Wednesday, December 2, 2009

Wanafunzi wafanya ngono hadharani

WANAFUNZI wawili nchini Australia wamegeuka gumzo la mji wa Sydney kwa kufanya mapenzi kwenye mnara wa saa wa mji huo mchana wakiamini kuwa hawaonekani.

Wapenzi hao waliwashangaza wapita njia kwa kuendelea kufanya mapenzi mchana kwenye mnara wa saa wa jiji la Sydney.

Kwa mujibu wa gazeti la daily Telegraph, watu walianza kukusanyika chini ya mnara wa jengo hilo ambalo limegeuzwa kuwa hosteli ya wanafunzi wa chuo kikuu.

Mmoja wa watu walioshuhudia sinema hiyo ya kikubwa ya bure aliwapiga picha wanafunzi hao walioendelea kufanya mapenzi bila kujali kama watu wanawaona au la.

"Awali ni watu wachache sana ndio waliofanikiwa kuwaona wapenzi hao, nilipoanza kuwapiga picha watu walianza kukusanyika wakionyeshana huku wakicheka", alisema shuhuda wa tukio alipokuwa akiongea na gazeti la Daily Telegraph la Australia.

"Kwa jinsi ilivyokuwa ikionekana, walikuwa hawajui kuwa watu wanawaangalia".
Inasemekana kuwa wapenzi hao ni wanafunzi wanaoishi kwenye jengo hilo na walidhamiria kufanya mapenzi kwenye paa la jengo hilo.

Jengo waliloamua kumalizia haja zao za kimapenzi ni mojawapo ya majengo machache ya kihistoria, lilijengwa mwaka 1923 na kutumika kama shopping mall kabla ya kugeuzwa kuwa hosteli miaka ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment