MVUA kubwa imenyesha Mwanza leo na kusababisha maeneo mengi ya jiji hilo kukumbwa na mafuriko.
Shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo mengi ya jijini hilo zimesimama na kwa ujumla watu wengi wameathirika kwa namna tofauti.
Uwanja wa ndege wa Mwanza umefungwa kuanzia saa 3.10 leo asubuhi kwa kuwa umejaa maji hivyo ndege hazitui wala kuruka.
Kwa mujibu wa uongozi wa uwanja huo, unatarajiwa kufunguliwa saa 9.10 alasiri.
Hadi wakati uongozi wa uwanja unatoa kauli hiyo, mvua ilikuwa inaendelea kunyesha, hivyo huenda huduma ya kutua na kuruka ndege itaendelea kusitishwa hadi hali ya uwanja itakaporuhusu.
Kwa mujibu wa uongozi wa uwanja huo, miundombinu ya maji uwanjani hapo ni mizuri lakini uwanja hupo kwenye mkondo unaotoa maji milimani hivyo suala la uwanja huo kujaa maji ni la kawaida mvua zikinyesha.
No comments:
Post a Comment