Thursday, December 10, 2009

Aliyechoma moto uume wa mumewe kizimbani

Mwanamke nchini Australia aliyeuchoma moto uume wa mumewe alidaiwa 'kutembea nje ya ndoa' atapandishwa tena kizimbani Januari mwakani kujitetea kuhusiana na mauaji ya mumewe.

Mwanamke huyo, Rajini Narayan(44) alipandishwa kizimbani Ijumaa iliyopita akikabiliwa na mashitaka ya mauaji, kusababisha moto, na kuhatarisha maisha ya watu.

Rajini ni mama wa watoto watatu, alizichoma moto sehemu nyeti za mumewe Satish Narayan, mwezi Desemba mwaka jana baada ya kumvizia akiwa amelala aliporudi toka kwenye ulevi.

Satish alipata majeraha makubwa sana katika sehemu zake za siri na alifariki dunia wiki chache baada ya tukio hilo.

Moto ulioziteketeza sehemu za siri za mumewe uliiteketeza pia nyumba ya familia yao na kusababisha hasara ya dola milioni moja.

Katika vikao vilivyopita vya mahakama, majirani wa Rajini waliiambia mahakama kuwa Rajini aliwaambia "Mimi ni mke mwenye wivu sana, uume wake ni mali yangu na niliamua kuuchoma moto ili mtu mwingine yoyote asiupate".

Rajini aliwaambia pia majirani zake kuwa hakutarajia nyumba yao ingeteketea kwa moto huo.

No comments:

Post a Comment