MSANII nyota wa nyimbo za kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Jide, a.k.a Binti Machozi, a.k.a Mama some food, a.k.a Comando amesema tuzo za muziki nchini, Kilimanjaro Music Awards hazimsaidii chochote hivyo hata asipozipata poa tu.
Jide amesema, anafanya muziki kwa ajili ya mashabiki na kuendesha maisha yake na si kupata tuzo hivyo Awards hizo si muhimu kwake!
Mama some food amesema, hawezi kulalamika kuzikosa tuzo za kili kwa kuwa anaamini wanaoziandaa wana vigezo vyao na wana mtazamo wao.
Msichana huyo mzaliwa wa Shinyanga yupo anahojiwa LIVE katika kipindi cha Leo Tena cha redio Clouds FM.
No comments:
Post a Comment