Tuesday, March 22, 2011

Asha Baraka aomba michango kwa ajili ya mazishi

KIONGOZI wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, amewaomba wadau wa muziki na Watanzania kwa ujumla watoe michango kufanikisha mazishi na maziko ya wasanii wa bendi ya Five Stars Modern Taarab waliokufa jana usiku katika ajali ya gari, Mikumi mkoani Morogoro.
Kiongozi huyo ni miongoni mwa wanakamati ya kufanikisha mazishi ya wasanii hao yanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam.
Miili ya marehemu ipo njiani kuletwa Dar es Salaam, itafikishwa muda wowote kuanzia saa 9 alasiri.
Miongoni wa waliokufa ni Issa Kijoti aliyeimba wimbo maarufu wa NICHUMU , NICHUMU TENA, MWAAH!
Miongoni mwa walioumia ni mwimbaji maarufu wa taarab nchini, Mwanahawa Ally ambaye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo.
Majeruhi wengine ni pamoja na Suzan Benedict, Zena Mohammed, Mwanahawa Khamis, Issa Khamis, Rajab Kombo, Haji, na Msafiri Mussa.
Asha Baraka ametaja namba zake ili watu wampigie kutoa michango ya fedha kufanikisha mazishi na kuzisaidia familia za marehemu.
Kwa mujibu wa mdau huyo wa muziki, fedha zitakazochangwa zitagawanywa sawa kwa familia 13 za marehemu.
Kama upo tayari kuchangia piga namba 0713 60 65 64, 0765 11 11 35, na 0787 60 65 64 utaongea na Asha Baraka.
Kama upo mbali na Dar es Salaam unaweza kuchangia kwa kutumia njia ya M-PESA kwa namba 0765 11 11 35.
Mwili wa aliyekuwa Meneja wa bendi hiyo, Nassoro Madenge, hivi sasa unaswaliwa msikitini Kibaha, mkoani Pwani, na baada ya hapo utazikwa huko huko Kibaha.
Miili mingine bado ipo njiani kuletwa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment