Monday, October 19, 2009

Katoa mimba 15 katika miaka 17

IRENE Vilar wa Colorado, Marekani alishika ujauzito mara 15 katika kipindi cha miaka 17 lakini alizotoa zote kabla hazijawa kubwa.
Anasema,alifanya hivyo si kwa sababu alikuwa na matatizo ya kiafya,mumewe hakutaka mtoto na hakutaka waachane kwa sababu hiyo.
Kwa sasa mwanamke huyo ana umri wa miaka 40, ameandika kitabu kilichosababisha malalamiko nchini Marekani kiasi cha kusababisha watu wengine wamtumie ujumbe wa kumtishia maisha yake.
Baadhi ya watu wanashinikiza Irene afungwe jela kwa vichanga 15 alivyovikatisha maisha yao.

Irene alianza safari yake ya 'kuzipanchi' mimba alipokuwa na umri wa miaka 16 akaimaliza alipofikisha umri wa miaka 33.

Ana watoto wawili Loretta, 5, na Lolita, 3, katika kitabu hicho ameeleza namna alivyotoa mimba hizo 15.
Kitabu hicho kinaitwa "Impossible Motherhood: Testimony of an Abortion Addict".

Irene alikubaliwa kuingia chuo kikuu cha New York University akiwa na umri mdogo wa miaka 15 na hapo ndipo alipoanza mapenzi na mwalimu wake wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 50 na baadae kuoana naye mwaka
uliofuatia.

Irene anasema, mwalimu wake huyo ambaye alikuwa ni profesa wa masuala ya lugha, alikuwa hataki kuzaa naye mtoto kwa kile alichodai kwamba uhusiano wake wa kimapenzi huwa hauzidi miaka mitano na kupata mtoto kungeharibu uhusiano wao.

Irene alikuwa akitumia vidonge vya kuzuia mimba mara chache sana na wakati alipoacha kutumia vidonge hivyo na kupata mimba, alikuwa akizitoa mimba hizo.
Irene anadai kwamba alikuwa akizitoa mimba hizo ili kuepuka asije akakimbiwa na mumewe huyo lakini baadae alitokea kupenda kutoa mimba.

Hata hivyo Irene alikataa kusema kama mumewe alikuwa na taarifa yoyote ya tabia yake ya utoaji mimba.

No comments:

Post a Comment