MKAZI wa mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia,Mazen Abdul Jawad, alikamatwa baada ya kuhudhuria kipindi kinachoitwa "Red Line" kinachoandaliwa na televisheni ya LBC yenye makazi yake nchini Lebanon.
Katika kipindi hicho chenye watazamaji wengi nchini Saudia, Jawad alijisifu kwa namna alivyokuwa akifanya mapenzi na wanawake mbali mbali.
Alijisifu pia kuwa alianza kufanya mapenzi tangu alipokuwa na umri wa miaka 14.
Kipindi hicho kilirushwa hewani julai 15 mwaka huu na kusababisha hasira miongoni mwa wananchi wa Saudi Arabia.
Takribani watu 200 walifungua mashitaka ya malalamiko dhidi ya Abdul Jawad, ambaye ni mfanyakazi wa shirika la ndege la Saudia.
Serikali ya Saudia iliamua kuchukua hatua kali kwa kuzifunga ofisi mbili za LBC nchini humo na kumkamata na kumfungulia mashitaka Abdul-Jawad.
Kipindi hicho kilianza kwa kumuonyesha Abdul-Jawad, akielezea namna alivyomla uroda jirani yake wakati huo akiwa na umri wa miaka 14.
Baada ya hapo aliwaongoza watazamaji kwenye chumba chake ambacho takribani vitu vyote ni vya rangi nyekundu na aliwaonyesha pia wanasesere wake kwa ajili ya ngono.
Baada ya hapo alijiunga na wanaume wengine watatu na kuanza kujadiliana masuala ya ngono.
Mahakama ya nchini Saudia ilimuona Abdul-Jawad ana hatia na ilimhukumu kwenda jela miaka mitano pamoja na kuchapwa jumla ya bakora 1,000.
Mbali na adhabu hizo, mahakama imeamuru kuwa,Abdul-Jawad,asisafiri kwa miaka mitano baada ya kutoka jela.
Kwa mujibu wa amri hiyo,hataruhusiwa kuongea na vyombo vya habari kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kumaliza kifungo chake.
Mwanasheria wake alitangaza kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.
alidai kwamba,Abdul-Jawad alikuwa akielezea maisha ya mapenzi ya watu wengine.
Mwanasheria huyo alidai kwamba televisheni ya LBC ilikuwa ikimrekodi mazungumzo yake bila kufahamu kwamba alikuwa anarekodiwa.
Wanaume wengine watatu ambao walichangia mawazo yao katika mjadala wa mapenzi wa Abdul-Jawad walipatikana na hatia ya kujadili masuala ya mapenzi hadharani na walihukumiwa kwenda jela miaka miwili na kuchapwa bakora
300 kila mmoja.
No comments:
Post a Comment