Friday, May 20, 2011

Sheikh Yahya Hussein afariki dunia


MNAJIMU na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, ameaga dunia saa kadhaa zilizopita jijini Dar es Salaam.


Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema.


Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-Salaam.


Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo cha Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo.


Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusoma masuala ya dini katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichopo jijini Cairo.


Alirejea nchini mnamo miaka ya mwanzoni ya 60 ambapo alianza kazi yake ya utabiri .


Sheikh Yahya Hussein ndiye mtabiri wa mwanzo kueneza utabiri wa kila siku katika magazeti mbalimbali ya Afrika Mashariki enzi hizo.


Jina lake lilivuma zaidi alipokuwa akitoa utabiri kupitia radio kuhusu mashindano ya mpira kati ya nchi tatu za Afrika Mashariki yaliyojulikana kwa jina la Challenge Cup au Gossage Cup.

1 comment:

  1. hakika huu ni mwisho enzi za utawala wa giza la kuongoza nchi kwa ramli, uchawi na ana-ana-ana-do zake. mungu amuweke pahala anapostahili.

    ReplyDelete