwa moja na hisia zake kwenye hiyo super highway.
Mwanaume anaweza akawa baadhi ya vitu hakumbuki, na ikumbukwe kwamba wanawake hupenda kuongea kuhusu hisia zao all the time.

Linapokuja suala la kuwaza kuhusu sex basi mwanaume huweza kuwaza kuhusu sex kila baada ya dakika mbili na mwanamke huweza kuwaza sex wengine ni siku kadhaa katika mwezi.

Je, ndo kusema mwanaume muda wote yupo kwenye foreplay na ndiyo maana huwa na dakika chake akikutana na mwanamke na kutaka kwenda south pole moja kwa moja kuchimba gold hata kabla mgodi haujawa tayari!

Kuingia na kutoka kwa mawazo kuhusu sex kwa mwanaume ni sawa na ndege zinavyoingia na kutoka katika International Airport kama vile Amsterdam, au London Heathrow na mwanamake ni kama kiwanja cha ndege kule Nduli - Iringa kiasi kwamba wakati mwingi ndege hata zikifika zinaweza zisitue hadi hali ya hewa iwe nzuri (hadi mwanamke akaribie kuwa fertile)

Hii ina maana kwa mwanaume mawazo kuhusu sex hutua kwa wingi kama madege makubwa kila baada ya dakika mbili (kutua na kuondoka) na mwanamke ni sawa na kiwanja kidogo ambapo ndege ndogo za mawazo ya sex (tena private jet) hutua kwa mwezi angalau siku chache tu au kwa siku mara moja.
Kwa mwanamke foreplay ni saa 24 kabla ya sex, wakati mwanaume foreplay ni dakika 3 kabla ya sex.
Hapa bila mwanaume kufahamu tofauti iliyopo na mwanamke mahusiano ya mapenzi huweza kuwa ya kuumiza au kutimiza wajibu tu.

Ndiyo maana linapokuja suala la kutaka sex mwanaume ndiye mara nyingi hulianzisha, ingawa hii haina maana kwamba mwanamke kama anataka sex kwa mumewe asubiri mume aanze. Wanaume hupenda kutafakari kuhusu sex all the time.
Mengineyo!

Data zinaonesha kwamba wanawake wengi huvutiwa na wanaume ambao wamewazidi umri zaidi ya miaka miwili na kuendelea,wanaume ambao ni warefu kidogo kuliko wanamke wenyewe ingawa wanawake wakiulizwa huwa wanaruka kimanga.

Pia wanawake wengi huvutiwa na mwanaume kwa sababu ya ukubwa wa wallet yake na reputation au status aliyonayo katika jamii na si sura, size, rangi au kitu chochote kwenye mwili wake.