MWANAMKE nchini Marekani, Alice (59) hivi karibuni alipoteza
kumbukumbu kwa muda baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa na mumewe.
kumbukumbu kwa muda baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa na mumewe.
Hali iliyomtokea Alice ya kupoteza kumbukumbu ghafla kitaalamu inatambulika kama "Transient global amnesia” au kwa kifupi TGA.
Hali hiyo husababishwa na msukumo wa damu kwenye ubongo wakati mtu anapofika kileleni wakati wa kujamiiana.
TGA husababishwa na shughuli mbali mbali zenye stress lakini mara nyingi zaidi husababishwa na tendo la kujamiiana.
Baada ya kujamiina na mumewe, Alice alipoteza kumbukumbu yote ya maisha yake na alikuwa hana uwezo wa kuhifadhi kumbu kumbu ya matukio yaliyofuatia baada ya hapo.
Baada ya kumaliza kufanya mapenzi Alice na mumewe Scott walikaa kuangalia luninga.
"Niliona mambo hayako sawa niliamua kumuuliza leo siku gani?", Scott alisema alipokuwa akihojiwa na CNN.
Wakati aliposhindwa kujibu swali hilo rahisi, Scott alimuuliza mkewe jina la rais wa sasa wa Marekani, Alice alijibu "Bill Clinton".
Baada ya jibu hilo Scott alipiga simu hospitali kuita ambulance, Alice alipofikishwa hospitali haukupita muda mrefu watalaamu wa masuala ya ubongo waligundua kuwa Alice amepata ugonjwa wa TGA unaowapata watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 50.
No comments:
Post a Comment