
KATIKA hali isiyotarajiwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Policarp Pengo leo amemtuma Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akahiji katika eneo alipozikwa hayati baba wa Taifa, Julius Nyerere ili afikishe shukurani zake kwa kujenga mazingira yaliyoliwezesha kanisa kufanya kazi zake.
Baba wa Taifa, alifarikidi dunia Oktoba 14, 1999 Katika hospitali ya Mt Thomas, London uingereza, alizikwa katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
Kadinali Pengo alimweleza Mkapa akamweleze Nyerere kuwa yeye (Pengo) ni mwendawazimu lakini anamshukuru kwa kuwa alijenga mazingira yaliyoliwezesha kanisa lifike lilipofika.
Wakati akizungumza hayo kwenye ibada ya maadhimisho ya miaka 25 tangu alipopata daraja la uaskofu mwaka 1984 kuna wakati Askofu Mkuu Pengo alikosea na kumwita Mkapa Mhashamu.
Masdhimisho hayo yalifanyika katika viwanja vya kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maaskofu wakuu wa kanisa katoliki nchini, maaskofu, mapadre, masista, watumishi wa kanisa wa kanyingine na waumini
Alimtaka Mkapa afikishe shukurani hizo kwa marais waliomtangulia akiwamo Nyerere, na mrithi wake, Jakaya Kikwete.
Pengo alipata daraja la upadre Juni 20, 1971, Novemba 1983 Baba Mtakatifu alimteua kuwa askofu, akawekwa wakfu Januari 1984, Machi 10 mwaka 1990 aliteuliwa kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, mwaka 1998 Papa alimteua kuwa kardinali.
No comments:
Post a Comment