KWA KUWA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUM KWA KILA CHAMA KATIKA BUNGE LA TANZANIA IMEZINGATIA IDADI YA WABUNGE WA VYAMA HUSIKA KATIKA MAJIMBO.
NA KWA KUWA IDADI YA WABUNGE WA CHAMA HUSIKA WANAWEZA KUPUNGUA KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI IKIWEMO KIFO AU KUJIUZULU KAMA ALIVYOFANYA ALIYEKUWA MBUNGE WA IGUNGA (CCM), ROSTAM AZIZ.
1. JE, IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUM CCM ITAPUNGUA?
2. KAMA JIBU NI NDIYO WABUNGE WANGAPI WA VITI MAALUM CCM WATAVULIWA UBUNGE?
3. VIGEZO VIPI VITAZINGATIWA KUAMUA HIVYO HASA IKIZINGATIWA KUWA, WABUNGE WA VITI MAALUM WANATOKA KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI WAKIWEMO KUTOKA KUNDI LA VIJANA, UWT, NGO'S NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI?
KAMA JIBU LA SWALI HAPO JUU NI HAPANA KWA MAELEZO KWAMBA UTAFANYIKA UCHAGUZI MDOGO,
1. KAMA MGOMBEA WA CCM ASIPOSHINDA, IDADI YA WABUNGE WAKE WA VITI MAALUM ITAPUNGUA AU ITABAKI KAMA ILIVYO SASA?
2. KAMA AKISHINDA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI, IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHAMA HUSIKA ITAONGEZEKA AU ITABAKI KAMA ILIVYO SASA?
3. KAMA CHAMA HUSIKA HAKITAONGEZEWA MBUNGE AU WABUNGE WA VITI MAALUM, NI KWA NINI?
No comments:
Post a Comment