Friday, July 31, 2009

Majambazi yapora NMB

MUDA mfupi uliopita nimepata taarifa zinazodai kuwa majambazi yamepora fedha katika benki ya NMB tawi la Temeke mkoani Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, majambazi hayo yameua polisi waliokuwa wakilinda katika benki hiyo.
Taarifa zaidi baadaye

Thursday, July 30, 2009

Kwa Madonna 'age's nothing'




PICHANI hapo juu ni mwanamuziki maarufu Lady Madonna akilishambulia jukwaa Julai 13 mwaka huu jijini Madrid, Hispania.
Msanii aliyeasili watoto wawili waafrika, Banda na Mercy alikwenda na mpenzi wake mpya Jesus Hispania kwa ajili ya onyesho hilo kwenye uwanja wa Vicente Calderon.

Nukuu ya leo

Migomo si suluhisho la matatizo yetu, si suluhisho hata kidogo, hatujapuuza hata kidogo kushughulikia matatizo yao ya fedha" Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, bungeni Dodoma Julai 16, 2009.

Mtaani kwetu

Dawa na mwanaume mwanaume mwenzie

Wednesday, July 29, 2009

TBL yanusurika kuungua

KIWANDA cha bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) cha Ilala, Dar es Salaam kimenusurika kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
Kuna taarifa kwamba moto umeunguza eneo la kuhifadhi ma-kreti ya bia.
Chanzo bado hakijafahamika ila inadaiwa kuwa transfoma ililipuka.

Tuesday, July 28, 2009

Mwakyembe ajitoa mhanga

Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameitaka Serikali iufunge mara moja mgodi wa dhahabu wa North Mara ili sumu inayodaiwa kutoka hapo isiendelee kuwadhuru wananchi.

Mbunge huyo pia ametaka mgodi wa dhahabu wa Geita ufungwe kwa sababu, kwa muda mrefu umekuwa ukitoa kemikali za sumu zinazowadhuru wananchi wa kijiji cha Nyakabale.

“Kwa nini tuogope wawekezaji kama mama mkwe?” amehoji Mwakyembe na pia kuuuliza kwa nini vifungu vya mikataba havitumiki kuwabana wawekezaji.

Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa mgodi wa North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara umekuwa ikimwaga maji yenye sumu katika mto Tigithe.

Kwa mujibu wa madai hayo, wananchi 21 kati waliyotumia maji hayo wamefariki dunia, wengine wamekumbwa na matatizo ya kiafya, na pia mifugo 200 imepoteza maisha.

Kampuni inayomiliki mgodi huo imekanusha taarifa hizo kwa madai kuwa polisi kwa kushirikiana na mamlaka za Wilaya ya Tarime zimefanya uchunguzi na kubaini kuwa hakuna uthibitisho wa kuwapo kwa madhara hayo.

Dk Mwakyembe amesema, anafahamu kwamba, kampuni inayomiliki mgodi wa North Mara, Barrick Tanzania, ni kubwa zaidi kwa uzalishaji wa dhahabu duniani na ina nguvu kubwa na inaweza kukutesa lakini hawezi kukaa kimya wakati wananchi wanaathirika na lazima hatua zichukuliwe.

“Hii nchi ni yetu, tutaongea kwa ujasiri tu” Dk Mwakyembe amesema bungeni mjini Dodoma wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2009/2010.

Kapteni Komba amzimia Waziri Nagu

Dakika chache zilizopita Kapteni John Komba amesema bungeni kwamba Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Mary Nagu amependeza kuliko siku nyingine zote.
Mbunge huyo amesema, sifa hizo zimpe moyo Nagu wa kulinda viwanda vya Tanzania.
Kama haitoshi, Komba kasema waziri huyo ana sura nzuri na anauzika. makubwa!

Diet inamgharimu Rais Sarkozy?

Rais Sarkozy na mkewe, Carla Bruni wakifanya mazoezi ya kukimbia

Rais Nicholas Sarkozy akiwa na mkewe, Carla Bruni wakitoka hospitali jana baada ya kiongozi huyo wa Ufaransa kuruhusiwa kutoka hospitali jana.
Rais Huyo alilazwa baada ya kuugua wakati anafanya mazoezi ya kukimbia.
Inadaiwa kuwa tangu amuoe Carla Bruni mwaka jana, Rais Sarkozy amekuwa katika mkakati wa kupunguza mwili ili aendane na 'mamsap'
Wadadisi wa mambo wanasema, kiongozi huyo wa Ufaransa anafanya diet hivyo kama anataka kuwa fit lazima aongeze kipimo cha vyakula anavyotumia badala ya kupunguza.
Soma hapo chini
As president, he has to keep up with international affairs, domestic politics and the economic crisis. And then there's Carla.

So perhaps it's no surprise that friends of Nicolas Sarkozy say the gruelling fitness regime he
started soon after his wedding to model Carla Bruni was a disaster waiting to happen.

The 54-year-old French president looked pale and a little shaken as he left the Val-de-Grace Military Hospital in Paris with his wife yesterday.

Close friend and MP Patrick Balkany said: 'Recently the president has looked very honed. He looks more like a Tour de France rider.

'The president is going to have to take more care, work a little less hard and eat a little bit more.'Mr Sarkozy started dieting within a few days of his wedding to 41-year-old Miss Bruni last year.

She introduced him to a fitness instructor who told him to lose 9lb and two trouser sizes --a change which many would consider unhealthy for a man who stands a mere 5ft5ins.

Saturday, July 25, 2009

Gaetano afunga ndoa



MTANGAZAJI maarufu wa radio na televisheni nchini Uganda, Gaetano Juuko Kagwa kaoa.
Alhamisi ya wiki iliyopita kijana huyo maarufu pia Afrika alifunga pingu za maisha na Enid Keishamaza Rukikaire.
Wapenzi hao walifunga ndoa katika kanisa la Mtakatifu Francis la Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.
Watu wasiozidi 30 walishuhudia viapo vya Gaetano na Enid, na kwa ujumla ndoa na harusi vilikuwa siri kiasi kwamba, hata mapaparazi hawakuweza kunusa kilichokuwa kikiendelea.
Ingawa haijawekwa wazi, huenda hata kufungwa kwa ndoa hiyo Alhamisi Julai tisa badala ya Jumamosi Julai 11 ilikuwa ni mikakati ya kuvikwepa vyombo vya habari.
Harusi ya mtangazaji huyo na Enid haikuwa na shamrashamra zozote na waliifanya simple kuliko ilivyotarajiwa.

Friday, July 24, 2009

Adebayor asema ya moyoni


ALIYEKUWA mshambuliaji wa Arsenal ya Uingereza, Ammanuel Adebayor amesema, mashabiki wa timu hiyo ndiyo waliosababisha aihame klabu hiyo.

Raia huyo wa Togo kajiunga na safu ya ushambuliaji ya Manchester City akiwa na Carlos Tevez na Robinhno.
Amesema hakupenda namna mashabiki wa The Gunners walivyokuwa wanamfanyia na kumfuatafuata
Soma hapo chini

EMMANUEL ADEBAYOR last night hit out at Arsenal's fans and claimed: You made me leave.
The Togo striker could make his Manchester City debut here tomorrow after a £25million move.

And Adebayor revealed the decision to join City was made easier after the Gunners faithful turned on him.

He said: "The way the fans behaved towards me was not nice at all. I can't understand why they were after me. I did my best for them and I was very happy there.

"I scored 30 goals in a season - it's not my fault that Milan, Barcelona or Real Madrid wanted to sign me."

City manager Mark Hughes snapped up Adebayor last weekend. The star added: "In any summer, Barcelona try to sign Cesc Fabregas.
"But the fans never turned on him."

Wabunge washambuliana bungeni

Wabunge wawili leo wameshambuliana bungeni, mmoja kasema mwenzake anakera, mwingine kamtuhumu mwenzake kuwa ni muongo.
Wametuhumiana kwa nyakati tofauti wakati Bunge lilijadili bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka wa fedha 2009/10.

Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi, amesema, ndani ya Bunge kuna mambo yanakera na amewashutumu wabunge wanaozungumza bungeni bila kufanya utafiti kwanza.

Mporogomyi amesema wabunge wanapaswa kutoa hoja zenye mantiki ili wabunge wafaidike na si kutoa hoja zinazohusu ndugu zao.

Tuhuma alizotoa Mbunge wa Singida Kusini, Mohamed Missanga, jana zimemkera Mporogomyi na amesema kuwa, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) linafanya kazi vizuri.
Mporogomyi amesema, ataipinga hoja binafsi ya Missanga ya kutaka iundwe tume huru ya Bunge kuichunguza NECTA.

Missanga jana alisema, Katibu wa Baraza hilo, Dk Joyce Ndalichako ni tatizo katika chombo hicho cha Serikali hivyo aondolewe kwa kuwa amekuwa akiiongoza NECTA anavyotaka yeye ikiwa ni pamoja na kuwafukuza ovyo wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Missanga, tangu mwaka 2005, Dk Ndalichako amefukuza wafanyakazi 118 NECTA na ameajiri wa kwake 180, na amedai kuwa walioajiriwa wanatoka katika kabila lake ( la Dk Ndalichako).

Alihoji ni kwa nini Dk Ndalichako hajiuzulu kwa kuwa baraza hilo limekuwa na matatizo mengi yakiwamo ya kuvuja kwa mitihani.

Mporogomyi amesema, baraza limeajiri wafanyakazi 79 kutoka mikoa mbalimbali na si wenye asili ya Singida pekee. “Na mimi sidhani kama tunataka mgongano humu ndani” amesema.
Mbunge huyo amesema, analolizungumza ndilo analoliamini na limetoka moyoni mwake.

Leo mchana, Missanga ameomba muongozo wa Spika na kuhoji kama ni sahihi Mbunge kumjibu Mbunge mwenzake aliyechangia jambo bungeni.

Mbunge huyo amesema, mengi aliyoyasema Mporogomyi ni uongo na kusema, baadhi ya wabunge waliowahi kuwa mawaziri wanajisahau na kudhani kuwa bado kwenye madaraka hayo.

Naibu Spika wa Bunge, Anne Makinda, amemuagiza Missanga afuate utaratibu mwingine kueleza ukweli kuhusu aliyoyasema Mporogomyi.
Makinda amesema, wabunge wanapochangia bungeni wanapaswa kuzungumzia mambo kwa ujumla kwa kutoa hoja badala ya kuwajadili watu.

Thursday, July 23, 2009

Obama aomba radhi kwa kuvaa 'Mom Jeans'


RAIS Barack Obama wa Marekani amewaomba radhi wote waliomshutumu kwa kuvaa suruali waliyoiita ni MOM JEANS.
Rais huyo amesema, huwa hapendi kwenda madukani kuchagua nguo na aliona kuwa jeans hiyo ilimfaa na alikuwa comfortable.
Watu wamekuwa wakimshutumu Rais hiyo kwa kusema kuwa kitendo cha yeye kuvaa jeans hiyo kunamaanisha kwamba hana choice nzuri ya nguo.
Rais Obama alivaa nguo hiyo chapa Levi's alipokwenda kufungua mashindano ya MBL All Star kwenye uwanja wa Burch, St Louis, Missouri nchini humo.
Soma hapo chini alichokisema obama kujibu shutuma hizo
When asked about his choice of denim on NBC’s Today Show, Obama said, “I’m a little frumpy.
I hate to shop, those jeans are comfortable.
For those of you who want your president to look great in his tight jeans I’m sorry, I’m not the guy.”

Monday, July 20, 2009

Buriani Makubo

MWANDISHI wa habari, Haruni Makubo(45) anazikwa leo kijijini kwao, Mriba mkoani Mara.
Makubo alifariki dunia Ijumaa usiku, ameacha mjane na watoto wanne.
Waandishi wa habari mkoani Mara jana waliungana na mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa mwandishi huyo aliyekuwa akiishi Songambele mjini Tarime.
Mungu ailaze roho Makubo mahala pema peponi, AMEN.

Masikini Beckham

Ilikuwa ni mara ya kwanza kuichezea Gallax tangu atoke AC Milan
Bango likimtaka arudi kwao na atubu

NYOTA wa soka Uingereza, David Beckham yupo kwenye wakati mgumu nchini Marekani baada ya mashabiki wa timu ya Los Angeles Gallax kumzomea uwanjani, kumshambulia kwa maneno makali na kunusurika kupata kibano.
Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wanasema Beckham ni MSALITI na kumtaka arudi kwao Uingereza.
Beckham ana mkataba wa kuichezea timu hiyo lakini alikwenda kukipiga AC Milan ya Italia kwa mkopo na huenda atarudi huko.
Jana mwanasoka huyo alibwatukiana na mashabiki wa Gallax, akataka kuruka uzio akapambane nao lakini walinzi walimzuia.
Mashabiki mameponda kwa kusema, alichokifanya Beckham uwanjani ni ujinga kwa kuwa mtu wa daraja lake asingefanya hivyo.
Kila alipopata mpira walikuwa wanamzomea na kusema buuuuu
, mkewe, Victoria ameshuhudia hali hiyo.
Soma hapo chini
'We boo a lot of players - they don't come out and challenge our guys. We're just here as fans. A security guy got our guy and security held him back.

'He was like "Come here, come here, come here". He instigated that.

'We were a little upset. He betrayed our team but don't come calling out one of our fans, that doesn't happen.

'I don't think he wants to be here, I think he should go.'

Cheer squad: Tom leads a round of applause for his close friend David
Eric Lewis, 43, also from LA, said: 'He called the guy out. He called out a drunk fan.

'How stupid is that? He's the player, he's the professional.

'He should have kept himself under control and he didn't.

'He shouldn't have done that, it was dumb. The guy was inebriated, Beckham should have known that.

'For a player to call out a fan is ridiculous, it's stupid.'

He added: 'He says he's full of class and he's been playing with all the best teams in the world. That showed absolutely no class.

'He's already gone. We don't even have to make that choice.'

But Shawn Cervantez, 22, from Sacramento, said Beckham did not appear to be looking for a confrontation when he approached the fans.

She said: 'As soon as half time started he came over here and it appeared to me he was coming over here to make amends.

'He had his hand out to shake a hand and then one of the guys was giving him the middle finger and I guess they got aggressive with each other and the guy came over the wall and started to attack him.

'It was unbelievable, really.

'I think that their complaints are legitimate but I think that's a bit much.

'Their signs are asking him to prove to them that he's here and that they want him to ask for forgiveness.

Saturday, July 18, 2009

Papa afungwa POP

KIONGOZI wa Kanisa katoliki duniani, Papa Benedict XVI amefanyiwa operesheni katika mkono wa kulia kurekebisha mfupa uliovunjika.
Papa alianguka chumbani usiku wa kuamkia jana, alipelekwa hospitali saa nne asubuhi jana na akaruhusiwa saa sita baadaye.
Kiongozi huyo alitoka hospitali akionyesha kuwa mwenye afya njema, aliwapungia watu kwa mkono wa kushoto na wakati fulani alionyesha kwamba ni kwa nini aliwasalimu kwa mkono huo.
Papa amefungwa POP, inatarajiwa kutolewa baada ya mwezi mmoja.

Friday, July 17, 2009

Tevez analitaka jumba la Ronaldo





Christiano Ronaldo(24) anauza jumba lake la kifahari lililopo kwenye eneo la vibopa, Cheshire nchini Uingereza.
Nyota huyo wa soka duniani anataka Paundi milioni tano ili aliachie jumba hilo lenye kila kitu unachoweza kukihitaji kwenye nyumba vikiwamo vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea, sauna na jakuzi.
Ronaldo alilinua paundi milioni nne miezi 18 iliyopita, aliyekuwa mchezaji mwenza Man United, Carlos Tevez kaonesha nia ya kulinunua.
Tevez ameshakwenda kuliona, huenda ataenda kuishi hapo wakati huu anapoanza maisha mapya akiwa na Man City.
Ronaldo anakwenda kuishi Madrid, Hispania, Man U imemuuza kwa Paundi za Uingereza milioni 80 ambazo ni sawa na zaidi ya sh BILIONI 160 za Tanzania.

Beckham ajuta, amuonya Terry

Beckham(kushoto), Walcott na Terry wakishangilia bao walipopambana na timu ya taifa ya Andorra mwezi uliopita

Nahodha wa Chelsea na timu ya Taifa ya soka ya England, John Terry

Terry na mkewe, Toni wakati wa sherehe ya harusi ya Joe Cole mwezi uliopita.

NYOTA wa soka Uingereza, David Beckham(34) anajuta kuhama Man United na ilimuumiza sana kiasi kwamba, kwa miaka mitatu, alishindwa hata kutazama mechi za mashetani wekundu.
Beckham amesema, Nahodha wa timu ya soka ya England, John Terry anapaswa kutafakari kwa kina kabla ya kuamua kuhama Chelsea.

Amesema, mabilioni ya Man City SI KITU kwa JT kama anaipenda Chelsea.
Amesema, alihama Man U wakati akiwa anaipenda klabu hiyo, alipanga kumalizia soka lake Old Trafford lakini hakuwa na la kufanya, ilibidi ahamie Real Madrid ya Hispania.

SOMA HAPO CHINI

DAVID BECKHAM has warned John Terry to think very carefully before making a decision to quit Chelsea.
Becks knows all about the pain of leaving the club you have always supported, having joined Real Madrid after 10 years at Manchester United.

And he reckons Manchester City's billions should not - and will not - be enough to lure 28-year-old Terry to Eastlands.

Becks said: "Happiness is the biggest thing. If you've got passion to play for the club you're at - and you're at the club you always wanted to be at - that goes beyond any money.

"JT's like that. He's passionate about football, not passionate about money. He'll decide what's best for his career. It won't be about money for him."

"He's England captain and you don't become England captain by being greedy. You get the job because you're passionate about the game."

Terry succeeded Becks as Three Lions skipper in 2006 and the two have become good friends.

And Beckham recalled the pain of leaving Old Trafford was so bad he could not even watch his old team on the telly.

The midfielder, 34, revealed: "I always wanted to stay at United for my whole career but there was nothing I could have done about it. It wasn't in my hands when I left United.

"I missed it. I couldn't even bear to watch them on the TV for the first three years after leaving just because it hurt me a lot."