Wednesday, February 18, 2009

Buriani Violet

MLIOHITIMU katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mwaka 2007 bila shaka mnamfahamu Violet Novatus. Msichana huyo alikuwa active kwenye michezo, alikuwa MC kwenye shughuli mbalimbali, na alikuwa kiongozi wa vijana.

Nasikitika kuwatangazia kuwa msichana huyo amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya Dk Hubert Kairuki (Mikocheni Hospital) jijini Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu, Allen amenieleza leo kwamba, Violet alikuwa na uvimbe tumboni akafanyiwa operesheni katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam, baada ya tiba hiyo amekuwa mgonjwa hadi alipoaga dunia jana.

Kwa atakayeweza tafadhali aufahamishe pia uongozi wa Don Bosco Upanga Dar es Salaam, wanamfahamu kwa kuwa, licha ya kuwa kiongozi wa vijana, alikuwa akicheza mpira wa kikapu kwenye viwanja hivyo.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na kaka wa marehemu kwa simu namba 0767-777774

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amen.

No comments:

Post a Comment