KAULI ya Waziri wa Maendeleo y a Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa kwamba hana taarifa kuhusu mpango wa kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuwapeleka wafanyakazi likizo bila malipo imezua utata.
Ijumaa iliyopita Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, David Mattaka alizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo akawaeleza kuwa Serikali ilimtuma akawape ujumbe wa ama kuachishwa kazi au kwenda likizo bila malipo kwa kuwa wapo wengi kuliko idadi ya ndege zilizopo.
Wafanyakazi jana walitoa msimamo wao rasmi kwamba hawataki kwenda likizo bila malipo ila wapo tayari kuachishwa kazi.
Kwa namna ‘sinema’ hii inavyoendelea bila shaka Serikali kuu itabidi iingilie kati kwa kuwa ndiye mmiliki wa kampuni.

No comments:
Post a Comment