Daktari Arnold Klein anadaiwa kuwa ni baba mzazi wa watoto wawili wanaotajwa kuwa ni Michael Jackson, Prince Michael 1 na Paris.
Dk Klein ni mtu wa karibu na Michael na mama mzazi wa watoto hao, Debbie Rowe.
Daktari huyo wa ngozi amemtibu Michael kwa miaka 20.
Mama wa watoto hao ni muuguzi, alikuwa muajiriwa katika hospitali ya Dk Klein kwa miaka 23.
Dk Klein amekiri kuwa amewahi kutoa mbegu za uzazi kwa jili ya benki ya mbegu hizo lakini haamini kuwa ni baba mzazi wa watoto hao.
Klein pia amekiri kwamba, alimpa Michael dawa KALI ziitwazo, DEMEROL na kwamba Michael alizitumia siku alipoaga dunia, Juni 25.
Michael akiwa amembeba Prince Michael 1, debbie kambeba Paris
Michael na Debbie walikutana wakati mwanamuziki huyo alipokwenda kupata tiba katika hospitali ya Dk Klein.
Walianza uhusiano wa kimapenzi, wakafunga ndoa mwaka 1996, waliachana mwaka 1999.
Paris na Prince Michael 1 wakiwa na mdogo wao Blanket
Wakati wa shughuli ya kumuaga Michael, Paris alisema Michael ni ' The best father you could ever imagine'
Si hivyo tu alisema, anampenda mno baba yake.
Paris na Prince wamekuwa wakimuita Dk Klein UNCLE.
Wakati mamilioni ya watu kode duniani wakimuaga sehemu ya ubongo wake ilikuwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi.
Hadi sasa Michael Jackson hajazikwa, na haijulikani atazikwa lini.
No comments:
Post a Comment