Friday, March 18, 2011

Wakenya watumia kondom 1 mwezi mzima

HUENDA si jambo la kawaida kwa watu wengi lakini kwa vijana wanaoishi katika maeneo ya wafugaji nchini Kenya, kutumia kondom moja zaidi ya mara moja kwa mwezi mzima si jambo la ajabu.
Vijana katika kijiji cha Shambani wamekiri kwamba wanatumia kondom moja zaidi ya mara moja kwa kuwa hawana fedha za kutosha kununua kinga hiyo kila mara.
Wamesema, baada ya kuitumia kondom, wanaifua na kuianika ndani ili waitumie tena baadaye wanapojamiiana.
Mmoja wa vijana hao amekaririwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akisema kuwa, anapopata fedha ananunua kondom, anapoitumia anaiosha na kuihifadhi kwa sababu anakuwa hana uhakika wa kupata fedha nyingine za kununulia kinga hiyo.
Kwa mujibu wa vijana hao, dukani kondom zinauzwa sh 50 (za Kenya), hivyo kwa kuwa wanahitaji kujamiiana wanalazimika pia kutumia nailoni kujikinga na Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.

No comments:

Post a Comment