Friday, September 4, 2009

Hi baby, hujambo?

KUNA mdau kanitumia ujumbe huu, kauandika kwa ajili ya mahabuba wake.
Hi Baby, Hujambo?
Nimekaa hapa mbele ya computer yangu nafikiria leo nikuandikie kwa lugha gani ili uelewe ninachotaka kusema.
Mwanzo nilitaka kuandika kwa kiingereza lakini nikasema mhh inawezekana nikakosa baadhi ya maneno matamu, nikaamua kuandika kwa lugha yetu ya Kiswahili.

Baby, ni jambo la furaha sana kupata nafasi hii nyingine kukuandikia kitu fulani, kuna watu saa hizi wanalia wameumizwa na wapenzi wao kwa njia moja au nyingine.

Kuna wengine muda huu wanafikiria kesho itakuwaje kwa sababu wamewaudhi wapenzi wao.

Kuna wengine wamekata tamaa ya maisha kwa sababu walijitoa sana kwa wapenzi wao wamekosa vyote walivyokuwa wanavifikiria.

Pole kwa kuongelea mambo hayo hapo juu lakini ni kukumbusha tu wajibu wako katika kuhakikisha mapenzi yetu yanaendelea kukua na yanadumu.

Kila siku unaposoma ujumbe wako ujue tu kwamba nimekufikiria kuliko jana kwa hiyo nakupenda zaidi, natamani uwe karibu yangu ili maneno ninayoandika nikuambie moja kwa moja ujisikie maalumu zaidi .

Pamoja na hayo mimi hapa nilipo naendelea vizuri, namshukuru Mungu tangu asubuhi mpaka sasa hivi umefika wakati wa kupumzika hakujatokea tatizo lolote ila moyo wangu unasikitika kwa nini sikukufahamu tangu miaka ileee nilipoanza kuwa na akili za kiutu uzima.
Mapenzi unayonipa sikuyapata huko kwingine kote,ninayapata sasa hivi ukubwani, natamani ingekuwa hivyo tangu mtoto hadi ninapoaga dunia .

Ahsante sana kwa mapenzi ya dhati unayonionyesha na kunipa, kwa kweli naamini mimi ndio mwanaume bora kuliko wote duniani.
Tukiwa na familia nitakuwa baba bora kuliko wote duniani nikiwa na wewe , kwa namna tunavyoishi sasa hivi nina ndoto na malengo mazuri sana kuhusu wewe, sijawahi kuwa na wasiwasi wowote mpaka sasa hivi .
Baby, naomba uendelee kuwa mwaminifu mvumilivu na mwenye malengo katika maisha yetu sote wawili , mie pia naahidi kuwa mwaminifu , mvumilivu na mwenye malengo katika maisha yetu.
Napenda kukuahidi kukupenda , kukujali na kuwa na wewe wakati wote wa maisha yangu.
Sijuti na wala sitajuta kukupenda, siwazi lolote baya kuhusu wewe, kama yalikuwepo basi yafute, anza maisha na mambo mapya kwa ajili yetu na watoto wetu.
Nakupenda sana , naomba niishie hapa, naenda kupumzika.

No comments:

Post a Comment