MFANYABIASHARA maarufu nchini, Idd Simba, amesema, lugha ya kiingereza imesababisha Tanzania iwe na sheria mbaya za madini.
Mbunge huyo wa zamani wa Ilala, Dar es Salaam amesema,anaona aibu kwa kuwa alishiriki kupitisha sheria mbaya za madini zinazotumika kuinyonya nchi.
Mwanasiasa huyo amedai kuwa,chanzo cha ubaya wa sheria hizo ni lugha ya kiingereza kwa kuwa zimeandikwa kwa lugha hiyo lakini idadi kubwa ya wabunge hawaielewi kwa ufasaha.
“Zile sheria ni mbaya na mimi naona aibu kwamba zilipitishwa wakati nikiwa kwenye lile Bunge, lakini unatarajia nini wakati sheria zile zinatungwa kwa Kiingereza,na si wabunge wengi wanaoelewa lugha hiyo,” amesema.
Akijibu maswali baada ya kuwasilisha mada kuhusu nafasi ya sekta binafsi kwenye utawala na maendeleo, Simba amesema,kwa kuwa sheria nyingi zimeandikwa kwa Kiingereza,mambo mengi yanapitishwa bungeni bila wabunge kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sheria husika.
“Huu ndio ukweli halisi na haya ni maoni yangu,” amesema Simba baada ya kuulizwa swali iweje sasa baada ya kukaa pembeni anaona namna sekta binafsi inavyonufaisha wageni zaidi kuliko wazawa, hasa kwenye sekta ya madini wakati sheria zilipitishwa naye akiwa Mbunge.
No comments:
Post a Comment