Alhamisi ya wiki iliyopita kijana huyo maarufu pia Afrika alifunga pingu za maisha na Enid Keishamaza Rukikaire.
Wapenzi hao walifunga ndoa katika kanisa la Mtakatifu Francis la Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.
Watu wasiozidi 30 walishuhudia viapo vya Gaetano na Enid, na kwa ujumla ndoa na harusi vilikuwa siri kiasi kwamba, hata mapaparazi hawakuweza kunusa kilichokuwa kikiendelea.
Ingawa haijawekwa wazi, huenda hata kufungwa kwa ndoa hiyo Alhamisi Julai tisa badala ya Jumamosi Julai 11 ilikuwa ni mikakati ya kuvikwepa vyombo vya habari.
Harusi ya mtangazaji huyo na Enid haikuwa na shamrashamra zozote na waliifanya simple kuliko ilivyotarajiwa.
No comments:
Post a Comment