Saturday, July 11, 2009

Ni kweli?

KUNA mdau kanitumia matokeo ya utafiti kuhusu muda wanaotumia wanawake kuchagua nguo za kuvaa.
Matokeo ya utafiti uliofanywa nchini Uingereza umeonyesha kuwa wanawake hutumia muda mwingi sana katika maisha yao kuchambua makabati yao kutafuta nguo ipi ya kuvaa wakati wanapotoka majumbani mwao.

Kwa mujibu wa utafiti huo wanawake hutumia muda mwingi sana katika maisha yao wakitafakari nguo ipi ya kuvaa wakati wanapoenda makazini, kwenda 'Out', kwenye vakesheni au shughuli zao za kawaida za kila
siku.

Utafiti huo uliofanywa na kampuni kubwa ya maduka ya nguo ya Matalan ya nchini Uingereza ulishirikisha wanawake 2,491.

Utafiti huo ulifanywa kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 16 na 60 ulionyesha kuwa wanawake hutumia takribani dakika 20 kutoa uamuzi wa nguo ipi wavae kabla ya kutoka kwenda kujirusha mwishoni mwa wiki.

Wanawake hutumia dakika 52 kutoa uamuzi wa nguo zipi za kuchukua wakati wanapoenda vakesheni.

Wakati wanapokuwa vakesheni wanawake hutumia dakika 10 wanapoamka asubuhi kuamua nguo ipi ya kushinda nayo mchana na nyakati za usiku hutumia dakika 10 nyingine kuamua kivazi kipi cha usiku cha kuvaa.

Utafiti huo ulionyesha pia kuwa wanawake hutumia dakika 36 kuchagua nguo ya kuvaa wakati wa kujiandaa kwenda kwenye sherehe na maharusi.

"Kwa wastani wanawake karibia wote hujaribu nguo zaidi ya mbili kila siku asubuhi kabla ya kufikia uamuzi nguo ipi ya kuvaa" ulisema utafiti huo.

Wanawake wanaofanya kazi nao hutumia takribani dakika 15 usiku wa kuamkia siku ya kazi kuchagua nguo ya kuvaa wakati wanapoenda makazini, ulimalizia utafiti huo.

No comments:

Post a Comment