Monday, March 21, 2011

Wenger akiri makipa ni tatizo Arsenal

Kocha wa washika bunduki wa London, Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa kuna tatizo la makipa katika timu hiyo.

Yaliyotokea Jumamosi wakati Alumnia alipofanya ujinga ulioigharimu timu ni mfano hai wa namna tatizo hilo linavyoigharimu Arsenal.

Kwa mtazamo wangu, kama kweli Wenger anataka makombe Arsenal, ni lazima akubali gharama za kusajili makipa na mabeki wenye viwango vya kimataifa.

Arsenal wana viungo wazuri akiwamo Samiri Nasri, Song, Jack Wilshire, na Cesc Fabregas, na wana washambuliaji wenye uwezo wa kucheka na nyavu, lakini mabeki na makipa mmmhhh!

No comments:

Post a Comment