Thursday, February 26, 2009

Katibu Mkuu UN kawasili Tanzania

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amewasili Dar es Salaam leo mchana kuanza ziara ya siku mbili bara na Zanzibar.

Ndege iliyomleta kiongozi huyo wa UN, wasaidizi wake, mkewe, Yoo Soon-taek, na waandishi wa habari ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere saa 8:54 mchana.

Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliwaongoza viongozi wa Serikali kumpokea Ban, Mratibu Mkazi wa Mashirika 17 ya UN yaliyopo nchini, Oscar Fernandez Taranco aliongoza ujumbe wa wafanyakazi wa mashirika hayo katika mapokezi hayo.

Viongozi kadhaa wa Serikali walishiriki kumpokea kiongozi huyo aliyetoka Afrika Kusini, wakiwamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Batilda Burian, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania UN, Balozi Augustine Mahiga, na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Patrick Tsere.

Baada ya kuteremka kwenye ndege ya UN, Ban na mkewe walipokea mashada ya maua, ukapigwa wimbo wa UN na wimbo wa Taifa la Tanzania, na alikagua gwaride.

Ban kesho anatarajiwa kwenda Zanzibar, atakuwa na mazungumzo na Rais Amani Abeid Karume, anatarajiwa kufungua ofisi za UN visiwani humo, atakwenda Arusha kutembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari(ICTR), jioni yeye na mwenyeji wake, Rais Kikwete watazungumza na waandishi wa habari, leo usiku kiongozi huyo wa UN anatarajiwa kuondoka nchini.

Mungu hakunyimi vyote


NYOTA Waziri ni miongoni wa wanamuziki wanawake Tanzania wenye sifa ya pekee.
Ni mke wa kiongozi wa bendi ya The Kilimanjaro, maarufu kama wana Njenje, ni mwimbaji pekee mwanamke katika bendi hiyo iliyonzishwa miaka ya 1970's.
Kwa muda mrefu Nyota na mumewe, Waziri Ally wamekuwa wakitafuta mtoto, hadi sasa hawajafanikiwa, hawajakata tamaa.
Nimewahi kufanya mahojiano na Nyota nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es Salaam, alibubujikwa machozi kwa sababu ya uchungu wa kukosa mtoto, inamuumiza.
Wapenzi wa Njenje wanamfahamu, sauti yake si mchezo, akiimba Gere ndo balaa, na siku hizi kabuni kitu, wakati wimbo huo unaisha wanawake hupata nafasi kuonyesha wanavyoweza kutumia nyonga zao.
Hutaja mikoa wanapotoka ili kuwaonyrsha wa mikoa mingine kuwa wao wapo juu, Nyota huwa huwahamasisha kwa kusema mfano, Tanga tupo juu, tupo juu, tupo juu, tup juu shitua waa!

Beckham nje ya uwanja





MWANASOKA maarufu, David Beckham akiwa na mwanae, Brooklin

Namba za Nature hadharani


MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature ametangaza namba zake za simu ya mkononi ili mashabiki wampigie kuuliza hili na lile kuhusu albamu yake mpya iitwayo Tugawane Umasikini yenye nyimbo 10.
Ukitaka kulonga na kiongozi huyo wa kundi la TMK wanaume Halisi piga 0787878108 au 0713424943.
Wasanii wengi wanaona namba zao kama almasi, hongera Nature kwa kuonyesha mfano.
Waziri Mkuu alitangaza namba zake hadharani itakuwa wewe?

Tanzania yapata Jaji Kiongozi


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu baada ya kumuapisha jana.

RAIS jakaya Kikwete jana alimuapisha Jaji Fakihi Jundu kuwa Jaji Kiongozi.

Jaji Jundu anachukua nafasi ya Salum Massati aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Baada ya kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jaji Kiongozi alitema cheche kwa mahakimu na majaji kwa kuwataka wawe makini wanapotoa uamuzi kuhusu kesi za ufisadi kwa kuwa jamii inafuatilia na kupima uamuzi huo.

Ivory Coast wanajuta kutufahamu


TIMU ya soka ya taifa, maarufu kwa jina la Taifa Stars jana usiku walitupa raha Watanzania kwa kuinyuka timu ya Ivory Coast bao moja kwa mzunguko hivyo kuwang'oa wenyeji hao kwenye michuano hiyo inayoshirikisha nchi nane.

Mrisho Ngassa jana alikuwa mwiba kwa Ivory Coast na ndiye alifunga bao hilo kqwa kichwa katika dakika ya 37 ya mpambano huo ulioonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa, TBC1.
Maximo boys wanastahili sifa, tangu mwanzo wa mchezo walionyesha dhamira ya kutaka kushinda, walicheza kwa kujituma kutetea nchi yao.

Stars wakiinyuka Zambia watatinga nusu fainali, kila la heri vijana wa Maximo, fanyeni kweli na wengine wajute kutufahamu.

Wednesday, February 25, 2009

Watoto wenye miaka 15 wazaa pacha



WATOTO waliozaa pacha wawili wamesema, watakuwa wazazi wazuri na wataendelea na masomo.

Watoto hao raia wa Uingereza, Sammii Humphries na Daniel Sargent wanasoma pamoja, walianza uhusiano wakati wakiwa na umri wa miaka 13.

Daniel amesema, atasoma ili aje kuwa polisi, Sammmii amesema anapenda kuja kuwa muuguzi.

Sammiii alipata ujauzito wakati akiwa na umri wa miaka 14, hakugundua hadi mimba ilipofikisha wiki 22.

Hivi karibuni, mtoto mwenye umri wa miaka 13, Alfie aliibuka kuwa baba, na kama kipimo cha DNA kitathibitisha kweli ni mwanae atakuwa ni baba mwenye umri mdogo zaidi nchini Uingereza.

Utani Kenya (2)

11. Nyanyako mzee mpaka chawa za nywele yake hutembea na bakora.

12. Ati nyinyi ni wengi nyumbani kwenyu yaani buda (baba) yenu hajui majina mpaka huwa address kama wananchi. (KAMA RAISI ANAPOTOA HOTUBA)

13. TV yenyu ni ndogo lazima ufunge jicho moja ndio uone picha.

14. Wewe mblack mpaka unasweat soot.

15. Wewe mnono mpaka ukivaa yellow watoto wanafikiria ni schoolbus.

16. Manzii wako ni m ugly mpaka alikataliwa ku act horror (movie ya kutisha) Hollywood.

17. Nyumba yenyu ni ndogo mpaka lazima utoke nje kuchange mind.

18. Kwenyu nyinyi ni wengi mpaka kwa hao (house) kuna round-about.

19. Kwenu nyinyi ni wa daft (WAJINGA) mpaka kupata driving license ilibidi mpelekwe boarding school.

20. Nywele za watoto wenyu ni ngumu mpaka mnazitumiaga kama steel wool.

Liyumba arudishwa Keko

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imefuta dhamana iliyotoa kwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya sh bilioni moja.

Amatus Liyumba jana alifika katika mahakama hiyo hivyo kumaliza uzushi kuwa alitoroka baada ya kujidhamini siku kadhaa zilizopita.

Mahakama imebaini kuwapo kwa makosa 10 katika hati alizowasilisha kwa ajili ya maombi ya dhamana ikiwa ni pamoja n akuwapo kwa majengo yanayofanana na inazitilia shaka hati hizo.

Mshitakiwa huyo pia aliwasilisha mahakamani hati ya kusafiria iliyokwisha muda wake, lakini imebainika kuwa ana hati nyingine ya kusafiria aliyoipata mwaka 2005, itakwisha muda wake 2015.

Liyumba alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Benki kuu Tanzania(BoT), yeye na mwenzake, Deogratius Kweka wanatuhumiwa kuidhinisha mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya taasisi hiyo ya Serikali bila idhini ya bodi ya BoT hivyo kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200.

Majengo hayo yapo Dar es Salaam, Liyumba atapandishwa kizimbani Machi 10 mwaka huu.

'usiniangushe'


Tuesday, February 24, 2009

Liyumba atinga Kisutu

MMOJA wa washitakiwa katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200, Amatus Liyumba leo amevunja ukimya na kubatilisha taarifa kuwa alitoroka baada ya kupewa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Liyumba alifika mahakamani hapo leo asubuhi, kesi ikaendelea kama kawaida huku kukiwa na mabishano kati ya mawakili wa Serikali na wale wa washitakiwa.

Hadi saa saba mchana leo mahakama ilikuwa haijatoa uamuzi kuhusu dhamana lakini hisia za wengi ni kwamba huenda Liyumba atarudi rumande kwa kuwa mawakili wa Serikali wamedai kuwa kitendo chake cha kuwasilisha mahakamani hati ya kusafiria iliyokwisha muda wake huku akiwa na hati nyingine kimeonyesha kuwa si muaminifu.

Kipi kinatangulia peponi?

The nun was teaching Sunday school, speaking to her class one morning and she asked the following question,

Nun: "When you die and go to heaven... which part of your body goes first?"

Suzy raised her hand and said: " I think its your hand."

Nun: " why do you think its you hands, suzy?

Suzy: " Because when you pray, you holds your hands together infront of you and God just take your hands first."

Nun: " What a wonderful answer "

Little Johnny raised his hand and said, " sister, I think its your legs.

The nun looked at him with the strangest look on her face.

Nun: "Now Johnnie why would you think it would be your legs?"

Little Johnny: "Well... I walked into mammy's and daddy's bedroom Other night... Mammy had her legs straight up in the air, and she was crying and saying, " OH GOD, I'M COMING!, If daddy didn't pinned her down, between her legs, We'd have lost her!"

Utani Kenya

1. Ati wee ni m-black mpaka ukiingia kwa ndinga dirisha zinakuwa tinted!

2. Kwenu kuchafu mpaka mende zinatema mate, ati ‘THU’ hii hao (HOUSE) ni noma.

3. Vile wewe mfupi, ukipigwa picha ya passport inatokea full.

4. Kwenu nyi wakristu hata dogi zenu zikiona mwizi anaiba, zinawaambia “wee iba tu Mungu anakuona.”

5. Ati hao (house) yenu ina gate lakini hakuna fence.

6. We' ni mshort mpaka ukikalia kwa pavement (sakafuni) miguu ina hang kwa hewa.

7. We mjinga mpaka ulifail blood test.

8. Wewe ni mblack mpaka mosquito ikitaka kukuuma lazima itumie torch.

9. We ni mrefu mpaka ukikunywa maziwa inafika kwa tumbo ikiwa mala (MGANDO/MTINDI).

10. Wewe ni mweusi ukikanyanga mahali unawacha footprint za blak kwa makaa.

Utaendelea kesho.

Kazi ni kazi bora...



KUNA watu ukizungumza nao wanalalamika kwamba aah nipo tu pale, kazi yenyewe nafanya tu basi, kazi nyingi, ngumu ila nitafanyaje inabidi tu nifanye.
Wakati wanayasema hayo kuna watu wanafanya kazi ngumu na kwenye mazingira magumu kuliko wao.
Thamini kazi yako, timiza wajibu wako, wewe ukisema ya nini, wenzio wanauliza wataipata lini.

Bora kuchelewa kuliko kutokufika


NDIYO hali halisi, wakati mwingine hatutumii busara hata kwa mambo ya msingi yanayohusu maisha yetu na tunaowapenda.

Monday, February 23, 2009

Mtoto aliyeuzwa sh 100, 000/=


Fatma Kisawiro akiwa na mama yake mzazi, Tabu William Polisi, Dar es Salaam.
MTOTO mwenye umri wa miezi tisa aliyezua utata baada ya mama yake mzazi, Tabu William(36) kudai kuwa amemuuza kwa sh 100,000 za Tanzania amepatikana akiwa hai Chalinze mkoani Pwani.
Mtoto huyo kwenye picha yake hapo juu amerudishwa kwa mama huyo huyo anayeandaliwa mashitaka ili ajibu tuhuma za kumuuza mwanae.
Nina mashaka kuhusu usalama wa mtoto huyo kwa kuwa siamini kama sababu zilizosababisha auzwe hazipo tena.

Liyumba bado kitendawili


Amatus Liyumba(kulia)

KUNA taarifa zinazodai kuwa mmoja wa watuhumiwa wawili katika mashitaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200, Amatus Liyumba amepatikana.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya Serikali iliyothibitisha taarifa hizi, kitendawili kitateguliwa kesho kwa kuwa ndiyo siku aliyopangiwa kufika tena mahakamani.

Liyumba aliachiwa kwa dhamana iliyozua utata na hadi sasa mengi yanasemwa mitaani kuhusu dhamana hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mtaani kwetu

ANA ASHUO LA PANYA AKIONA WAGENI ANAJIPITISHA

Mbona leo hukwenda shuleni?


RAIS Jakaya Kikwete amekuwa mfano wa kuigwa kwa namna anavyoweza kujishusha na kuzungumza na wananchi wa hali ya chini wakiwamo watoto kutoka katika familia masikini.
Unaweza kutoa tafsiri nyingi kuhusu picha ya hapo juu ila usisahau kwamba huyo anayezungumza na mtoto ni Rais wa nchi hivyo hadi mtoto huyo afike hapo kwenye gari lazima kiongozi huyo alimuita, jamaa wa usalama wakamruhusu.
Pia unapoitafsiri hiyo picha ujiulize kwa nini Rais alimuita mtoto na si mtu mzima?

Utapeli mpya Dar es Salaam


MUDA mfupi uliopita nimepata nyepesi kuhusu aina mpya ya utapeli jijini Dar es Salaam ambao pia unahatarisha maisha ya raia wasio na hatia.

Kuna wajanja fulani wanaotumia fursa ya kwamba kila anayepigiwa kelele za Mwizi Mwizi Mwizi hadharani atasulubiwa bila ya kuhojiwa, wamezua mtindo wa kuwaomba watu simu zao, wajifanye wanabip.
Ukiwapa simu wanapigiwa na yule waliyembip ambaye ni mwizi mwenzake, wanawaomba waliowapigia wawatajie namba ya simu waliyoitumia - kwa kuwa ni washirika wenzao katika dili - ili baadaye wanadai kuibiwa simu.

Katika purukushani ya kumtafuta Mwizi huyo wa simu, ambaye si mwizi, ila yule ambaye anayedai kuibiwa ndiye mwizi halisi, inatajwa namba ya simu inayodaiwa kuibwa. Inapolia, inaita kwa mtu ambaye si mhusika, hapo hapo anaanza kusulubiwa bila kuhojiwa.

Uovu huu wa kuwahukumu watuhumiwa badala ya kuwapeleka katika mamlaka husika wakajibu tuhuma zinazowakabili umeanza kuwaathiri raia wema. Hii ndiyo bongo, kaeni chonjo, msije kuitwa wezi mkachomwa moto.

Ushauri: Mtu usiyemfahamu akikuomba simu yako ili abip kataa kata kata, mwambie simu yako haibip hata siku moja, anakushusha hadhi! Akisema si wewe unayebip, unamwambia hata kama si wewe! Akileta za kuleta unamkata kibano cha nguvu na kumpigia kelele za Mwizi Mwizi, wamsulubu yeye!

Saturday, February 21, 2009

Mtaani kwetu

KUZUNGUKA MBUYU SI KAZI, KAZI NI KUUKUMBATIA

Liyumba yupo wapi?


Amatus Liyumba

YEYE na mwenzake, Deogratius Kweka wanashitakiwa kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200.

Liyumba alipewa dhamana iliyozua utata kwa kuwa hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Khadija Msongo, aliruhusu mshitakiwa huyo awe nje kwa dhamana ya sh milioni 882 tu wakati mwanzo alitakiwa kudhaminiwa kwa fedha taslimu sh bilioni 55 au mali zisizohamishika zenye thamani hiyo.

Siku moja baadaye mshitakiwa huyo alitakiwa mahakamani tena lakini hakuonekana, na hadi sasa anatafutwa.

Harusi watoto wa vigogo



BINTI wa Rais Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Jacob Zuma, Gugutethu, amefunga pingu za maisha na mtoto wa Katibu Mkuu wa Chama MDC cha Zimbabwe, Welshman Ncube, Bongani Ncube.
Picha ya msichana huyo akiwa na mumewe, Bongani, picha ya chini ni Zuma na akiwa na binti yake siku ya harusi hiyo. Picha hizo ni kwa hisani ya drfaustine.blogspot.com

Kuhalalisha ombi lililokataliwa

Dear Sir / Madam,

RE: ADVERTISED POSITION: YOUR LETTER OF REJECTION

Thank you for your letter of 20th January 2009.

After careful consideration I regret to inform you that I am unable to accept your refusal to offer me employment with your company.

This year I have been particularly fortunate in receiving an unusually large number of rejection letters. With such a varied and promising field of candidates it is impossible for me to accept all refusals.

Despite your company's track record and previous experience in rejecting applicants, I find that your rejection does not meet my needs at this time.

Therefore I will start work with your company on Monday 23 February 2009 at 8.00 am.
I look forward to seeing you then. Don't call me I'll call you.

Yours sincerely

Sugusugu Sugumba

Mungu akisema NDIYO nani atasema HAPANA?


Barack Obama(kulia) enzi hizo alipowatembelea ndugu zake Kenya


Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na Rais Mstaafu wa nchi hiyo, George W Bush White House jijini Washington

Askofu Pengo amtuma Mkapa kwa Nyerere



KATIKA hali isiyotarajiwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Policarp Pengo leo amemtuma Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akahiji katika eneo alipozikwa hayati baba wa Taifa, Julius Nyerere ili afikishe shukurani zake kwa kujenga mazingira yaliyoliwezesha kanisa kufanya kazi zake.

Baba wa Taifa, alifarikidi dunia Oktoba 14, 1999 Katika hospitali ya Mt Thomas, London uingereza, alizikwa katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.

Kadinali Pengo alimweleza Mkapa akamweleze Nyerere kuwa yeye (Pengo) ni mwendawazimu lakini anamshukuru kwa kuwa alijenga mazingira yaliyoliwezesha kanisa lifike lilipofika.

Wakati akizungumza hayo kwenye ibada ya maadhimisho ya miaka 25 tangu alipopata daraja la uaskofu mwaka 1984 kuna wakati Askofu Mkuu Pengo alikosea na kumwita Mkapa Mhashamu.

Masdhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maaskofu wakuu wa kanisa katoliki nchini, maaskofu, mapadre, masista, watumishi wa kanisa wa kanyingine na waumini

Alimtaka Mkapa afikishe shukurani hizo kwa marais waliomtangulia akiwamo Nyerere, na mrithi wake, Jakaya Kikwete.

Pengo alipata daraja la upadre Juni 20, 1971, Novemba 1983 Baba Mtakatifu alimteua kuwa askofu, akawekwa wakfu Januari 1984, Machi 10 mwaka 1990 aliteuliwa kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, mwaka 1998 Papa alimteua kuwa kardinali.

Thursday, February 19, 2009

Fukuto ATCL


KAULI ya Waziri wa Maendeleo y a Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa kwamba hana taarifa kuhusu mpango wa kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuwapeleka wafanyakazi likizo bila malipo imezua utata.

Ijumaa iliyopita Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, David Mattaka alizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo akawaeleza kuwa Serikali ilimtuma akawape ujumbe wa ama kuachishwa kazi au kwenda likizo bila malipo kwa kuwa wapo wengi kuliko idadi ya ndege zilizopo.

Wafanyakazi jana walitoa msimamo wao rasmi kwamba hawataki kwenda likizo bila malipo ila wapo tayari kuachishwa kazi.

Kwa namna ‘sinema’ hii inavyoendelea bila shaka Serikali kuu itabidi iingilie kati kwa kuwa ndiye mmiliki wa kampuni.

Bongo Dar es Salaam




Picha kwa hisani ya Michuzi Jr

NDIYO hali halisi jijini Dar es Salaam mvua inaponyesha.

Simu za mkononi zinaua





INASIKITISHA sana, simu yako ya mkononi inakusababishia kifo!
Miezi kadhaa iliyopita nilishuhudia tukio kama hili, mimi na wanafamilia tulikuwa nyumbani, mmoja wetu alikuwa anachaji simu.
Wakati tukiendelea na mazungumzo ile simu ililipuka na kuunguza kidogo kochi, kwa bahati hakukuwa na mtu jirani hivyo hakuna aliyeumia.
Ujumbe niliotumiwa kwenye barua pepe umenikumbusha tukio lile, kuna mtu alikuwa anachaji simu, akapigiwa, akapokea wakati bado kaichomeka kwenye umeme, wakati anaendelea na mazungumzo ikamlipukia.
Wazazi wake walimkimbiza hospitali huku hajitambui, baada ya muda madaktari walisema alikuwa amefariki dunia. USHAURI WA BURE: Usitumie simu wakati imechomekwa kwenye umeme ni hatari kwa maisha yako.

Wednesday, February 18, 2009

Mchezaji bora Afrika au muafrika?


Mchezaji bora wa Afrika 2009, Emmanuel Adebayor

KUNA mdau kanitumia hii,nimeona ana hoja, wadau wa soka ifanyieni kazi hii

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana uteuzi wa mchezaji bora Duniani katika mabara mbalimbali ila mpka sasa nashindwa kuelewa ni vigezo gani wanavitumia wenzetu wa mabara mengine kwani uteuzi wao ni tofauti kabisa na unaofanywa na bara la Africa CAF.

Ukianza na Brazil Kaka, Ronaldinho, Ronaldo na wengine wengi wote hao wamewahi kuwa wachezaji bora DUNIANI ila hata mara moja hawajawahi kushinda tuzo ya mchezaji bora America ya Kusini, kwanini...?

Sababu ni moja wao na wengine wote isipokuwa Africa,wanathamini mashindano yanayofanywa ndani ya mabara yao na best player anatokana na katika mashindano ya vilabu ndani ya bara lao.

Tukirudi Ulaya wachezaji wote niliowataja hapo juu wa brazil pamoja na waafrika kama George weah wamewahi kuwa wachezaji bora Ulaya ingawa wao sio wazaliwa wa hapo...Simple because wanacheza katika vilabu vya Ulaya.

Sasa iweje huku kwetu Africa kila mwaka mchezaji bora wa Africa anatoka Ulaya? je wanatumia vigezo gani kumpata huyo mchezaji? mwisho kwa mchezaji aliyekuwa anachezea ndani ya bara la Africa kuwa mchezaji bora ilikuwa mwaka 1985 mchezaji toka Morocco Mohammed Timoumi aliyekuwa akiichezea FAR Rabat ndiye alishinda tuzo hiyo..., je hii ni sawa?

ni sawa kulinganisha wachezaji wanaocheza Champions league, EPL, La Liga na makombe yetu ya vilabu Africa..?,

Je huyu tumuite Mchezaji bora wa Africa au Mchezaji bora Muafrica.., maana kwa utaratibu huu hata kaka akija kucheza Africa hawezi shinda tuzo hii maana inaonekana jambo la kwanza hapa tunaloangalia ni uafrica na sio mchezaji anachezea wapi.

Kwa kuzingatia hoja ya hapo juu, Emmanuel Adebayor ni mchezaji bora Afrika mwaka 2009 au mchezaji bora muafrika mwaka 2009?

Mkongwe wa dansi katutoka


Picha kwa hisani ya Issamichuzi.blogspot.com

MMOJA wa watunzi mahiri wa bendi ya Ottu Jazz Band 'Wana msondo ngoma', Joseph Maina amekufa jana Dar es Salaam wakati akienda Studio Oysterbay jijini humo.
Kiongozi wa bendi hiyo, Muhidin Ngurumo amesema marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume na watatu wa kike. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amen

Buriani Violet

MLIOHITIMU katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mwaka 2007 bila shaka mnamfahamu Violet Novatus. Msichana huyo alikuwa active kwenye michezo, alikuwa MC kwenye shughuli mbalimbali, na alikuwa kiongozi wa vijana.

Nasikitika kuwatangazia kuwa msichana huyo amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya Dk Hubert Kairuki (Mikocheni Hospital) jijini Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu, Allen amenieleza leo kwamba, Violet alikuwa na uvimbe tumboni akafanyiwa operesheni katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam, baada ya tiba hiyo amekuwa mgonjwa hadi alipoaga dunia jana.

Kwa atakayeweza tafadhali aufahamishe pia uongozi wa Don Bosco Upanga Dar es Salaam, wanamfahamu kwa kuwa, licha ya kuwa kiongozi wa vijana, alikuwa akicheza mpira wa kikapu kwenye viwanja hivyo.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na kaka wa marehemu kwa simu namba 0767-777774

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amen.

Mshindi BSS bado yupo yupo


KINARA wa shindano la kusaka vipaji vya wanamuziki, maarufu kama Bongo Star Search(BSS) la mwaka jana, Misoji Nkwabi amekuwa kimya kwa muda mrefu lakini huenda utaanza kumsikia muda si mrefu.
Nimewasiliana naye leo akanieleza kuwa bado yupo kwenye game, amemaliza kurekodi albamu hivyo anajiandaa kuiingiza sokoni.
Misoji amesema alikuwa kimya kwa kuwa alikuwa akijiandaa kufanya mtihani wa kidato cha sita, na ameshamaliza kufanya mtihani huo hivyo sasa yupo free.

Tuesday, February 17, 2009

Jitahidi uende Isimila






Eneo la kihistoria la Isimila mkoani Iringa

Mkataba wa ndoa

Soma mjadala huu wa mke na mume, kumbe ndoa si paradiso!

WIFE: Honey what are you looking at?

HUSBAND: Nothing!

WIFE: Nothing! and you have been reading our marriage certificate for an hour?

HUSBAND:I was looking for the expiry date of this damn marriage contract!

Mtaani kwetu

INAWEZEKANA kutokana na shughuli zako au mazingira unayoishi unashindwa kusikia baadhi ya kauli au misemo ya uswahilini, si vibaya ukiifahamu kwa kuwa ipo hivyo hata nisingekuambia kwenye blog hii ya jamii ingendelea kuwepo.

Nitajitahidi kadri ninavyoweza kukujulisha yanayosemwa mitaani kwa kuwa ni mengi hivyo kila nitakavyoyapata nitakusimulia.

Leo naanza na hii ' KAMA KUOGA NI USAFI TAULO ISINGECHAFUKA'

Na wewe?


Amri 10 za usalama barabarani

1. You shall not kill.

2. The road shall be for you a means of communion between people and not of mortal harm.

3. Courtesy, uprightness and prudence will help you deal with unforeseen events.

4. Be charitable and help your neighbor in need, especially victims of accidents.

5. Cars shall not be for you an expression of power and domination, and an occasion of sin.

6. Charitably convince the young and not so young not to drive when they are not in a fitting condition to do so.

7. Support the families of accident victims.

8. Bring guilty motorists and their victims together, at the appropriate time, so that they can undergo the liberating experience of forgiveness.

9. On the road, protect the more vulnerable party.

10. Feel responsible toward others.

Monday, February 16, 2009

maswali?


Nani Oprah wa Tanzania?





OPRAH Winfrey ni miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani, na nathubutu kusema huenda anaongoza kwa umaarufu miongoni mwa wanawake hivi sasa.
Namtafuta Oprah wa Tanzania, si lazima utajiri kama mwanamke huyo wa Marekani ila ni lazima mwanamke huyo Mtanzania 'awe nazo' na awe mwanamke maarufu zaidi Tanzania.
Si vibaya na sisi tukianzisha utaratibu wa Kutambuana, kama unahisi una sifa za kuwa Oprah wa Tanzania tafadhali tuma ujumbe kwenye blog hii ya jamii, na endapo unamfahamu mwenye sifa hizo pia tufahamishe.


Zimbabwe itabadilika?


Dunia inasubiri kuona kama Serikali ya umoja italeta mabadiliko Zimbabwe

Mtaji wa masikini







SINA hakika kama kweli mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe

Tanki la mafuta lapasuka DSM

KUNA taarifa kwamba tanki la lori la mafuta limepasuka muda mfupi uliopita katika makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, polisi tayari wamefika kwenye eneo la tukio kuhakikisha usalama ikiwa ni pamoja na kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na mlipuko wa moto.

Kwani unabisha?


UKIAMBIWA utaje wasanii watatu wakali wa bongo flava si rahisi kuyaacha majina ya hao hapo juu, Lady Jay Dee na Profesa J.
Wapo wanaoamini kuwa, Jide na Jay ndiyo wakali zaidi kwa bongo flava, kama una hoja kupinga hilo sema usikike