Mtalaka wa Michael, Debbie Rowe akilia wakati mtoto wao, Paris, akieleza upendo wa baba yake kwake na namna yeye(Paris) anavyompenda.
Debbie na Michael walifunga ndoa mwaka 1996, waliachana mwaka 1999, walizaa watoto wawili, Prince Michael Jr(12) na Paris(11).
Mama huyo hakuhudhuria shughuli ya kumuenzi Michael iliyofanyika jijini Los Angeles, alishuhudia kupitia televisheni.
Wanaubeba mwili wa mdogo wao
Kaka wa Michael, Jackie na Jermaine wanafarijiana, pembeni yao ni baba yao mzazi, Joe
Usher Raymond akiimba kwa uchungu pembeni ya jeneza la Michael
Kaka wa Michael, Randy anamfariji mtoto wa kwanza wa mfalme wa pop, Prince Michael Jr.
Mwili wa Michael Jackson haujazikwa.
Maiti ya nyota huyo wa muziki duniani bado ipo mochwari na haijulikani atazikwa lini.
Kuna taarifa zinazodai kuwa huenda atazikwa baada ya ubongo wake kurudishwa, unachunguzwa ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Michael aliaga dunia Juni 25, saa 48 kabla ya kifo chake alikuwa jukwaani akifanya mazoezi kwa ajili ya maonyesho yaliyopangwa kufanywa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment