Friday, April 10, 2009

Kumbe Kardinali Pengo ni raia wa Vatican




NAMSHUKURU Mungu kwa kuniwezesha kufanya kazi ninayoifanya, na naamini ataniwezesha kuifanya hadi hapo atakapoamua yeye vinginevyo.

Nimewahi kuandika makala nyingi zikiwamo zinazohusu maisha ya watu wa hadhi, rika, na fani tofauti, ila sikuwahi kuandika makala kama niliyoiandika wiki hii.

Sikutarajia kama kuna siku nitaandika makala kuhusu kiongozi Mkuu wa dini yoyote Tanzania, hivyo nafarijika kwamba nimefanya hivyo wakati huu wa Pasaka.

Nilimpigia simu Askofu Mkuu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini kuomba idhini ya kuandika makala kuhusu maisha ya Raia wa Vatican, Kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Kardinali Pengo, aliponiruhusu nilifurahi.

Soma HabariLEO Jumapili wiki hii umfahamu Kardinali Pengo ametoka wapi, alifanya nini miaka ya nyuma, familia yake, na mambo mengine.

Kwa kifupi tu ni kwamba, wakati anateuliwa kuwa Askofu alikuwa Mhazini na Mkuu wa Seminari(Gombera) ya Segerea iliyopo Dar es Salaam, ni Raia wa Vatican lakini hataki kwenda kufanya kazi huko.

No comments:

Post a Comment