Tuesday, April 10, 2012

Vilio, majonzi viwanja vya Leaders

Mwili wa Steven Kanumba umefikishwa muda mfupi uliopita katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.


Watu wamefurika katika viwanja hivyo, wengi wanalia, wengine wanapoteza fahamu.


Mwili wake upo kwenye jeneza jeusi.


Kuna waliokuwa hawaamini kwamba, Kanumba hatupo naye, lakini baada ya kuliona jeneza hilo sasa wameamini, kwamba, ni kweli Steven Kanumba ameaga dunia.


Ibada ya kumuombea marehemu Kanumba imemalizika katika viwanja vya Leaders.


Wasanii, viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, wadau wa sanaa, waandishi wa habari na wananchi wengine wanahudhuria ibada hiyo na baadaye watauona kwa mara ya mwisho Kanumba.



Hivi sasa viongozi mbali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal wanatoa heshima za mwisho ili waweze kuondoka katika viwanja hivyo wakaendelee na shughuli nyingine.



Baada ya viongozi hao kumuaga Kanumba, ratiba ya shughuli hiyo inayooneshwa ndani na nje ya Tanzania itaendelea kama kawaida, na hatimaye mamia ya wananchi waliojaa eneo hilo watatoa heshima za mwisho.


Hadi Kanumba anaaga dunia, aliweza kuigiza zaidi ya filamu 40.

1 comment: