Thursday, October 15, 2009

Maswali kabla ya kuoa/kuolewa

KABLA ya kutamka “Hadi kifo kitakapotutenganisha”, au hata kabla ya kukubali kuvishwa pete ya engagement kuna maswali muhimu sana (hard questions) ambayo unahitaji kujiuliza.

Ukijiuliza maswali hayo unaweza kufahamu success au failure ya mahusiano ya ndoa pengine hata kabla ndoa haijafika popote.

Kujiuliza mwenyewe na kumuuliza yule unayatarajia kuoana naye itakusaidia kufahamu kama umempata mtu sahihi na pia kuweza kuondoa matatizo ya kawaida ambayo wengi hupelekea kuachana.

Chukua muda (honestly) kufanya evaluation ya namna unavyojisikia (feelings) na motivations kwa ajili ya wewe kuoa au kuolewa.

Ni vizuri kupata majibu ya maswali kabla hujaoana naye ili kuweza kushughulikia matatizo hayo kabla ya ndoa kuanza.

Kuna maeneo muhimu sana katika ndoa ambayo bila kuyafahamu na kuingia kichwa kichwa hakuna wa kumlilia isipokuwa wewe mwenyewe.

Suala la ndoa ni sensitive sana,ukishindwa acha utapata alama utakayoibeba maisha yako yote hapa duniani na pia unaweza kuathiri maisha ya wengine.

Swali la kwanza

Je, ni kweli tunapendana?
Je, ni kweli nitaendelea kumpenda hata miaka 30 ijayo?
Ni kitu gani au sifa zipi zinanifanya nimpende?
Uwe mkweli unapoyajibu haya maswali.

Unahitaji kufahamu na kujisikia ni kweli unampenda mwenzako isije kuwa ni tamaa tu.

Upendo huanza kidogokidogo na hutokea kwa kumpenda mtu mzima kama alivyo, awe ana pesa au la na pia si kumpenda kama wewe unavyotaka awe.

Kumbuka mke au mume si kipande cha udongo wa mfinyanzi kwamba utamefinyanga kwa kadri unavyotaka wewe.
Swali la pili:
Kwa nini tunaoana?
Kwa nini namhitaji kuoana naye?
Ni kwa sababu ninataka mtoto?
Ni kwa sababu ninataka hela zake au najisikia upweke upweke, au nataka sex au nataka kuondokana na kero za mama au wazazi?

Au naona nachelewa kuolewa/kuoa? au rafiki zangu wananisema sana au na mimi nionekane nimeoa au kuolewa?
Kuoa au kuolewa kwa sababu za ajabu ajabu huweza kukufikisha mahali ambapo utajikuta upo disappointed, frustrated na hatimaye kuachana.

Oa au olewa kwa sababu ni wakati wake na umwe umeamua wewe.
Swali la tatu:

Ni nini matarajio ya ndoa yangu?

Umejiandaa kuwa mume/ mke?
Umejiandaa kuwa baba/mama?
Upo tayari kuvumilia changamoto za ndoa?

Matarajio ya mtu anapoamua kuingia kwenye ndoa huweza kujenga au kuharibu ndoa.

Kuna baadhi ya imani potofu kuhusu ndoa,unatakiwa kuzifahamu hata kabla hujaingia kwenye ndoa. Kuamini kwamba ukiolewa basi mwenzako anatakiwa kukufanya happy si kweli, furaha unayo wewe kwanza.

Kufikiria kwamba eti mume/mke ataweza kusoma akili yako si kweli, unahitaji kueleza kile unachotaka na si kubaki kimya eti anajua.

Kuamini kwamba ukioa au kuolewa basi kila kitu mtafanya pamoja si kweli, kila mtu ana interest zake.

Na kutaka kuwa na ndoa unayotaka wewe badala ya wote kwa pamoja unaweza kujikuta kwenye total disappointment. "Truly loving another means letting go of all expectations.

It means full acceptance, even celebration of another's personhood."

No comments:

Post a Comment