Mtoto Dong Dong wa nchini China ana umri wa miaka MINNE, kawashangaza watu wengi kwa tabia yake ya kunywa pombe na kuvuta sigara kupita kiasi.
Picha ya mtoto huyo akivuta sigara ilitolewa kwenye gazeti la Jianghuai Morning Post.
Gazeti hilo limesema, mtoto huyo alianza kuvuta sigara tangu alipokuwa na umri wa miaka miwili.
Dong Dong anaishi na bibi na babu yake kwenye kijiji cha Banqiao katika mji wa Anhui nchini China.
Bibi yake ambaye ana duka la chakula, sigara na bidhaa mbali mbali kwenye kijiji hicho, alielezea tabia ya mtoto huyo kuiba sigara kwenye duka lake.
"Wakati anapohitaji sigara huchukua toka nyumbani au huiba paketi ya sigara kwenye duka langu".
Bibi yake aliendelea kusema, mbali na tabia yake ya kuvuta sigara iliyopindukia Dong Dong pia hunywa sana pombe.
Daktari Zhang Gong, toka hospitali ya watoto ya mji huo, alielezea kushangazwa sana na jinsi mtoto huyo anavyovuta sigara na kutoa moshi kama gari moshi.
"Kwa jinsi anavyovuta sigara, anaonekana ni mzoefu sana na ana historia ndefu ya kuvuta sigara ingawa umri wake ni mdogo", alisema Dr Zhang.
Dong Dong ni mmoja kati ya watu milioni 350 wanaovuta sigara nchini China.
Idadi hiyo ya wavutaji sigara China ni kubwa kuliko nchi yoyote duniani.
Kwa mujibu wa tovuti ya TobaccoChina.net , asilimia 60 ya wanaume wa nchini China wenye umri wa kuanzia miaka 15 wanavuta sigara mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment