Monday, March 21, 2011

David Luiz kanikuna!

Kwa wanaofahamu nashabikia timu gani Ulaya wanaweza kushangaa kwa nini nimesema, beki wa Chelsea, David Luiz kanikuna!
Katika soka ni jambo la kawaida kuipenda timu fulani lakini kuufurahia uchezaji wa mchezaji wa timu nyingine, ndivyo ninavyomaanisha.
Mimi si shabiki wa Chelsea na wala haitatokea, lakini nimejikuta napenda namna David Luiz anavyocheza kiasi kwamba natamani angekuwa katika katika timu ninayoipenda.
Kabla ya kusajiliwa Chelsea sikuwa namfahamu, lakini katika muda mfupi tangu aende darajani amethibitisha kwamba, matajiri wa London hawakufanya makosa kumnyakua kutoka Benfica ya Ureno.
Ninavyomuona, Luiz ni mmoja wa mabeki wazuri zaidi wa kulia duniani kwa sasa, yupo juu, ana bidii, hakati tamaa, ana vitu fulani vinavyovutia upende kumuona ana mpira, na kikubwa, yupo kikazi zaidi!
Si vibaya nikisema na hata nisiposema ndivyo ilivyo, napenda uchezaji wa David Luiz wa Chelsea, congrats Dogo.

Katika mechi ya jana kati ya Chelsea na Man City, licha ya kucheka na nyavu, nadiriki kusema kuwa alikuwa man of the match.

Kocha wa Chelsea akimbusu Ramires kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya jana.


Mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres akipeana mkono na kocha wake, Ancelotti wakati Elnino akitoka kumpisha Drogba.

No comments:

Post a Comment