

Miezi kadhaa iliyopita nilishuhudia tukio kama hili, mimi na wanafamilia tulikuwa nyumbani, mmoja wetu alikuwa anachaji simu.
Wakati tukiendelea na mazungumzo ile simu ililipuka na kuunguza kidogo kochi, kwa bahati hakukuwa na mtu jirani hivyo hakuna aliyeumia.
Ujumbe niliotumiwa kwenye barua pepe umenikumbusha tukio lile, kuna mtu alikuwa anachaji simu, akapigiwa, akapokea wakati bado kaichomeka kwenye umeme, wakati anaendelea na mazungumzo ikamlipukia.
Wazazi wake walimkimbiza hospitali huku hajitambui, baada ya muda madaktari walisema alikuwa amefariki dunia. USHAURI WA BURE: Usitumie simu wakati imechomekwa kwenye umeme ni hatari kwa maisha yako.
No comments:
Post a Comment