Wednesday, December 16, 2009

Na watoto wa 'kiswahili' ruksa?

Kashfa za ngono zinavyomtesa Tiger Woods


Mke wa Tiger Woods, Elin








Tiger Woods,mkewe, Elin, wakiwa na mtoto wao, Sam.

Nyota huyo wa gofu yupo kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuamua kupumzika kucheza mchezo huo ili kuweka sawa mambo ya familia yake.

Anadaiwa 'kujirusha' na wanawake kibao, amekiri.

Kampuni kadhaa ziilizokuwa zikimdhamini zimetangaza kusitisha udhamini wao, na nyingine zimepunguza kiwango cha udhamini wao.

Berlusconi alivyoshambuliwa

Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi, akivuja damu baada ya kushambuliwa.
Mtu aliyekuwa na chuma akimshambulia Berlusconi
Wasaidizi wa Berlusconi wakimsaidia baada ya kushambuliwa
Wanausalama wakimdhibiti mwanaume aliyemshabulia Berlusconi (Mwenye track yenye mstari mweupe)

Kuna taarifa kwamba Berlusconi amepasuaka pua na pia amepoteza meno mawili

Ni utoto, wakikua wataacha

Friday, December 11, 2009

Msaidizi wa balozi mbaroni Dar

POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamemkamata Katibu Muhtasi wa Ubalozi wa Canada, Jean Touchatte (48) kwa tuhuma za kuwatemea mate askari wa Usalama barabarani na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .
Touchatte anatuhumiwa kumshambulia askari wa usalama barabarani aliyekuwa akiongoza magari katika eneo la Banana wilaya ya Ilala.
Kaimu kamanda wa kanda hiyo, Charles Kenyela, amesema, mtumishi huyo wa ubalozi anadaiwa kufanya makosa hayo Desemba 9 saa 8.45 mchana wakati askari huyo namba E 1653, Koplo Samson akiwa kazini maeneo hayo.
Kwa mujibu wa Kenyela, wakati akiendelea kuyaruhusu magari yanayotokea Ukonga kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Touchatte alifika eneo hilo akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 17 CD 178 Toyota Land Cruiser Prado mali ya Ubalozi wa Canada.
Amesema, mtuhumiwa huyo alikuwa anatoka Ukonga kwenda uwanja wa ndege, ghafla alipunguza mwendo, akafungua kioo cha gari lake na kumtemea mate askari huyo.
Kenyela amedai kuwa,kitendo hicho kiliwashangaza wengi walioshuhudia,na kwamba sababu ya kufanya hivyo haikufahamika, hivyo polisi wa doria walipewa taarifa ili kulifuatilia gari hilo.
“Askari wetu walianza kufuatilia kwa nyuma gari hilo na walipofika barabara ya Nyerere karibu na Kamata gari hilo lilikamatwa na kupelekwa moja kwa moja hadi makao makuu ya polisi Trafic Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuwekwa chini ya ulinzi” amesema.
Kwa mujibu wa Kenyela, wakati mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa,waandishi wa habari akiwemo Jerry Muro(29) wa TBC walifika kituoni hapo, wakitaka kufahamu nini kilichotokea ndipo mtuhumiwa huyo akamtemea mate sehemu ya chini ya kidevu chake na kusambaa katika flana aliyokuwa amevaa.
Muro alifungua jalada la shambulio CD/IR/4818/2009, na kwa mujibu wa Kenyela, mtuhumiw alipohojiwa hakuwa tayari kujibu wala kutoa maelezo yake kwa madai kwamba mpaka balozi wake awepo.

Gerrard na wanawe uwanjani

Kiungo wa Kimataifa wa Liverpool na timu ya soka ya England, Stephen Gerrard, akiwa na wanawe, Lexie na Lilly, kabla ya mpambano wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kati ya Liverpool na Fiorentina ya Italia.
Like father, like Daughters


Mke wa Gerrard, Alex Curan, naye alikuwepo Anfield kumsupport mumewe.

Married But Available

SIFAHAMU zamani ilikuwaje, ila kwa sasa si jambo la ajabu kwa mwanamke au msichana 'kutembea' na mume wa mtu.
Wanawake wamewabatiza wanaume hawa jina la MBA-Married But Available.

"Wezi' hawa wa waume za watu wametoa sifa kibao kwa 'ma sweet heart' wao wakidai kuwa MBAs wana vitu ambavyo bachellors wengi hawana.

Miongoni mwa sifa hizo ni

1. Wana-care kuliko bachellors a.k.a Living Singles
2. They take you seriously than bachelors and most of all
3. They happen to have mature advice to these ladies problems than the bachelor ones.
4. Wanakupa uhuru wako-huulizwi where have you been or why are you late? e.t.c

Penzi shata shata

Mjibu mtoto

Thursday, December 10, 2009

Kumaliza hang-over

KICHWA kinagonga, unaona kizunguzungu, mwili hauna nguvu, unasikia kichefuchefu, kama unataka kutapika lakini hutapiki, kwa kifupi unajisikia hovyo kwa sababu ya unywaji wa kupindukia jana! Hali hii inaitwa HANG-OVER au uchovu.

Ingawa hatupendi kuelezwa ukweli au kufikiria madhara ya pombe, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa pombe ni dawa ya kulevya.
Ina dhoofisha mwili na pale mtu anapokunywa kupita kiwango, mwili hujawa na sumu.

Unapokutana na hali hiyo, mwili hujaribu kujinasua kama vile ambavyo kitu chochote kingefanya kinapovamiwa na kitu kigeni.

Njia bora ya kuondokana na uchovu (hangover) ni kunywa kiasi au kuacha kabisa ulevi.
Kama utashindwa kujizuia kunywa na unataka kujiepusha na uchovu asubuhi, ni vyema ukila vitu vifuatavyo ambavyo vinaweza kukusaidia:

1. NDIZI MBIVU

Unapozidiwa na kilevi, kiasi kikubwa cha madini ya potasiamu hupotea, hivyo kwa kula ndizi mbivu ambazo zinaaminika kuwa na kiwango kikubwa cha madini hayo, kutakusaidia kupunguza makali ya hang-over.
Unachotakiwa kufanya ni kutafuta ndizi mbivu nzuri, menya na kula kwa wingi.

2. TANGAWIZI

Tangawizi mbichi imekuwa ikitumika kwa muda mrefu kutibu magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya kusikia kichefuchefu na mafua.

Andaa juisi ya tangawizi mbichi na kunywa kama ilivyo, au unaweza kuandaa kwa kukata vipande kati ya 10 hadi 12 na uchanganye na vikombe 4 vya maji. Chemsha kwa dakika 10, epua na chuja.

Changanya na juisi ya chungwa moja, kipande cha limau na nusu kikombe cha asali.
Kunywa mchanganyiko huo utapata nafuu mara moja.

3. ASALI NA LIMAU
Asali na limau ni kinywaji bora kuliko vyote katika tiba hii, ni rahisi kutengeneza na kunywa.

Kinarudisha haraka kiasi cha sukari na maji kilichopotea wakati wa kunywa kilevi.

Chemsha maji kiasi cha kikombe kimoja, changanya limau na asali kupata ladha unayoitaka.

Ni bora kutumia asali ili kupata sukari ya asili, badala ya kutumia sukari ya kawaida.

Ili kupata ahueni, kunywa mchanganyiko huo mara kadhaa kwa siku.
4. SUPU, WALI

Mtu anapoanza kupata nafuu kutokana na uchovu, chakula huwa kitu cha mwisho kabisa kutamani kula, lakini pamoja na kutojisikia hamu ya kula, unahitaji kula ili mwili upate nguvu.

Unashauriwa kuanza kwa kula vyakula vyepesi kama vile wali mweupe, supu, n.k
5. KINYWAJI MAALUM

Kunywa pia vinywaji maalum vinavyotumiwa na wanamichezo kwa lengo la kurejesha nguvu na madini yaliyopotea mwilini.

Unaweza pia kunywa vinywaji vya kutia nguvu mwili (energy drink) kama vile, Red Bull, Shark, Malta Guiness, n.k
6. BARAFU

Ili kutuliza maumivu ya kichwa, chukua vipande vya barafu, weka kwenye mfuko wa plastiki ambao utazungurusha kwenye kitaulo na kuweka kwenye kipaji chako cha uso kinachogonga.
7. JUISI

Juisi, hasa fresh ya machungwa, husaidia kupandisha kiwango cha sukari kilichopotea na husaidia kuondoa dalili za uchovu mwilini.

Hata hivyo, kama tumbo lako limechafuka sana, kunywa juisi ya epo (tufaha) badala ya machungwa ambayo ina asidi.

8. MAJI
Mbali ya muda, maji ni tiba bora ya uchovu.
Upungufu wa maji unaotokana na kunywa kiasi kingi cha kilevi ndiyo unaoleta kasheshe mwilini. Kunywa maji mengi wakati wote wa mchana, siyo chini ya glasi nane kwa siku.

DONDOO MUHIMU

Ili kujiepusha na ‘hang-over’ asubuhi baada ya kunywa kupita kiasi, kunywa maji mengi sana kabla ya kupanda kitandani.

Au kunywa taratibu, kinywaji kimoja kila baada ya saa moja kwani huo ndiyo muda unaotumika na kinywaji kusambaa mwilini na kutoweka

Mambo ya Shakira







Aliyechoma moto uume wa mumewe kizimbani

Mwanamke nchini Australia aliyeuchoma moto uume wa mumewe alidaiwa 'kutembea nje ya ndoa' atapandishwa tena kizimbani Januari mwakani kujitetea kuhusiana na mauaji ya mumewe.

Mwanamke huyo, Rajini Narayan(44) alipandishwa kizimbani Ijumaa iliyopita akikabiliwa na mashitaka ya mauaji, kusababisha moto, na kuhatarisha maisha ya watu.

Rajini ni mama wa watoto watatu, alizichoma moto sehemu nyeti za mumewe Satish Narayan, mwezi Desemba mwaka jana baada ya kumvizia akiwa amelala aliporudi toka kwenye ulevi.

Satish alipata majeraha makubwa sana katika sehemu zake za siri na alifariki dunia wiki chache baada ya tukio hilo.

Moto ulioziteketeza sehemu za siri za mumewe uliiteketeza pia nyumba ya familia yao na kusababisha hasara ya dola milioni moja.

Katika vikao vilivyopita vya mahakama, majirani wa Rajini waliiambia mahakama kuwa Rajini aliwaambia "Mimi ni mke mwenye wivu sana, uume wake ni mali yangu na niliamua kuuchoma moto ili mtu mwingine yoyote asiupate".

Rajini aliwaambia pia majirani zake kuwa hakutarajia nyumba yao ingeteketea kwa moto huo.

Haya hayawezekani Kigamboni?

No, no, please!

Ungekuwa wewe ungefanya nini?

Wednesday, December 2, 2009

Mfungwa atunukiwa shahada ya sheria

MKUU wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT),Dk John Malecela, amemtunuku mfungwa,Semayoga Ernest,Shahada ya Sheria.

Mfungwa huyo anayetarajia kumaliza kifungo Agosti mwakani ameiomba Serikali iwasamehe wafungwa waliojirekebisha.

Ameyasema hayo katika mahafali ya pili ya 21 yaliyofanyika jana katika Ukumbi wa KM, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Ernest anatumikia kifungo cha miaka 10 katika gereza la Ukonga,Dar es Salaam,ana ndoto za kujiunga kwa shahada ya uzamili ya sheria.

Alifungwa baada ya kukamatwa akifanya biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Malaysia mwaka 1999.

Ernest amesema,aliamua kusoma sheria ili kusaidia wafungwa kwa kuwa hawafahamu haki na taratibu za kuwasaidia kuandaa rufaa zao.

Wanafunzi wafanya ngono hadharani

WANAFUNZI wawili nchini Australia wamegeuka gumzo la mji wa Sydney kwa kufanya mapenzi kwenye mnara wa saa wa mji huo mchana wakiamini kuwa hawaonekani.

Wapenzi hao waliwashangaza wapita njia kwa kuendelea kufanya mapenzi mchana kwenye mnara wa saa wa jiji la Sydney.

Kwa mujibu wa gazeti la daily Telegraph, watu walianza kukusanyika chini ya mnara wa jengo hilo ambalo limegeuzwa kuwa hosteli ya wanafunzi wa chuo kikuu.

Mmoja wa watu walioshuhudia sinema hiyo ya kikubwa ya bure aliwapiga picha wanafunzi hao walioendelea kufanya mapenzi bila kujali kama watu wanawaona au la.

"Awali ni watu wachache sana ndio waliofanikiwa kuwaona wapenzi hao, nilipoanza kuwapiga picha watu walianza kukusanyika wakionyeshana huku wakicheka", alisema shuhuda wa tukio alipokuwa akiongea na gazeti la Daily Telegraph la Australia.

"Kwa jinsi ilivyokuwa ikionekana, walikuwa hawajui kuwa watu wanawaangalia".
Inasemekana kuwa wapenzi hao ni wanafunzi wanaoishi kwenye jengo hilo na walidhamiria kufanya mapenzi kwenye paa la jengo hilo.

Jengo waliloamua kumalizia haja zao za kimapenzi ni mojawapo ya majengo machache ya kihistoria, lilijengwa mwaka 1923 na kutumika kama shopping mall kabla ya kugeuzwa kuwa hosteli miaka ya hivi karibuni.

Jeniffer Lopez 'akikamua' jukwaani





MWANAMUZIKI na muigizaji maarufu, Jeniffer Lopez, akifanya vitu vyake jukwaani wakati wa hafla ya tuzo za muziki za Marekani 2009, jijini Loe Angeles, California nchini Marekani.