Saturday, September 5, 2009

Mbowe ang'ara, Dk Slaa kupeta leo?

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umemchagua Freeman Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Mbowe ameshinda kwa asilimia 92.9 ya kura 457 katika uchaguzi uliofanyika jana, Dar es Salaam.

Mbowe hakuwa na mshindani,alipata kura 425,wajumbe 22 sawa na asilimia 4.8 walipiga kura za kumkataa.

Kura 10 ziliharibika ambazo ni sawa na asilimia 2.1.

Kwa upande wa Makamu wa Mwenyekiti, Bara iliyokuwa ikiwaniwa na watu watatu, Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi, alishinda kwa kupata kura 315 sawa na asilimia 69.

Arfi amewabwaga Sambwee Shitambala aliyepata kura 99 (asilimia 21.7), na Dk. Ben Kapwani aliyepata kura 40 sawa na asilimia 0.5 ya kura ni 456.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed aliibuka kidedea kwa kupata kura 243 sawa na asilimia 53 dhidi ya Said Mzee Said aliyepata kura 212 sawa na asilimia 46 ya kura 456,kura nne ziliharibika.

Matokeo hayo yaliyotangazwa na mmoja wa wazee wa Chadema, Bob Makani, yalipokewa kwa furaha na shangwe baada ya kutaja ushindi wa Mbowe.

No comments:

Post a Comment